You know what? it's like to love someone totally and completely

Sham777

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
295
1,000
Kipindi nipo darasa la Sita shule moja jijin mbeya Kuna mwanafunzi wa kike alihamia darasani kwetu alikuwa anaitwa Innah.. Alikuwa ni mzuri sana, hakika ni mzuri hatari. Na ndio mara yangu ya kwanza kumpenda Binadamu wa kike. Innah alikuwa anatokea familia ya kitajiri kutokana na mazingira niliyo yaona. Hasubui aliletwa shule na usafiri private mbaka Geti la shule ila jion alipanda daladala ivyo ndio ilikuwa chance yangu pekee ya kuongozana na Innah sababu wote tulikuwa tunatokea sehem moja ila vituo tofaut vya kushukia.

Innah alipata marafiki wengi shulen pale (Chawa) hivyo ilikuwa ni nadra sana kumkuta peke yake mda wote alikuwa amezongwa na marafiki sababu kubwa alikuwa analipa Bills mida ya Break, kuwanunulia chakula, ice cream na vitu vingine vidogo vidogo.


Siku zilivyo zidi kwenda ndipo nilipo zidi kuona Uzuri wa Innah, hakika alizidi kupendeza zaid na zaidi na mim ndipo nilimpenda zaidi na zaid mbaka kupelekea kila siku namuota ndotoni nikiwa nimelala.. Kipindi icho sikuwa na uwezo wa kuongea na mwanamke face to face nilikuwa nina aibu sana pia nilikuwa mkimya sio mwongeaji hata kwa mtu nilie mzoea. Hii ilipelekea kukosa marafiki shuleni pale na kuishi kipweke sana.


Mda wa kurudi nyumbani ulipo fika mim na Innah tukawa tumeongozana kuelekea kituo cha basi, njian hatukua na stori ila tulipo fika stand hakukuwa na basi hata moja siku iyo kulikuwa na mgomo wa daladala. Tulikaa pale stand zaidi ya saa zima tukisubiri usafiri pamoja na wanafunzi wengine bila mafanikio yoyote..

Ndipo nikamwambia Innah anifate, karibu na kile kituo cha daradara kulikua na ofisi za serikali na ndipo alipo kuwa anafanyia Mzazi wangu kazi. Tukafika pale nikasalimia wafanyakazi wenzake nikakutana na mzazi nikamwambia tumekosa usafiri sababu kuna mgomo madeleva wa daladala. Baada ya dkk 10 mzazi alikusanya vitu vyake na ulikuwa mda wa kufunga ofisi umesha fika ivyo wote tukaenda kupanda gari la ofisi kipindi icho wafanyakazi wa serikali wanarudishwa makwao na magari ya ofisi (walikula sana bata), Innah alipo fika kituoni kwake alishushwa na mim namzaz tulienda kushushiwa nyumbani getin.


Kesho yake ilikuwa siku ya Jumamosi hivyo hakukuwa na shule mbaka Jumatatu. Nilimiss sana shule sio kama nilikuwa napenda shule rahh ila nilikuwa nataman nikamuone Innah..


J.tatu ilifika hasubui kama kawaida nilikuwa nimemiss sana kumwona Innah, weekend kwangu huwa inakuwa ndefu sana bila kumwona Innah. Sikufanikiwa kumwona Innah Mstarini (Assembly Arena) kwa sababu wanaume tunakaa upande wetu na wanawake wanakaa upande wao.. Ila tulipp ingia darasan Nilistaajabika Nilimwona Malaika i saw an Angel of that am sure, macho yetu yaka gongana and She smiled at me alikuwa mzuri zaidi zaid ya siku zote kama nilivyo sema mwanzo kila baada ya siku Innah alizidi kuwa mzuri zaidi na zaidi na vile nilikuwa sijamuoana siku mbili ndivyo uzuri wake uliongezeka mara mbili.


Darasani mim nilikuwa nakaa dawati la nyuma kabisa na Innah alikiwa anakaa dawat la mbele. Wakati vipindi vinaendelea nakumbuka tuligongana macho zaidi ya mara tano na Innah alikuwa anageuka geuka nyuma na haikuwa kawaida yake mwanzo..


Ulipo fika mda wa mapumziko (break time) mida ya saa nne Innah alimtuma moja wa Chawa wake aliniletea mfuko ndani yake ulikuwa una Pringle's nilishangaa sana kwanini imekuwa hivi ila nilifurahi sana siku iyo. Na ilipo fika jion mda wa kutoka Shule mim na Innah tuliongozana kama kawaida yetu ila siku iyo ilikuwa tofauti kidogo tulipiga story njian tukielekea kituo cha daradara, na tulipo fika hatukupanda daladala tulisimama pembeni na kuendelea na storu zetu zaidi ya saa zima..

Na baada ya kulizika tukapanda daladala ilikiwa hiace tulikaa zile seat za wanafunzi wanaitaga bansen burner. Nilishangaa baada ya kuona Innah kapitisha mkono wake begani kwangu (mara nyingi hii huwa inatumika kwa marafiki kila mmoja anapitisha mkono begani kwa mwenzake). Wakati tunaendelea akatoa biscuits tukawa tunaendelea kula mdogo mdogo. Nilihisi gari linakimbia speed ya jet kwani lilitumia mda mdogo sana mbaka kufika kituoni anaposhukia Inna siku zote.

Alishuka nikampa begi lake maana nilikuwa nimelishika mim alinipa nikalie yeye alikalia sweeta lake. Kwa wale alio wai kaa kwenye bunsen burner ya daladala wameelewa kwanini nilikalia bagi lake.. Nilitaman nishuke ila ilikuwa haiwezekan sababu kulikuwa na vituo kama viwili mbele ili nifikie na mim kituo changu na Iyo siku ndio ilikuwa Mwisho wangu wa kumwona Innah..


Siku iyo ilikuwa ni siku yangu ya furaha sana hata nilipo kuwa nyumban nilitaman kesho ifike haraka sana ili niwai shuleni nikamwone Innah kama ilivyo kuwa kawaida. Nakumbuka nilimwomba mzazi hela usiku ule na mim nilinunua chocolate moja pamoja na pipi toffi za kutosha tu kipindi icho ndio zilikuwa pipi za kishua zilikuwa zinauzwa tsh 20 wakati nyingine ilikuwa tsh 10 adi tsh 5.


******

Kwanini nimesema Siku ile wakati Innaha anashuka ndio ilikuwa mwisho wangu wa kumwona..


Wakati Innah ameshuka kwenye daladala alipo kuwa ana vuka barabara aligongwa na gari alichukuliwa na kukimbizwa hospital ya Rufaa ila alifia njian.. Siku weza kujua siku ile sababu daladala tulio panda ilikuwa imesha ondoka eneo lile..


Vaa kiatu changu.

"Picture" unampoteza rafiki yako mpya unae mpenda kupita maelezo..


"Picture" Unampoteza mtu ambae huwezi kumkosa hata kwa siku moja na huji kumwona tena maisha yako yote..


"Picture" mtu ulie zoea kumwona kama pambo lako darasan unakuja kumwona kwenye Jeneza akiwa ajielewi tena..


R.I.P Innah nitakupenda milele


NB: Innah sio jina lake halisi. Deleva alie mgonga alifanikiwa kukimbia hakupatikana tena. Pia mmoja wa marafiki zake Innah (classmate) alikunywa sumu baada ya kupata izo taarifa akafariki.. Kwa tulio soma wote wanakumbuka huu msiba wa shule..


Madeleva mjitahidi sana kuwa makini pindi mnapo endesha magari yenu mabarabarani ili kupunguza ajari zinazo tokana na uzembe. Tulipoteza classmate wawili kwa uzembe wa mtu mmoja..


Mwisho...
 

Depal

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
14,349
2,000
R.I.P Innah na mwenzako
Mhh!! Mkuu STD 6 mshaanza kupata hisia za dizaini hiyo?
 

Bella Ciao

JF-Expert Member
May 28, 2019
1,746
2,000
Aisee innah wetu..

ila mkuu kwa mfano ndio unamuhadithia msela story hivi alafu huyo demu bado yupo hai lazima tu atamtamani
 

Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,173
2,000
pole sana mkuu

no matter what ikifo kinauma jamani

kisikie tu kwa jirani yako kisikukute
 

Mcqueenen

JF-Expert Member
Nov 2, 2019
987
1,000
First love tena ya utotoni bana daah!! huwa ni the strongest believe me.
Nimekuwa na lovers wengi lakini I can say nliowaPENDA kweli hawazidi wanne.
ila yule nliempenda darasa la sita anaitwa pendo although tushapotezana baada ya kumaliza la saba but i swear hata nikikutana naye nimeshaoa,nikakutana naye ameshakuwa kilema hana jicho moja na mguu na uso uliungua tindikali...walahi namuacha mke namuoa pendo.
Na nimetumia jina lake sahihi ili kama niyeye akisoma hapa please PM me.
 

Sham777

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
295
1,000
First love tena ya utotoni bana daah!! huwa ni the strongest believe me.
Nimekuwa na lovers wengi lakini I can say nliowaPENDA kweli hawazidi wanne.
ila yule nliempenda darasa la sita anaitwa pendo although tushapotezana baada ya kumaliza la saba but i swear hata nikikutana naye nimeshaoa,nikakutana naye ameshakuwa kilema hana jicho moja na mguu na uso uliungua tindikali...walahi namuacha mke namuoa pendo.
Na nimetumia jina lake sahihi ili kama niyeye akisoma hapa please PM me.
Aisee hii comments ina hisia hatari.. First love huwa haifi hata siku moja na huwa aijalishi ni mtu gani awe mzuri au mbaya lazima umpende tu kivyovyote.. Ila hizi relationship za ukubwani ndio za uwongo sana sababu zinakuwa zime base kwenye Sex, hela , na mambo mengine ya hovyo ....

Hope utakutana na Pendo siku moja..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom