Ndg Bushman....hayo ni mawazo yako ambapo kwa kiasi kikubwa ni mawazo mgando sana! Nadhani wewe huijui siasa na sio mpembuzi hata kidogo kwani Ole Miria alitumia haki yake ya kikatiba kugombea jimbo lake la Simanjiro. Na katika kampeni zake alitumia busara sana kunadi sera zake kwa ufasaha na kwa umakini mkubwa mno kiasi cha Ole sendeka kumkubali na kuwataka wanasimanjiro kumchagua Ole Milya kama kura zisingetosha kwa Sendeka! Ole sendeka alizitaja sababu za kumkubali Ole Milia kuwa ni Mwanasiasa makini, asiemchafua mtu, sera zake ni makini, anabusara na hekima, mpole na mvumilivu lakini pia Msomi mzuri mwenye Masters ya Sheria! Anachoeleza hapa Bushman ni mambo ambayo Makamanda hawa wameyamaliza kitambo na kila mmoja anaganga yajayo! Itakumbukwa kuwa Ole Sendeka baada ya kushinda kesi; Ole Milia hakukata rufaa na baada ya Olesendeka kushinda kwenye kura za maoni Olemilya hakukata rufaa kama alivyofanya mgombea wa tatu Bw. Lenganasa Soipei. Mtazamo alioutoa Jethro ndio mtazamo chanya.....hatupaswi kuwarudisha watu nyuma badala yake tuwasihi na kuwatia moyo wasonge mbele daima! Tafakari!