Yuko wapi Mungu?

Sun is Sun

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2024
Posts
1,152
Reaction score
1,696
Ninajiuliza kila siku bila kupata jibu
Yuko wapi Mungu, wakati watoto wanalala njaa?
Yuko wapi Mungu, wakati watu wanapoteza wapendwa wao kwa magonjwa wasiyoweza kutibu?
Mbona dunia imejaa vilio, lakini mbingu zimejaa kimya?

Wanasema Mungu ni mwenye huruma, lakini mateso haya yanaongezeka kila siku.
Wanasema Mungu anatuona, lakini mbona kila kilio kinaonekana kupotea hewani bila jibu?
Ni vigumu kuamini kuwa kuna nguvu ya upendo juu yetu ilhali dunia inateketea kwa huzuni.

Kama kweli Mungu yupo mbona hawatendei haki wale waliobeba upendo ndani yao?
Mbona wanaoomba sana ndio huumia zaidi?
Mbona wale wanaoteseka hawaonekani kusikilizwa?

Ninataka kuamini. Nilitaka kuamini.
Lakini kila siku ninapoona mateso ya wasio na hatia,
Imani yangu huponyoka na kuendelea kuamini kwamba hayupo.

Log-0ut.
 
Mungu ni akili yako…kwenye philosophia sio kila swali lazima liwe na jibu…over
 
Usisema Mungu pekee haitoshi.


Muhimu taja Jina la Huyo mkusudiwa .Mungu NI sifa ya uumbaji. Waumbaji WAko wengi .

Mungu Allah (waislamu.)

Mungu Yekova (wakristo

Mungu Zumaridi (......) n.k
Kama unauulizia Mungu zumarid Basi Huyo ako anapakatwa msubiri Kesho .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…