Yuko wapi jembe huyu tido muhando

Yuko wapi jembe huyu tido muhando

MSIPI

Member
Joined
Jan 31, 2012
Posts
18
Reaction score
5
Ndugu zangu wana Jf mnamkumbuka jembe huyu Tido Muhando? Sote tunakumbuka enzi za Radio Tanzania (RTD), na TVT. Sasa vyombo hivi vina sura mpya na muonekano mpya kabisa, hatutakuwa na fadhila katika hili bila kumkumbuka kamanda Tido Muhando. Ndugu zangu wana Jf nani anafahamu alipo jemedari huyu na anafanya nini? Na ni kipi kilichomkimbiza TBC.
 
Pale TBC alitimuliwa kwa sababu za kisiasa,kosa alilolifanya pale TBC ni kuwaita kwenye mdahalo wagombea urais ktk uchaguzi mkuu uliopita na ikaonyesha kwamba kampaisha SLAA kwa sana mpaka akamtia jamba jamba baba fulani ktk kukitetea kiti chake cha kuenderea kula bata pale maeneo ya magogoni!!!!!bila shaka ushampata.
 
Kwa habari zisizo rasmi ni kua Tido ameteuliwa kua mkurugenzi wa al jazeera swahili(Africa) ambayo makao makuu yake yatakua Nairobi Kenya!inasidikika serikali ilikataa kumuongezea mkataba Tido kwa kukaidi maelekezo ya chama magamba na kutekeleza kipindi cha mchakato majimboni ambacho kwa njia moja au nyingine kiliwaamsha wananchi ktk baadhi ya majimbo na matokeo yakawa mabaya kwa chama magamba!na tokea kuondoka kwa tido kumepunguza sana ufanisi wa tbc
 
Huo ndo ukweli halisi fitina za magamba ndo zilimuondoa TBC, ukitazama hata ubora wa habari za TBCCM umepotea wanachakachua taarifa hata zile tulozipata humu jf zenye fact na clarity. mfano taarifa ya Mwakyembe kwa vyombo vya habari TBC waliichakachua hadi aibu. Tido ni jembe haswa na kwa habari nilizozipata kwa vyanzo mbalimbali anakula shavu Aljazeera swahili na pia alikuwa suport kwa kijana JERRY ashinde kesi.
 
Back
Top Bottom