Nakumbuka tetesi hii kutoka kwa Dereva wake wakati akiwa Kagera: Kuna mama mmoja alichukua maziwa lita 5 eti anaenda kumpelekea nyumbani kwake, akamkuta anapiga deki, basi akaambiwa asubiri kidogo. Baada ya kumaliza Kaisi akatoka na Mugs mbili, akamwambia yule mama lazima wayanywe wao wawili mpaka yaishe kwani yeye anakaa peke yake na yule mama anajua hilo (Nasikia alikuwa Secretary wake). Basi zoezi likaanza Mama wa watu akajikuta anakunywa maziwa vikombe kibao bila kutaraijia na yaliyobaki yule mama aliambiwa aondoke nayo.
Kwa kweli alikuwa anaepuka vishawishi vya Rushwa za aina zote.