Yesu Kristo anarudi

Amina mpendwa kwa hakika Yesu yu karibu kuliko tulivyoanza kuamini.
Ni kweli ndugu, tupo nyakati mbaya sana. Vipi unaizungumziaje kuhusu unyakuo, dhiki kuu, utawala wa miaka 1000 ya Bwana Yesu na hukumu kwa watu wote baada ya utawala wa miaka 1000 ya Bwana Yesu hapa duniani?
 
Great!
 
Hakuna ajuaye siku wala saa ndiyo maana tangu hujazaliwa watu wanatangaza anarudi anarudi wanakufa wanasahaulika wanakuja wengine anarudi anarudi....
 
Mi naomba siku atakayokuja niwe nimekunywa Konyagi ili nimtwange maswali mujarab!!
 
Lini?
 
Ungezaliwa na kulelewa kwenye uislamu saiv Uzi ungesomeka "jamani tusilimu uislam ndo dini ya mwenyezi MUNGU" ungezaliwa India ungekua zako bize unamuabudu brahaman, ungekua ugiriki ungekua unamuabudu Apollo, Zeus au Wotan , ungezaliwa Kwa wahdzabe ungekua uko bize saivi unawinda tu huna muda na dini na kuabudu
 
Ngoja tusubiri mungu wa yesu atavowachoma moto wasio wakristo takribani watu bilioni 6 pia mungu wa waislam (Allah) atavowachoma moto wasiofata dini ya haki na kweli ya mwenyezi mungu uislamu.
 
Mteule wa Mungu, ni kweli Yesu Kristo ANARUDI. Zamani tulisema siku hizi ni za mwisho lakini sasa tukio linalokuja kutokea duniani ni kurudi kwa Yesu. Maana saa ya wokovu wetu imekaribia kuliko tulivyoanza kuamini(Warumi 13:11).

Tazama yuaja na mawingu na kila jicho litamwona( Ufunuo wa Yohana 1:7)

Mimi binafsi kwa neema ya Mungu nimepata maono na njozi nyingi juu ya kurudi kwa Bwana Yesu, uhalisia wa upendo wa Mungu kwetu, jehanamu, anguko la Shetani, unyakuo wa watakatifu(rapture of the saints) na mengineyo. Kama nikipata muda nitajitahidi kushare hapa ili mwenye masikio ya kusikia na asikie.

Jambo la muhimu kwa sasa ni inatupasa kutubu na kuishi maisha matakatifu maana Yesu anarudi kuchukua wateule wake wasio na mawaa yeyote wasio na dhambi yeyote, watu waliyoyafua mavazi yao na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo wa Mungu. Na Roho Mtakatifu ndiye sumaku ya kutufanya tuweze kunyakuliwa ile siku kuu ya kuja kwa Yesu. Pia tuzidi kuwaambia wengine juu ya pendo la Mungu kwa wanadamu.

Mungu awabariki. Maranatha.Amen
 
Amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…