Yuko wapi Nyerere? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yuko wapi Nyerere?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MESAYA, Jan 22, 2012.

 1. MESAYA

  MESAYA Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  MCHINA Jiang Jing Ying aliyekuwa Tanzania mwaka 1969 kwa ajili ya kujenga reli ya TAZARA amefika nchini na kulia machozi baada ya kuona hali mbaya ya reli hiyo pamoja na wafanyakazi wenzake wa Kibongo ambao walijenga nao reli hiyo na kwa sasa wamestaafu.

  Anauliza HIVI HAKUNA NYERERE MWINGINE? na Tanzania haipo? Anasema kwao Nyerere ni kama Mtume au Nabii kama alivyo kwao Mao Tse Tung na kuuliza kama tunamuenzi kwa vitendo kiongozi huyu badala ya maneno!

  Anasema yeye huwa anatembea na picha za Nyerere na kusema Wachina wanampenda sana Nyerere na sera zake pamoja na Mao ambazo ndizo zimeifikisha China ipo!

  Anauliza Nyinyi Watanzania mna tatizo gani? mbona bado mpo nyuma sana?
   
 2. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,237
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  teh teh Jiang Jing Ying...pole sana, nchi hii saizi haifai, imeoza, inanuka tena ineanza kuvunda!!! kila kiongozi anajali masilahi yake binafsi,

  viongozi wako madarakani kwa uchu wa madaraka na mali. hakuna wa kuwakemea kama bosi kubwa ndo wamemuweka wao.. so usijali bwana JING YING.

  Nasikia enzi zile uchumi wa tanzania ulikuwa unafanana na wachina lakini leo duuuu (aibu yetu)

  NYERERE ALISHAKUFA MWAKA 1999, na fikra, matendo na mawazo yake nayo yamekufa. Kwa sasa tunatumia mawazo ya KIFISADI FISADI.

  POLE SANA BWANA JIANG JING YING...
   
 3. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Wakuu tumpe pole bwana jiang jing au tujipe pole wadanganyika?leo nimepita urafiki pale kweli hii nchi inasikitisha mno,kiwanda kimekufa kabisa,eti wamekodisha watu kwa mbele wauze malori,hii kweli ni akili?wapi ubungo spinning mill ya kule mabibo ndani,mmewapa wahindi kwa bei ya kutupwa,nao wamewapangisha msd kwa bei ya juu kabisa!what a shame!watanzania tumerogwa au?nakukumbuka sana mwalimu j.k.n kwa jitihada zako za kuikomboa nchi hii kifikra na kiuchumi,ila watanzania wa leo sio wale wa miaka ile,hawana uzalendo,wamebaki kua watumwa na washadadiaji wa siasa wakati uchumi wao na hatima yao na familia zao ni vilio vitupu
   
 4. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Shame be upon us and our children!!!
   
 5. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #5
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Nenda Butiama alizikwa yeye na azimio la Arusha
   
 6. Muhoka

  Muhoka Member

  #6
  Jan 24, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nyerere ameshakufa na yopo motoni anateseka, fikra zake za kidikteta, ubaguzi,udini nazo zimekufa.
   
 7. nimie

  nimie JF-Expert Member

  #7
  Jan 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Jiang Jing Ying si kwamba anataka kujua alipo Julius K. Nyerere. Anajua fika kuwa Nyerere alishakufa, ishu ya mahali alipo kwa uhakika ajuaye ni Mungu. Point ipo hapa "HIVI HAKUNA NYERERE MWINGINE?". Na ni kujichetua tu kuyazika mazuri ya Nyerere kwa mapungufu yake ya kibinadamu.

  Jiang Jing Ying, kina Nyerere wengine wapo wengi tu, tatizo njia za kufika alipofikia zimebanwa na mafisadi na viongozi makabaila, mabwanyeye, na wezi tena wasio na UZALENDO. Leo hii huwi kiongozi kama huna pesa za kuhonga, enzi zile kwenye kampeni watu walipigia kampeni kwa kutumia alama ya JEMBE na NYUMBA. Leo hii watu wanatumia fedha bana, na kwa kuwa wananchi ni walalahoi badi ndo wanatoa kura zao kwa wali, kanga, kofia, t-shirt na ahadi za peponi. Nchi imeshikwa na wahuni, nao wamekaba kila kona! Kwa taarifa yako alipoondoka Nyerere tu, tukaanza safari ya kurudi tulikotoka.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Jan 24, 2012
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Muhoka wa 10th January 2012.
   
Loading...