Yu wapi Dr. Slaa aliyekuwa akililia Utawala wa Sheria?

Yu wapi Dr. Slaa aliyekuwa akililia Utawala wa Sheria?

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Namkumbuka sana Dr Willibrod Slaa mara kwa mara katika hotuba zake, ampeni zake alikuwa akihubiri na kulilia utawala wa sheria katika nchi hii.

Nataka kujua huko aliko, msimamo wake ni upi juu ya matumizi ya sheria na ufuatwaji wa Katiba katika nchi hii kwa sasa, kama anaridhika nao ama la.

Je, anaona Katiba na Sheria za nchi hii zinafuatwa kama alivyokuwa anataka?

Bila kusahau suala la CAG na mambo mengine yanayohusu Katiba na Sheria.
 
Yupo Lumumba kwa kigezo cha Ubalozi. Unafiki unalipa
 
Huwezi kumuona huku Dr.Slaa... muda unakwenda mbio
 
Dr. Slaa nafsi itaendela kumsuta, kaisaliti demokrasia ya Tanzania ambayo akiapa kuitunza kwa nguvu zake zote na kwa akili zake zote.

Haya yanayoendelea nchini yatakuwa yanamfedhehesha sana ila sasa tumbo nalo je?, na kibaya sana ni kurudi kwa ile aliyoitafaninisha na toilet sasa anafanya nayo kazi apende asipende.
 
Wapinzani hawazingati Sheria wanajiona wajuaji wa sheria.

Ccm inaponda ponda katiba kwa miguu.

Mambo ni vururuvururu bora liende.

MWACHENI BABU AMALIZE UZEE WAKE SALAMA.
 
Back
Top Bottom