Lukolo
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 5,143
- 3,212
can it be said that African intellectuals (pardon the generalization) are busy doing research, writing papers to be published in peer review magazines? While some are busy writing proposals to get funding for the next project?
Well, it might be very true that intellectuals are busy with researches and publications, but what else could they do? Hakuna anayewatumia, hawana kazi nyingine zaidi ya hiyo. Hata consultancies za kawaida kabisa ambazo wangeweza kuzifanya yanapewa makampuni na watu wa nje, sasa wasomi wa Tanzania wafanye shughuli gani zaidi ya kuandika research proposala na kupublish paper? Suala la research si la wasomi wa nchi zinazoendelea tu, bali hata katika nchi zilizoendelea wasomi wapo busy kufanya research. Lakini wenzetu wale matokeo ya research yakishachapishwa kwenye hizo peer reviewed journals, yanachapishwa pia kwenye magazeti ya kila siku. Mara ngapi tumesoma magazeti na kusikia kwenye TV wakitangaza matokeo ya research yaliyochapishwa kwenye journal fulani? Lakini hapa kwetu mlisikia lini vyombo vya habari vikireport matokeo ya utafiti uliofanyika nchini?
Kama matokeo ya tafiti hizi yangeripotiwa kwenye vyombo vya habari, ina maana kila mtu ndani ya nchi angejua ni nini wanaweza kufanya kwa ajili ya kuboresha hali za maisha ya watu wao au kutatua baadhi ya matatizo yaliyopo katika nchi. Lakini hapa kwetu, research ikishachapishwa kwenye hiyo sijui internation journal of economic and development ndiyo basi, findings zake zitatumiwa na mataifa mengine kuboresha kwao na si taifa letu.
Tuna viongozi ambao ni wavivu kusoma kupita kawaida. Na solution nyingi za matatizo yanayoikabili nchi ni zile za muda mfupi (adhoc solutions) ambazo mtu binafsi let say waziri ndiyo anatoka tu na wazo na anaagiza lifanyiwe kazi. Ndiyo yaleyale ya mabilioni ya Kikwete, yaliishia wapi? Hatuna utamaduni wa kusoma na kujua wenzetu India kwa mfano hivi sasa wana advance kwa kasi economically wamefanyeje? Ukitaka kuprove haya, nenda kwenye website za wizara mbalimbali, utashangaa kwamba hazijajisubscribe kwenye journal hata moja. Haya ni maajabu. Wizara ya Elimu kwa mfano ilitakiwa iwe ina subscription kwenye Journal za mambo ya elimu, kwa ajili ya kupata up to date information za research zinazofanyika kwenye nchi nyingine na nchini, ili kuboresha elimu nchini. Wizara ya kilimo, vivyo hivyo. Lakini hapa kwetu ni bora liende tu. Ndiyo yale ya akina Mngai kuibuka na masomo ya PhysicsChemia.
Hakuna mtu ana muda wa kusoma. Na ukitaka kujua kwamba serikali haifagilii matumizi ya tafiti, angalia kwenye fungu la pesa linalotengwa kwa ajili ya research. Hata REPOA ambao walikuwa ndiyo agent mhimu wa research za kukabiliana na umaskini sasa hivi wameminyiwa fundings.
So kwenye suala la wasomi kufanya tafiti na kuandika proposal za project mimi sioni kama kuna shida, shida ni watumiaji wa hayo matokeo ya tafiti zinazofanywa.