Youtube Kuna Mambo

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
219
Hapo mwanzo niliwahi kuandika kuhusu YouTube na hati miliki haswa za sanaa zetu hapa Tanzania, tangia hapo nimekuwa mpenzi kutembea YouTube kuangalia sanaa mbalimbali haswa za miziki kutoka Tanzania.

Jumapili hii nilikutana na vitu vingine vipya, nilikuwa natafuta nyimbo za Safari Sound ya Kenya, nyimbo inayoitwa "Karibuni Kenya". Naipenda hii nyimbo, nilikuwa namwonyesha mtu mwingine aliyebalii mfano wa nchi jirani inavyotangaza utalii wao kupitia YouTube.

Ukitazama picha za nyimbo hiyo utaona kuna picha za maeneo muhimu ya kiutalii katika nchi ya Kenya, mbuga za wanyama, misitu, mapori, watu, maziwa, nyumba za kale na kadhalika.

Kinachoshangaza katika nyimbo hii ya "Karibuni Kenya" ni picha moja ya Mlima Kilimanjaro. Kwa uzoefu wangu, picha hiyo imepigwa sana katika njia kuu ya kwenda Moshi mjini, lakini katika video inatangaza mbuga na hifadhi za Kenya. Kweli hii sio haki.

Mtu aliyetengeneza video hiyo na kuiweka anaitwa LamuBoy, pia kuna video zingine haswa za Chakacha, ambazo zina Alama ya Televisheni ya East Africa ya jijini Dar es Salaam, nazo ziko katika YouTube bila idhini ya East Africa TV.

Huko tunapoelekea siko, lazima tulinde mali zetu hata katika mitandao na kuiambia jamii ya mitandao kwamba vitu hivi na vile ni mali ya Tanzania au viko Tanzania na sio nchi jirani. Na video hizi ambazo zinatangaza mali na huduma za wengine kwa visingizio vya uhuru nazo tuongee na wamiliki wa tovuti hizi, pengine wazitoe au waangalie njia za kuweka alama maalumu kuhusu mwanzo au vyanzo vyake.
 
Umefanya jitihada gani kuhakikisha Mali na vitu vya kitanzania vinatunzwa na kuheshimiwa katiak youtube ?
 
Back
Top Bottom