Yuko wapi Dr. Ndodi

hapo ndo ujue mganga hajigangi na hata yeye mwenyewe njaa ilikuwa inamxumbua ndo maana baada ya kupiga hela akapata kitambi...!! teh teh teh
 
Ameshavuna huyo baada ya kucheza na saikolojia ya watu maana alishagundua kwamba watz wengi tunapenda zaidi kutibu kuliko kukinga na kula lishe bora, ukimwambia mtu kupaka kitunguu kwenye ngozi kunaondoa vitu flani ata-apply faster ila hivyohivyo vitu ukimwambia ukila aina flani ya chakula huwezi pata hata umshikie bunduki hali
 
Huyu bwana alikuwa anapinga kunenepa na kuota vitambi, baada ya kupiga hela yeye naye kitambi kikaanza kutoka loh!! Mtanzania zaidi ya umjuavyo

hapo ndo ujue hata yeye njaa ilikuwa inamxumbua lakini baada ya kuzifuma za wagonjwa naye anamiliki kitambi...
 
bora mchawi kuliko mnafiki ilikuwa kumwona tu 15000 je dawa wewe alikupa bure

Daah..atakuwepo pale Magomeni(Itumbi Hotel) amepaki Range anakula bata tu..nlienda pale..dawa za kutibu fungus za miguuni nikambiwa laki 6,na hamsini..nilondoka bila kuaga..!!!
 
Hicho kigabachori sijui kiko wapi nilikua nacheka sana kakianza kupiga fix zake
 
Huyu Dokta yupo ila kysema kweli alisaidia watu sana hata mimi alinisaidia
 
Ndodi n mteule so acheni kuwanyoshea vidole wafuasi wa yesu!
 
Ndodi sio daktari ni mganga wa kienyeji tena std 7 kwao songea. Ukitaka muudhi muulize kasoma chuo gani. Sik hizi wapo vijana wasomi wana mpa za usoni kavu bila gloves.
 
nasikia ashafungua kiwanda cha kusaga unga wa sembe eneo la mwenda pole. Sasa anapiga hela tu.
 
kumuita huyu jamaa "Dr." ni sawa na kumuita mgambo "Inspector"
..only in tz kwakweli

Ungeuliza maana ya Dr ungefahamishwa tu, kuliko kuleta assumption zako zisizo na kichwa wala miguu.
 
Kwani kafanya nini xaxa? (kuna wengine sasa anaandika xaxa hapo ndio nachoka kabisa
 
iv kwanza alikua daktari kweli au alkua na idea za udaktari?? ningependa kujua hospitali aalyokua ameajiriwa

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Nilikua naogopa sana kuangalia vipind vyake maana alikua anafia chumvi kwenye kuelezea afya...mpaka unaeza ukadhan unakufa kesho lol
 

ni wanentu hawa,, wenyewe wanadhani kwamba wako inbox na washikaji zao... ipo siku hata application letter za kazi wataandika madudu hayo na baadae waje kulaumu kazi kuchukuliwa na wageni
 
Ungeuliza maana ya Dr ungefahamishwa tu, kuliko kuleta assumption zako zisizo na kichwa wala miguu.

zimpompolimpo kweli wewe, maana ya "dr." unaijua kweli wewe? pathetic layman!! ndo maana nimesema only in tz, maana hata mganga wa mitishamba ni "dr." hata kama haapi kwa hippocrates oath..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…