Kujenga timu bora inahitaji.
1. Walipe vizuri
Assumption: Wako productive. Unawalipa kwanza ili wawe productive au wawe productive kwanza ndio uwalipe vizuri? Chicken and egg...!
Kuwalipa vizuri ndio inakuwaje? Ni fedha tu au na mazingira ya kazi? Ain't that simple, is it?
2. Washikishe malengo ya kampuni, wajione ni sehemu ya kampuni.
Ulimaanisha washirikishe? If that is the case, then I agree. Maono ya kampuni yanapaswa kuwa so deep entrenched kwa kila employee. Lakini kama anafanya kazi kwa sababu ya (1) then hana haja ya kujua maono kivile. Anakuwa anaishi sio kusukuma maono per se bali anafanya kazi zake zamwezi huu ili ATM isome!
3. Waheshimu, omba ushauri kwao inapo idi.
Waheshu kweli, Ndio sura ya biashara kwa wateja. Ila kama hawajiheshimu hii itafeli tu!
Utaomba ushauri kama wana value ya kuongeza au cha kushauri. Kama ni vilaza kuomba ushauri ni suicidal mission!
4. Wape mafunzo. Trainings za soft skills, Digital, Sales, marketing Nk.
Hii ni kama wana mpango wa kukaa. Unagharimika na mafunzo unawanoa wakiwa kwenye shape bora, wanasepa kwenye dau kubwa zaidi.
5. Pamoja na kuwa ni wafanyakazi lakini fahamu ni binadamu
Kweli kabisa, na kuna binadamu wa tabia nyingi tofauti, nzuri na mbaya!
6. Kujenga timu bora mpe kila mtu majukumu yake, Fanya waamini wanaweza kutatua tatizo bila kulifikisha juu.
Kuweka majukumu wazi (Clear delegation of authority) ni jambo muhimu. Niongeze tu unapowapangia majukumu lazima uwape mamlaka ya kutekeleza majukumu hayo. Ila tena kumwamini mtu asiye makini na mamlaka ni tatizo, atayatumia malaka vibaya tu!
Ninachojaribu kusema ni hiki: Hatua ya kwanza kujenga timu ni kupata watu sahihi ambao watakuwa watafuta sio kijiwe cha kupatia mia mbili mia tatu, bali sehemu ambayo wanataka kuwekeza moyo wao na ujuzi wao, ili kuungana na mwajiri kujenga anachotaka kujenga. Kwao hawa malipo ni compensation tu ya wao kuwa sehemu ya ujenzi wa maono.
Hawa kuwapata duniani, sio kazi rahisi. Hawa kuwapata Bongland, ni mziki mnene!
Ila ukiwapata, hatua tajwa inakuwa rahisi kwenda nazo japo sio mteremko kama inavyoonekana!
IG @adiuta_biz
π