Yuko wapi Mamluki James ole MILYYA?

bushman

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,411
743
HUYU KIJANA KUNAKIPINDI FULANI ALIFUNGUA KESI YA KUSHAMBULIWA NA MH.CHRIS OLE SENDEKA,AMBAPO WACHAMBUZI WA MAMBO WAKANENA KATUMWA NA LOWASA ILI AMHARIBIE OLE SENDEKA KWA SABUBU YA KUMWAMBIA LOWASA UKWELI KUHUSU RICHMOND,WANA JF HAKUCHUKUA FOMU YA KUWANIA UBUNGE KTK JIMBO LLTE?:israel::israel:
 
Ni wakati wake sasa wa kujipanga na kutizama upepo unakwenda wapi naye ajikite wapi ili ajue wapi pa kwenda kwa faida yake na kuwa kiongozi wa watu, ni muda pia wa kutumia busara na hekima ya juu kabisa kwani nae ni msomi mzuri tu na ajue jinsi ya kuchanganua mambo kwa upeo mkubwa
 
Ndg Bushman....hayo ni mawazo yako ambapo kwa kiasi kikubwa ni mawazo mgando sana! Nadhani wewe huijui siasa na sio mpembuzi hata kidogo kwani Ole Miria alitumia haki yake ya kikatiba kugombea jimbo lake la Simanjiro. Na katika kampeni zake alitumia busara sana kunadi sera zake kwa ufasaha na kwa umakini mkubwa mno kiasi cha Ole sendeka kumkubali na kuwataka wanasimanjiro kumchagua Ole Milya kama kura zisingetosha kwa Sendeka! Ole sendeka alizitaja sababu za kumkubali Ole Milia kuwa ni Mwanasiasa makini, asiemchafua mtu, sera zake ni makini, anabusara na hekima, mpole na mvumilivu lakini pia Msomi mzuri mwenye Masters ya Sheria! Anachoeleza hapa Bushman ni mambo ambayo Makamanda hawa wameyamaliza kitambo na kila mmoja anaganga yajayo! Itakumbukwa kuwa Ole Sendeka baada ya kushinda kesi; Ole Milia hakukata rufaa na baada ya Olesendeka kushinda kwenye kura za maoni Olemilya hakukata rufaa kama alivyofanya mgombea wa tatu Bw. Lenganasa Soipei. Mtazamo alioutoa Jethro ndio mtazamo chanya.....hatupaswi kuwarudisha watu nyuma badala yake tuwasihi na kuwatia moyo wasonge mbele daima! Tafakari!
 
Millya ni mamluki wa EL na ameumbuka kiasi cha kuficha uso wake kila akipita mbele za watu.Kilichompata millya ndicho kitampata Mashimbo(Mwanaume aliyeshindwa kumhudumia mke.Mke akamkimbia kwenda kwa mwanaume wa kweli).
 
I can tell who you are! Am I right?
Ndg Bushman....hayo ni mawazo yako ambapo kwa kiasi kikubwa ni mawazo mgando sana! Nadhani wewe huijui siasa na sio mpembuzi hata kidogo kwani Ole Miria alitumia haki yake ya kikatiba kugombea jimbo lake la Simanjiro. Na katika kampeni zake alitumia busara sana kunadi sera zake kwa ufasaha na kwa umakini mkubwa mno kiasi cha Ole sendeka kumkubali na kuwataka wanasimanjiro kumchagua Ole Milya kama kura zisingetosha kwa Sendeka! Ole sendeka alizitaja sababu za kumkubali Ole Milia kuwa ni Mwanasiasa makini, asiemchafua mtu, sera zake ni makini, anabusara na hekima, mpole na mvumilivu lakini pia Msomi mzuri mwenye Masters ya Sheria! Anachoeleza hapa Bushman ni mambo ambayo Makamanda hawa wameyamaliza kitambo na kila mmoja anaganga yajayo! Itakumbukwa kuwa Ole Sendeka baada ya kushinda kesi; Ole Milia hakukata rufaa na baada ya Olesendeka kushinda kwenye kura za maoni Olemilya hakukata rufaa kama alivyofanya mgombea wa tatu Bw. Lenganasa Soipei. Mtazamo alioutoa Jethro ndio mtazamo chanya.....hatupaswi kuwarudisha watu nyuma badala yake tuwasihi na kuwatia moyo wasonge mbele daima! Tafakari!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom