Yesu yupo Galaxy nyingine, atachelewa!

Jumong S

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
7,377
10,640
Vitabu vyote vya Biblia na Kulani vinaamini kuwa Yesu atarudi kwa ukombozi au kuufanya mwisho wa dunia.

Studies zinaonesha yupo Sayari nyingine huenda ktk Galaxy ya Nebula au hii ya Milky way akifanya ukombozi kwenye sayari zenye viumbe kama wanadamu wa dunia hii.

Tukumbuke kuwa, kwa mujibu wa NASA, Universe ina Galaxes zaidi ya bilioni 100 hii ni kutokana na studies za lensing au telescope za sasa hivi ambapo huko mbeleni zikiwa improved, galaxes nyingine kwa mabilioni mengi zitagundulika. Katika Galaxy ya Milky way tuliopo sisi, ina maelfu ya sayari ambazo zina mfano wa dunia yetu na zinaaminika kuwa na viumbe hai kama sisi.

Sasa kwa hesabu ya makadirio kila galaxy yenye mabilioni ya sayari inakadiliwa kuwa na sayari zenye maisha. Viumbe hao wenye ubinadamu nao wanafikiriwa kumkosea muumba na hivyo huenda Yesu yupo huko pia akiwakomboa. Hesabu zinaonesha itachukua muda mrefu sana kuzimaliza.

Haifahamiki ataanzia sayari gani au galaxy gani kuwarudia na kufanya unyakuo. Hivyo zamu yetu ya unyakuo baada ya ukombozi wa sayari nyingine itachukua muda mrefu. Kikubwa jiandae ufe vizuri, maana kwa kizazi cha leo kuifikia siku ya unyakuo ni ndoto.

Ishi kama mwisho wa dunia ni siku yako ya kufa. Tenda mema, toa sadaka kwa wahitaji (epuka kutoa sadaka kwa makanisa ya wajasiliamali wanyonyaji) na ishi purpose yako!!

Kila la kheri
 
ha ha ha! wazee wa kujikanyaga mara yupo mbinguni amekaa kuume kwa baba! mara kwenye galaxy! ilimradi umefata upepo tu hata hujielewi tangu lini vitabu vya dini vimegusia kuna galaxy,sayari au maisha nje ya dunia yenye ufanano na dunia..?
 
Sayari nyingine zimegundulika viumbe wake hawajagundulika anafanya ukombozi wa nini sasa!?..
 
Maandiko yanasema kuwa ni sayari ya Dunia pekee ndiyo iliyotenda dhambi, sayari zingine zipo kama kawaida na yesu huenda kuwatembelea na kuonana nao kama ilivyokuwa sisi mwanzo katika bustani ya Edeni kabla ya kutenda dhambi, hivyo huo ukombozi wa sayari zingine unatoka wapi! ni Dunia pekee ndio inasubiri kukombolewa. hao wanaosema hivyo ni wale wanaojaribu kujipa moyo ili waendelee kufanya anasa.
 
Haha yaani we jamaa, nimependa ulivyohotimosha ila kule juu kuna mkanganyiko mwingi sana.
- Una uwakika gani kwamba kuna viumbe vingine katika sayari zingine ambazo ziko earth like habitable planets?
- Je viumbe wote ni lazima wawe kama binadamu? Ya kwamba sisi ni carbonic beings je hakuna aina nyingine ya beings mpaka iwe kama binadamu?
- What kind of assurance uliyonayo kuwa Yesu ndiye Mkombozi wa universe nzima? (Here give a biblic facts) What if kama viumbe vya kwenye galaxies zingine navyo vina miungu yao huko?
Nasubilia majibu yako kwa hamu mkuu
 
Yesu yupo sayari ya Venus anapata good time, baada ya mateso makali, na inasemekana hiyo sayari INA utajiri wa kufa MTU,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom