Yesu mzungu, shetani mwafrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yesu mzungu, shetani mwafrika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaitaba, Oct 19, 2009.

 1. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #1
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wanaojua maandiko, naomba msaada wenu

  Inakuwaje Yesu acholwe akiwa wa kizungu, lakini shetani anachorwa akiwa wa kizungu?

  Je huu sio udhalilishaji kwetu waafrika?
   
 2. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #2
  Oct 19, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  swali halieleweki?
   
 3. r

  ronteru New Member

  #3
  Oct 19, 2009
  Joined: Oct 3, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hayo mambo ni controversial ni kuyaacha kama yalivyo. Tuangilie dini zetu zinatwambiaje. Kuna Mungu au laa? Siyo lazima kukubali kuwa kuna Mungu kwa sababu anamuona baba yako anaenda kanisani. Kanisani bilashaka nikama mahali pa kujumuika (socializing) kwa watu wasiopendelea kujumuika kwenye fujo kama kwenye disko la vijana walevi labda. Cha msingi ni mtu kuwa na roho safi yaani ubinadamu kwako na kwa wenzako na siyo utu. Ukiweza kumsaidia mtu, hutukani, nuibi, huchukui mke anu mme wa mtu, unaheshimu na hmsikiliz mkubwa na mdogo bila kubagua. Kwa hayo yote basi utakuwa umeokoka na siyo lazima uende sijui kwa kakobe au wengine et ili uokoke.

  Waliotuletea dini hizo wenyewe hawaendi kanisani lakini hawaishiwi kila siku wanatuletea misaada nasi kwa ulafi tunaifisadi na kuweka kilemba cha ukoka kwa kujifanya walokole kumbe wezi wakubwa.
   
 4. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #4
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kwa wale wanaojua maandiko na kufuatilia picha na sanamu za yesu na shetani, utakuta Yesu anacholwa akiwa wa kizungu, lakini shetani ucholwa akiwa ni mwafrika, je sisi waafrika ni sawa na mashetani na wazungu na Yesu ni sawa na wazungu?

  Au ni udhalilishaji!!!

   
 5. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #5
  Oct 19, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 50,922
  Likes Received: 23,561
  Trophy Points: 280
  ????????????????? Agrrrrrrrr???????????
   
 6. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #6
  Oct 19, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,366
  Likes Received: 661
  Trophy Points: 280
  Wee,usituletee bangi humu ndani,uzungu na uafrika wote upo ndani ya uwezo wako,ukitaka kuwa mzungu unakuwa mzungu,ukitaka kuwa mwafrika unajiafrika tuu,kwanza wapi umeiona hiyo michoro,hujawahi ona sanamu za yesu wa mpingo?au unaandika tu ?Hii inaonyesha jinsi gani hujikubali!!
   
 7. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #7
  Oct 19, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Juu kabisa nimesema kuwa, picha za Yesu na shetani, sio vinyago,

  Wewe ndo haujikubali maana unakubali sisi tufananishwe na shetani, bali wao wajifananishe na Yesu.
   
 8. JS

  JS JF-Expert Member

  #8
  Oct 19, 2009
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  kaka/dada, hakuna anayejua kama yesu au shetani ni mzungu au mwafrika. hizo ni imaginations zao tu wala zisikuumize kichwa hata chembe. wala usiconclude kutokana na movie za yesu ambazo yesu ni mzungu zile ni movie tu kama zingine na wale ni actors kama wengine ambao ni wazungu.
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Oct 19, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Hueleweki mkuu, Yesu anachorwa kizungu -hayo bado ni makosa, Yesu hakuwa mzungu bali Myahudi(Semite) na kwa mbali hana tofauti na Mwarabu(Arabs)
  Mwafrika anachorwa kama shetani, hiyo ni imagination ya mchoraji maana hata wewe unaweza kuimagine na kuchora utakavyo.
  Jiulize je dracula(wa Central Europe) kishetani kinacho sadikiwa kunyonya damu anachorwaje?-kizungu
   
 10. Shomari

  Shomari JF-Expert Member

  #10
  Oct 20, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Nadhani unamaanisha kwanini yesu awe mweupe ( yaani mzungu ) na shetani awe na rangi nyeusi.
  kwa kukusaidia ni kwamba si kweli kwamba rangi ya mwafrika ni nyeusi, na si kweli kwamba rangi ya mzungu ni nyeupe. bali ni neno hilo kutumika katika lugha ya utani ama lugha ya alama. mfano rangi nyeusi : huchukuliwa kama rangi isiyokuwa na uhai pia ni rangi inayowakilisha maovu. Giza linapoingia usiku na maovu nayo huongezeka tofauti na mchana, kutokana na hilo tunaweza kusema kwamba rangi nyeusi ni rangi iliyojawa na aibu ( kama ulikuwa hujui aibu nayo ni dhambi ).
  kulingana na mwendelezo huo wa rangi nyeusi kutumika kama alama ndipo hapo utakuta maneno mengine kama: Black sheep , Black horse , Black widower, Black mail, Black out, Black market.....na kuendelea, ukiangalia tafsiri za maneno yote hapo juu huwa hayana maana nzuri lakini bado mimi hainiumizi sababu rangi yangu ni Kahawia na si Nyeusi ( kama mkaa ) na bado huwa ninayatumia maneno hayo kila mala. asante
   
 11. Calnde

  Calnde JF-Expert Member

  #11
  Oct 20, 2009
  Joined: Oct 7, 2008
  Messages: 1,373
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0

  Tatizo ni wao(weupe) kuwa na technolojia na kuanza kuigiza zamani! naamini kama tungenza kuigiza na Yesu mweusi, hata leo watu wangeamini hivyo. However, weusi au weupe wa Yesu kwetu sidhani kama una umuhimu sana. ( to me its immaterial). Jambo la Msingi ni kwamba tunaikubalije kazi ya Yesu(kama unamwamini) pale msalabani. Ni lazima, kwa sababu tunaamini alikuja kama binadamu, angechukuwa rangi mojawapo, labda mweusi, mweupe, nk. Hiyo haina maaana weupe ni watakatifu kama ikiwa Yesu alikuwa Mweupe. Kumbuka woooote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu. Tuiamini kazi ya Yesu Msalabni, hatuokolewi kwa kuwa na rangi kama yake, bali kwa kumwamini kwamba alikufa kwa ajili ya dhambai zetu. Yatosha
   
 12. D

  Darwin JF-Expert Member

  #12
  Oct 20, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kama hao KKK wanajiita conservative Christians mpaka leo na wala sijawahi sikia many white Christians wakiwakemea.

  Ila ndio hivyo deen imeletwa kwa watu wasio na uwelewa wa mambo.
  Hao hao walioileta hio deen sasa wanawaruhusu wanaume kwa wanaume kubanjuana tena nakuoana makanisani.
  Haya waafrika na nyinyi igeni maana kila afanyacho mzungu ndio bora.
   
Loading...