Yuko wapi rais Kikwete? Wako wapi viongozi wa nchi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yuko wapi rais Kikwete? Wako wapi viongozi wa nchi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 1800, Sep 9, 2012.

 1. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wadau naamini wote tunayajua mambo ya mauji ra raia wasio na hatia yanavyoendelea kiholela huku kukiwa hakuna nia ya dhati toka kwa viongozi wetu kuanzia wa serikali mpaka jeshi la polisi,bad enough kwa kua hao viongozi wanaouliwa sio ndugu zao,wanazidi kututia uchungu kwa kwa kutuona Watanzania ni mahayawani wa kutupwa kwa kuja na majibu ya kejeli na propaganda nyepesi juu ya mauaji yanayoendelezwa.

  Kauli kama za Chagongja,Tendwa,Nape Nnauye na jana Wassira kupitia Tbc,ni kauli za dharau kwa Watanzania kwa vile wanatuchukulia ni mahayawani tusiokua na tafakari hata kidogo kwa mambo yaliyo na majibu ya wazi kama matukio hayo ya mauaji yanayoendelea!nimeangalia video ya tukio la vurugu za Iringa,video ambayo nina amini serikali na jeshi la polisi wasingependa ionekane kwa Watanzania kutokana na udhalimu waliofanya na uongo wa kitoto wanaojaribu kutupa Watanzania,katika video hiyo labda mwanadamu aliye na upeo wa level ya kuku ndie atakaekubaliana na matamko ya kipropaganda mfu yanayotolewa na viongozi wetu kama Wassira na Tendwa!!

  Najiuliza kitu kimoja rais wetu Kikwete mbona yuko kimya hajatoa kauli hata moja kama vile mauaji haya ni halali kabisa!ni wazi kipindi cha mwalimu Nyerere mtu kama kamanda Kamuhanda na askari wote waliohusika na tukio lile kwa kua wameonekana wazi sasa hivi wangekua ndani ya mikono ya sheria!serikali yetu imeshndwa kutumia rasilimali zetu kuendeleza viwanda,kuendeleza elimu afya hata kulinda raia wenu mpaka mnabariki mauaji kwa sababu na propaganda zisizo na kichwa wala miguu.

  Wakumbuke Mwi Nyerere alijenga viwanda,aliboresha elimu kwa kilimo tu,hakugusa madini wala kulangua ardhi kwa wageni,wao wanagawana madini,wanagawa ardhi kwa kisingizio cha uwekezaji kumbe ni uchukuaji,wameua viwanda,wanadidimiza elimu kiasi cha wasiojua kusoma na kuandika imeongezeka (wanatengeza taifa la wajinga) bado hawaridhiki na sasa wameamua kuua raia wake bila hatia!ila wakumbuke kua bila kuchukua taadhari ukweli ni kua mwisho wa yote uko mlangoni,dalili za raia kuto ogopa wala kuheshimu vyombo vya dola hasa polisi,maandamano ya juzi ya waislamu yenye sauti kali mpaka waziri kusalimu amri,ni wazi sasa Watanzania hawako tayari kuendelea kunyanyaswa na wanajua haki zao zinakandamizwa na wachache!viongozi amkeni sasa kabla ya kuchelewa
   
 2. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,973
  Likes Received: 37,542
  Trophy Points: 280
  Jamaa hafai kwa nafasi aliyonayo.Yeye cha muhimu kwake ni kujijengea jina katika mataifa ya nje.Sijui anaota kuja kufukuzia ukatibu mkuu wa umoja wa mataifa?

  Tuna hasara kama taifa.
   
 3. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu kwa kweli inatia shaka, hasira na huzuni pia! yeye kama kiongozi mkuu wa taifa ilipaswa kua mkali waziri wa wizara husika na IGP pia, naamini nao wangekua wakali na kuwachukulia sheria wote wanaofanya uovu huo! Sasa yeye hasipokua mkali anategemea nani atamuogopa?

  Si kila mtu atakua anafanya madudu kwa kuamini kua mkuu hana muda wa kufuatilia mambo haya! Nakumbuka kipindi cha uongozi wa Mwl Nyerere, kuna vifo vilitokea kizembe na waziri wa mambo ya ndani kipindi hiko Alhaj Ally H Mwinyi alilazimika kujiuzuru bila kushinikizwa na hii yote ilitokana na uadilifu wa kiuongozi na ufuatwaji wa sheria chini ya Mwl Nyerere, lakini awamu hii kila waziri akifanya madudu tena ya wazi yeye ndie anakua mkali kwa wananchi na kejeli za dharau kama vile sijiuzuru,mtapata wapi waziri kama mimi!what a ****??!

  Naamini Mh K.i.k.w.e.t.e angekua mkali kwa mawaziri na watendaji wake tusingeyashuhudia haya yanayolipelekea taifa letu kwenye giza la chuki, uhasama na wananchi kuanza kutolieshimu wala kuogopa jeshi la polisi na serikali
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mheshimwa wetu mtukufu Edward Lowassa alishasema kua hii nchi haina uongozi, kila mtu anajifanyia anachotaka...boy was he soo right...Hii nchi ina Rais on paper kwamba kikatiba rais tunae lakini kiuongozi hatuna na hii nchi imeshamshinda...he knows that..the people surrounding him know that and wananchi know that as well..hapa tunasogeza siku tuu tuna count down to 2015
   
 5. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #5
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nduguyangu hihi nchi ipo auto pilot kwahiyo wala usishangae
   
 6. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #6
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Inamaana hao umoja wa mataifa watakuwa wajinga kama waTz kwa kuongozwa na mtu asiyejua matatizo yao?
   
 7. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #7
  Sep 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu fanya kuediti na uondoe neno mtukufu wetu maana kama ni utukufu ni kwako na si wengine kama fisadi huko kwenu ndo mnaowatusa ishia kujisemea wewe na siyo wengine
   
 8. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #8
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Umoja wa mataifa ni mbali sana huko,hapa hapa Africa mashariki tu sidhani kama kuna nchi itakayohitaji hata ushauri tu wa mkuu huyu mara atakapotoka kuna madarak
   
 9. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 9, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,872
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180
  ukimya wake ni ishara kuwa naye ni mhusika, tunachomwomba Mungu ni kuwa alikabidhiwa nchi hii salama na haiache salama. ukimya juu una lake jambo.
   
 10. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #10
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Amechanganyikiwa:A S-confused1:
  Anaogopa nguvu ya umma:behindsofa:
   
 11. Thanda

  Thanda JF-Expert Member

  #11
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,915
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mtukufu ni Mungu peke yake, hakuna mwanadamu yeyote aliye na utukufu na aezaye kutukuka..soma Isaya 48: 7-8
   
 12. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #12
  Sep 9, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  tuwekww hiyo video
   
 13. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Uko sahihi kabisa mkuu
   
 14. k

  kwitega Senior Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 166
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unayemwita mtukufu ni kwako wewe mwenyewe. usisemee watu wengine inawezekana unakula mafao haramu ya Richmwend na Dowananasi.
   
 15. t

  tenende JF-Expert Member

  #15
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Hakuna haki wala haki haitatendeka iwapo wafuatao hawatajiuzulu au kuchomolewa na Kikwete kupisha uchunguzi:1. Waziri Nchimbi;2. Mkuu wa mkoa wa IRINGA; 3. RPC;4. Mkuu wa wilaya;5. OCD; na 6. mkuu wa upelezi mkoa (RCO), 7. Chagonja.
   
 16. kavulata

  kavulata JF-Expert Member

  #16
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 3,181
  Likes Received: 1,536
  Trophy Points: 280
  Leo naitangaza CCM kama janga la kitaifa linalohitaji kushughulikiwa na wananchi wote wenye mapenzi na hamu ya maendeleo. Ubaya wa CCM unaonekana vizuri kama mtu atatoka nje ya nchi hii. CCM imeshindwa kuunda serikali inayoshindwa kusema:
  1. Acha rushwa, rudisha mali uliyoiba
  2. Usijenge hapo
  3. Usifanyie biashara hapo
  4. Usifanye biashara hiyo hapo
  5. Lipa kodi hata kama unauza sindano ya kuweka vishikizo kwenye shati
  6. Kata miti hiyo wape vijana VETA wachonge madawati watoto wote wasikae chini
  7. Sambaza maji ya mto huu na ule watu wote wapate maji
  9. Chimba visima hapo na bwawa pale wananchi na mifugo yao wanywe maji
  10. Jenga masoko kila kata watu wauze mazao na mifugo yao kirahisi
  12. Vijana acheni kuhamia mijini kama hamna kazi za uhakika
  13. Nununua boti na meli zile wakopeshe wavuvi wavue kisasa serikali ipate kodi yake
  14. Wilaya hii limeni zao hili kisasa na wilaya ile limeni lile na nyie huko fugieni mifugo yenu huko huko
  15. Bomoa jengo hili na lile hayakujengwa sehemu yake na hayana viwango
  16. Asilimia 3 katika mikataba ya madini haitoshi kama ni hivyo yaacheni madini yetu mpaka itakapotangazwa tena

  Msururu wa mambo ambayo serikali ya CCM inahitaji kutamka tu na kusimamia ili vilete tija kubwa kwa wananchi na taifa bila kuhitaji nguvu nyingi ama fedha za kigeni ni mengi. Kwanini CCM isitangaze kung'atuka kama alivyofanya muasisi wake alipotangaza kung'atuka wakati wananchi walivyokuwa wanafua nguo zao kwa mapapai mabichi? Hivi kweli viongozi wa CCM hawaoni aibu wanapotembelea miji ya nchi nyingine na kukuta mambo yanakwenda barabara? CCM sasa mtaji wao ni propaganda, wizi wa kura, nguvu za dola na rushwa, iko tayari kuona damu inamwagika ikilinda Tanzania isiangukie chama kinyinge, CCM itatutumbukiza katika janga baya sana kuonekana Afrika muda si mrefu kama itaendelea na spirit hii. Maana haitaweza kutunyamazisha wananchi wote mara moja kila mara, iko siku idadi ya watakaochoshwa na maisha haya itaongezeka, mungu si athumani yawezatokea mfadhili huko nje akakisikia kilio cha wanakandamizwa na CCM miaka nenda rudi, hapo ndipo janga kamili litakapotokea. Hebu ona Dar es Salaam iko kama gulio, kila mtaa umejaa nyanya, mitumba, chips, grocery. Mvua ikinyesha kidogo ndo usiseme, elimu duni, hospitali wagonjwa wako chini ya sakafu, nk. kwanini lakini CCM inahisi lazima ibaki madarakani?
   
 17. t

  thatha JF-Expert Member

  #17
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu umezidi kuipaisha CCM , kama hizo ndo zitakuwa sera za Magwanda.
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Sep 10, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Kama hiyo ndiyo vision ya CDM, tufwile nyambala!
   
 19. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #19
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tanzania hatuna rais wa nchi,hatuna viongozi wa nchi tunaviongozi wa ccm.ambapo wanachojali ni kulinda masilahi yao na familia zao. MUNGU IBARIKI TANZANIA.
   
 20. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #20
  Sep 10, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280

  Mfano mdogo tu wa uongozi bora - kama Mhe Kikwete angekalipia kwa dhati mauaji ya Morogoro sidhani kama kuna kichaa ye yote kama huyu Kamuhanda angethubutu kufanya mauaji mengine Iringa baada ya wiki mbili.

  Na sidhani kama kuna mediocres wake kama akina Nchimbi, Nape, Wassira, na Tendwa wangepata uthubutu wa kufanyia unyama huu kejeli kama hizo wanazotoa!!!

  Binadamu anauwawa kama kuku (hata kuku huwa anawekewa staha ya dua) lijitu linajiita mkuu wa nchi linakaa kimya kana kwamba hiyo habari haimhusu.

  Kweli ni kiwete wa akili!!!!!
   
Loading...