Jamani na Mzee wa CCM imeishiwa pumzi,aliyekuwa mlezi wa waganga wa Jadi Tanzania,kwamba chama Tawala wamuombe radhi Lowasa la sivyo PATACHIMBIKA HAPA NCHINI YUKO WAPI?siyo siri kila nikikumbuka yale maneno mmh,nabaki kujisemea mwenyewe hivi wenzetu hapa pakiharibika si wanarukia ndege kwenda nchi za nje?Mtu ametumia robo tatu ya maisha yake yoote serikalini na Chama alifikia hatua ya kusema HAKUNA LOLOTE LA MAANA LILILOTENDWA NA CHAMA TAWALA,mbona jibu la hayo halihitaji uelewa na elimu ya chuo kikuu,safari ya bus toka Mbeya-Sumbawanga ilikuwa siku mbili njiani,ukisema ufike hadi Mpanda siku tano,toka Mwanza kwenda Tabora njia haikuwepo,mmh siasa ni mchezo mchafu mno.