Kisu Cha Ngariba
JF-Expert Member
- Jun 21, 2016
- 22,130
- 48,862
Ni mda mrefu sijamsikia Waziri wa Fedha na Mipango akiongea. Tokea alivyojikoroga kuelezea ni nani atalipa kodi ya mihamala ya simu na benki hajawai kutoka na kuongea tena.
Bandari imekauka hila kila mwezi TRA inavuka lengo,aje atueleze TRA wanavuka vipi lengo wakati TPA ndio chanzo mama cha mapato hapa nchini?
Waziri njoo utueleze kwanini hospitali wanalia ukata,amna dawa,vifaa tiba wakati wizara yako inakusanya pesa na kuvuka malengo,je pesa hazifiki uko hospitali au MSD?
Waziri toka utuelezee kwanini Wizara yako kushirikiana na Wizara ya Elimu imeamua kupunjwa wanafunzi mikopo wakati kila mwezi mnavuka malengo? Mwezi August Bodi ilichelesha hela ya Field Practical kwa kisingizio cha uhakiki lakini sasa hivi wamesema bajeti ya mkopo ina kikomo. Wakati bajeti za miaka iliyopita bajeti ya mikopo ya elimu ya juu ilikua haina kikomo?
Philip Mpango tuka uko ulipojificha uje utuelezee kwanini hali ya nchi kiuchumi imekua mbaya hivi?