Yuko wapi Polepole, katibu wa itikadi na uenezi CCM?

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,055
Habari wanajf
Katika uchunguzi wangu nimebaini kuwa, licha ya kuwa ndugu polepole anang'ang'anizwa kukitumikia chama chetu, yeye naona moyoni make hajisikii kufanya hivyo.

Mtakumbuka kuwa kabla ya kuteuliwa kuwa DC huku Musoma na Baadae Dar, Polepole alikuwa miongoni mwa watu ambao walikuwa mahili Wa kujenga hoja katika masuala mbalimbali ya kitaifa, jambo lililopelekea ccm kumuona kuwa anawafaa katika kazi zao ingawa hakuwa mwanaccm.

Mara tu alipoteuliwa uDC akapotea kabisa, watu walihoji sana utendaji wake na ikabidi Raid amhamishe kumleta dar kama kumfurahisha lakini halo iliendelea vilevile. UVCCM tulimtetea kuwa yeye ameamua kuwa Wa kazi tu badala ya maneno, lakini kumbe tulikuwa tunajidanganya.

Kama CCM tuliamua kumubadilishia cheo, na kumpa Ukatibu Wa itikadi na uenezi, sasa hapa ndio amepwaya kabisa, Ni kama chama hakina MTU katika nafasi hiyo

Ushauri wangu! Polepole jitathimini kama unaona ngazi tunazokupatia kama chama hazikufai bora uachie na utuachie chama chetu.

Ni hayo tu, mwenye nyongeza unakaribishwa
 
Mara nyingi critic huwezi uongozi. Mfano TL akipewa nchi hata leo hataweza kuiongoza vizuri. Ku challenge na ku arrange ni vipawa viwili tofauti.
 
Mwenezi wa nini?? Ccm? Hahahahaaaaaa
Wewe ukipewa kazi ya kuuza gazeti la Uhuru utaweza? Je kusambaza uongo? Fitna? Majungu?Ngada? Ukiweza kuuza kopi tatu za gazeti la uhuru kwa siku moja basi unafaa kuwa katibu Mwenezi wa ccm
 
Watu muna naneno saana....kwani hilo gazeti haliuziki..????
 
Kwanza kabisa naomba nijulikane sipo upande wowote wa kisiasa, Ila naomba nimwelezee pole pole kidogo kulingana na upeo wangu mdogo

Pole pole ni MTU wa kupiga kazi kimya kimya hasa kwa siku za hivi karibuni hasa baada ya kupata UDC Ubungo, alikuwa anapenda kufanya mambo kimya kimya pasipo kutumia Media kama Madereva , ilifikia kipindi jamaa alikuwa anapiga kazi hadi SAA Tano usiku pale aneo lake la kazi kwa kusimama muda wote huku akisikiza na kusolve kero za watu bila kujali ukada,
Kiukweli Mimi nilikuwa namfuatilia kwa karibu sana na hata alivyotoka pale wananchi wa Ubungo walisikitika sana kwa jinsi jamaa alivyojitoa. Kwa Mara ya kwanza toka nizaliwe ndo niliona kazi ya Mkuu wa wilaya kwa jinsi jamaa alivyokuwa anafanya kazi yake, nikawa najiuliza hii ndo kazi ya mkuu wa wilaya au jamaa kapililiza majukumu yake.

Kulingana na haya Nina amini kule aliko Ajenda ya kupiga kazi kimya kimya inaendelea na Matokeo yanaweza kuonekana kwa jinsi wao wanavyojitasmin,

Hivyo kuwa Mwenezi kwa upande wake inawezekana anaendesha kwa jinsi anavyoona na jopo lake la Uongozi, Tuchukulie hata CDM, kwa wale ambao hawafuatilii sasa karibu mwenezi sizani kama anawika sana kiasi kwamba hata mtoto wa Primary anamjua huyu ni mwenezi wa CDM
 
Mara ya mwisho alioneka wapi na vipi mmetoa taarifa polisi ya kumtafuta; nawaza saa nane mchana
 
Hawezi tena kusimamia misingi ya haki na kuwa mchambuzi wa mambo ya kisiasa.
Ukisha teuliwa inabidi uwe mtu wa fitna na unafiki.
 
Kwanza kabisa naomba nijulikane sipo upande wowote wa kisiasa, Ila naomba nimwelezee pole pole kidogo kulingana na upeo wangu mdogo

Pole pole ni MTU wa kupiga kazi kimya kimya hasa kwa siku za hivi karibuni hasa baada ya kupata UDC Ubungo, alikuwa anapenda kufanya mambo kimya kimya pasipo kutumia Media kama Madereva , ilifikia kipindi jamaa alikuwa anapiga kazi hadi SAA Tano usiku pale aneo lake la kazi kwa kusimama muda wote huku akisikiza na kusolve kero za watu bila kujali ukada,
Kiukweli Mimi nilikuwa namfuatilia kwa karibu sana na hata alivyotoka pale wananchi wa Ubungo walisikitika sana kwa jinsi jamaa alivyojitoa. Kwa Mara ya kwanza toka nizaliwe ndo niliona kazi ya Mkuu wa wilaya kwa jinsi jamaa alivyokuwa anafanya kazi yake, nikawa najiuliza hii ndo kazi ya mkuu wa wilaya au jamaa kapililiza majukumu yake.

Kulingana na haya Nina amini kule aliko Ajenda ya kupiga kazi kimya kimya inaendelea na Matokeo yanaweza kuonekana kwa jinsi wao wanavyojitasmin,

Hivyo kuwa Mwenezi kwa upande wake inawezekana anaendesha kwa jinsi anavyoona na jopo lake la Uongozi, Tuchukulie hata CDM, kwa wale ambao hawafuatilii sasa karibu mwenezi sizani kama anawika sana kiasi kwamba hata mtoto wa Primary anamjua huyu ni mwenezi wa CDM
Si ndio maana unaambiwa amepwaya...Uenezi halafu tena kimya kimya Duh!
 
Back
Top Bottom