Himidini
JF-Expert Member
- May 8, 2013
- 5,534
- 4,193
^^

Ni kawaida sana katika mapenzi kusikia kauli kwamba "we ni wangu".. mpenzi wangu... mke wangu.. Mume wangu na mengineyo mengi yanayosaidia kukua kwa mahusiano, kuyafanya yalete maana na muungano mzuri. Utajisikaje kuishi na mtu ambae mnaitana wapenzi lakini kwenye kamusi yake maneno hayo yalirukwa, kifupi hayajui wala hakuwahi kuyatamka hata kwa bahati mbaya? Bila shaka utajisikia vibaya. Tunahitaji kuhitajika, kuthaminiwa, kuona kuwa upendo tuutoao unapata majibu mazuri.
Sasa kuna wale wenzangu na mimi ambao neno " wangu " linatumika ipasavyo. Akikupenda ndio basi tena hataki uonekane umesimama na mwingine, hataki ushikane na mwingine,anataka muda wote uwe umetazama simu yako kusubiria meseji yake, ukiwa matembezi huna wa kumtazama isipokuwa yeye... Kwake hiyo ni maana ya neno "wangu" We ni wake, hupaswi kwenda pengine, yuko radhi akuletee chakula ndani, utapewa kila kitu utakacho, iwe pesa, mavazi, chakula, Tv ilimradi tu unakosa uhuru wako.

UKIMPENDA USIMGEUZE HATI MILIKI
Kupenda hakuna maana umnyime haki yake ya kuwa yeye. Ni kweli ni wako lakini nae ni mwanadamu anaehitaji kufurahia maisha. Maisha hayako kwako tu, maisha yako kwa watu. Kupendwa kwa aina hii ni utumwa, ni mateso ni kukosa furaha. Huyo si gari lako ambalo lipo tu kusubiri kuongozwa wakati wote na kule upendako. Wala kummiliki hakukupi wewe usalama wa mapenzi. Migogoro mingi utaiepuka ukimpa uhuru anaostahili.

UKIMPENDA KUBALI VIPAJI VYAKE
Kumbana kupita kiasi ni kumfanya mwenza wako aue vipaji vyake ambavyo kayika uhalisia vingeweza kuinua kipato cha familia au kuboresha hali zenu za mahusiano. Kama anajishughulisha na kazi ambayo inahusisha mchanganyiko wa watu wengi wenye hulka na silika tofauti, ambazo unadhani zitahatarisha mwenendo wa mwenza wako, jaribuni kukaa pamoja mtazame namna ya kubadilisha kazi hiyo. Hili ni msingi hasa ikumbukwe kuwa unamjengea mwenzako namna nzuri ya kujitegemea maana Ya Mungu mengi, kesho na kesho kutwa hutakuwepo, anaweza kuhudumia uwapendao vizuri.

UKIMPENDA RUHUSU URAFIKI NA WENZAKE
Kuna mtu akikupenda basi sahau habari za marafiki uliokuwa nao, utaulizwa maswali usiombe, huyo nani, kwa nini anakusalimia kila anapokuona, kwa nini anakuremulia macho, unaenda kutazama mechi huko kwani hapa hakuna TV, n.k Ni kweli una haki ya kujua rafiki zake ila hilo halikufanyi umbane mpaka akose pumzi. Wewe usiishi kwa niaba ya maisha yake. Mpe nafasi aione dunia, ajue mapya ya siku nzima, ajue hali za wengine. Life is like a boat don't sail alone.
TAHADHARI;
UKIPEWA UHURU ONESHA KUJALI
Kuna watu watu katika mahusiano wanapopewa uhuru, hawajui wafanye nini, wapi na wakati upi. Mambo madogo madogo mbele ya watu yanaweza kumkwaza mwenzako, au maelezo ya kuunga unga hujenga mashaka zaidi.

UKITAKA KUMJUA MTU MPE UHURU
Kutoa uhuru haina maana unalinda uaminifu. Uzoefu unaonyesha kuwa uaminifu ni tabia ya mtu.
Ukitaka kumjua mtu we mpe uhuru. Wahenga walisema mvishe jogoo kofia utaona mwendo wake, ataringa atajivuna, atapagawa ikiwa hivyo mvue kofia. Kama ataiona kofia ile ina mfaa kujikinga na jua basi mwachie.
If am all faithful, understanding, human and you real love me, give me my freedom. Don't possess me.GENUINE LOVE IS NOT POSSESSIVE