Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Keshaijabutege mbona umeweka malav lav ?
Ina maana moyo unaumia kumkosa Binti Cheusi
Huyu huwa anatokea kama mvua za masika
Kesho tu utamuona hapa
yuko hanemuni...imikulwa kwako!:A S-heart-2:Ninamsaka Cheusi, Cheusi wangu Mangala,
Mtoto kama mdosi, asopenda masihala,
Naona kama kaasi, sioni zake makala,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:First Ladi nahisi, umemficha mahala,
Ninazo pia tetesi, kwa Preta analala,
Rose mtingisha nyusi, yu wapi wangu Mangala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Kila mlo ukakasi, sipati hamu ya kula,
Cheusi njoo upesi, niepe huu msala,
MadamT mkwasi, ni yupi kwangu mbadala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Nakuuliza Demsi, ijibu hii makala,
Ninagona kama fisi, usiku nianapolala,
Chapachapa mikamasi, nalowesha matambala,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Mangala wangu Cheusi, nijuze pako pahala,
Nachekwa kandamnasi, mapenzi yanifanya ****,
Nitajitwanga risasi, nipumzike kwa Mola,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Kaditama yangu pasi, kwako Cheusimangala,
Una utamu wa tasi, laini kama salala,
Sukari kama fenesi, sehemu gani walala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
Keshaijabutege mbona umeweka malav lav ?
Ina maana moyo unaumia kumkosa Binti Cheusi
Huyu huwa anatokea kama mvua za masika
Kesho tu utamuona hapa
:A S-heart-2:Ninamsaka Cheusi, Cheusi wangu Mangala,
Mtoto kama mdosi, asopenda masihala,
Naona kama kaasi, sioni zake makala,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:First Ladi nahisi, umemficha mahala,
Ninazo pia tetesi, kwa Preta analala,
Rose mtingisha nyusi, yu wapi wangu Mangala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Kila mlo ukakasi, sipati hamu ya kula,
Cheusi njoo upesi, niepe huu msala,
MadamT mkwasi, ni yupi kwangu mbadala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Nakuuliza Demsi, ijibu hii makala,
Ninagona kama fisi, usiku nianapolala,
Chapachapa mikamasi, nalowesha matambala,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Mangala wangu Cheusi, nijuze pako pahala,
Nachekwa kandamnasi, mapenzi yanifanya ****,
Nitajitwanga risasi, nipumzike kwa Mola,
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
:A S-heart-2:Kaditama yangu pasi, kwako Cheusimangala,
Una utamu wa tasi, laini kama salala,
Sukari kama fenesi, sehemu gani walala?
Ni siku kenda sijala, kwa kumkosa Cheusi.
Hahaha! sawa mdogo wangu,ulitaka niseme nini haya si yale ya 'niitie mkeo' ?hihihi...pole sana ndugu Kashaijabutege....ukweli ni kwamba Cheusi na Uporoto01 walikuja kunitembelea hapa Yaeda wiki iliyopita na walinieleza wanaelekea Mang'ola....sasa anachosema hapo juu huyu Uporoto01 ni mapya....labda atueleze zaidi yu wapi huyu kimwana
Dah hapa napo mama umenigusa, natamani ungenitungia na mimi. Nasuburi mama!kweli umeishampenda, bila kujali weusi,
sasa watoa tenda, asakwe kama muasi,
huku wadondoka denda, kama mpanda farasi,
cheusimangala aja, kaa mkao wa kula
heri uketi kitako, ajapo iishe hamu,
sio urande makoko, asijekukuta homu,
kisha useme mnoko, eti kakupa pumu,
cheusimangala aja, kaa mkao wa kula
nasikia yuko mahali, hanemuni ndo shughuli,
tena hataki maswali, ya jaji wala wakili,
hawezi hata kuswali, yuko bize kama kuli
cheusimangala aja, kaa mkao wa kula
ngoja nitakurudia, kukujuza yalomsibu,
ikiwa ataridhia, kumchombeza kibabu,
majuto nitamtia, jamvini aje atubu
cheusimangala aja, kaa mkao wa kula
Dah hapa napo mama umenigusa, natamani ungenitungia na mimi. Nasuburi mama!