Chakula kwa Fikra Zako: CCM wamefanikiwa jambo moja ambalo sikulidhania linaweza kufanikiwa miezi michache tu nyuma; wamewachagulia wapinzani mgombea wao wa Urais, timu yake na mashabiki wake na kulazimisha upinzani (hasa CHADEMA) kubadilisha wagombea wake na kuwapokea kwa furaha waliotolewa kama zawadi na CCM kwao.
Kama kweli - alivyodai Lissu - kuwa CHADEMA walishampitisha Dr. Slaa kuwa mgombea wao wa Urais kwenye kikao cha Kamati Kuu basi kumuondoa yeye (aliyekuwa anahofiwa sana na CCM labda kuliko mtu mwingine yeyote miaka hii mitano) ni mkakati ambao umefanikiwa kupitiliza. Leo wana CDM (sijui kama ni wengi au la) wamejipanga kushangilia mapinduzi ya kimkakati waliyofanyiwa na CCM wakiamini kuwa wamepewa zawadi.
Leo mtu aliyekijenga chama na kupigwa pamoja nao anaonekana hana mpango ati ni kikwazo cha "mabadiliko" wakati mtu ambaye hajawahi kuwa na rekodi ya mabadiliko au hata kuutetea upinzani anahusishwa na mabadiliko! Jeraha hili la upinzani haliwezi kuponeshwa na wale wale waliosibabishwa; tuliambiwa "akili ndogo zisitawale akili kubwa"... sasa siyo tu akili ndogo zinatawala akili kubwa; akili kubwa zenyewe hazijijui kuwa ziliwahi hata kuwa akili kubwa!
Vyovyote vile itakavyokuwa CCM itaendelea kutawala ama kupitia Magufuli au kupitia Lowassa. Hili wapo ambao hawataki kuamini ndilo limetokea huku wenyewe wakiamini kuwa wanapigania "mabadiliko". Kuigeuza upande mmoja wa shilingi ukasema "umebadilisha" ni kweli; lakini hujabadilisha shilingi!
Hapa CCM wametutia kidole...
Cha macho!.. hata hatuoni tena.
MMM
Upo Tanzania? Issue siyo Lowasa Vs Magfuli au Ukawa Vs CCM. Issue ni Change Vs CCM and my best choice is Change. Period.