Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga (CHADEMA) Mheshimiwa Yosepher Komba ametembelea hospitali ya teule ya Muheza ambapo alipata nafasi ya kuona jinsi wagonjwa wanavyopatiwa huduma katika hospitali hiyo.
Pia Mheshimiwa mbunge alitembelea katika wodi ya wazazi ambapo alitoa msaada wa vifaa na zawadi kwa akina mama waliokuwemo katika wodi hiyo. Katika ziara hiyo aliambatana na mwenyekiti wa BAWACHA mkoa wa Tanga Bi. Aminata Saguti pamoja na wanachama wengine wa CHADEMA.