Yeriko Nyerere, Shirika la Majesuit la Kanisa Katoliki siyo majasusi kama unavyodanganya

SubiriJibu

JF-Expert Member
Jun 26, 2009
1,803
1,863
Miaka kama mitano nyuma nilipoanza kumfahamu Yericko Nyerere nilimuamini na nikiri kwamba nilikuwa mshabiki wake.

Lakini nikaja kugundua jambo moja wasilolijua wengi. Yeriko si mvivu wa kusoma, anasoma sana. Lakini yuko katika mazingira ya watu wavivu kusoma yaani watanzania.

Hivyo, Yeriko anaonekana ni very brilliant kwa kutokana na mazingira hayo. Kwa sababu hoja zake zinaenda kwa wavivu wa kusoma na ukicheza huwezi kuzipangua.

Hana tofauti sana na Zitto Kabwe maana wote ni wazuri katika kusoma. Tatizo la Yeriko na Zitto Kabwe ni kwamba wote wawili ni wanasiasa.


MWanasiasa anaposoma kitu ni bora mkajadili naye mtaani hapo anaweza kukupa ukweli halisi. Lakini wanasiasa wengi wakiamua kuchambua kitabu hadharani, basi karibu wote hfanana kwamba wanakichambua kisiharibu mitizamo yao ya kisiasa.

Wanamcheka Mwakyembe kukana PhD yake kwenye Bunge la Katiba lakini wote hata akina Yeriko Nyerere ni walewale tu.

Yeriko nimekuja kumfahamu vizuri alipoanza kuandika masuala anayoita ujasusi na kulihusisha kanisa katoliki, kanis ambalo sisi wengine ni wataalamu na hapo ndipo tulipogundua uzuzu wa Yeriko Nyerere.

Humu kuna thread ameleta kuhusu picha za watawa waliomfadhili Nyerere kwenye UNO mwaka 1955. Nimehamisha thread kwa sababu mada yangu ni pana zaidi na nina hofu ikiungwa kule inaweza isisomwe.

Sasa kuhusu picha ya hao watawa ni kwamba Yeriko hajui hata sifa za watawa wa kanisa katoliki zikoje na ningeshangaa kama Otorong'ong'o asingekuja humu kumuumbua mtu kama huyu na tayari ameshaonyesha picha za watawa zikoje.


MImi naenda mbali kwa maelezo. Kwanza mashirika anayosema Yeriko yaani Maryknol na Jesuit mimi yamenilea hivyo sifundishwi kuhusu Maryknol au Jesuit ninayafahamu mashirika haya ingawa sintakwambia na hutajua yamenilelea wapi.

Kwanza sifa za mtawa (religious) yeyote wa kanisa katoliki lazima atakuwa na msalaba. Mmezoea sana jina watawa ni masista lakini sisi wataalamu wa kanisa katoliki watawa tunawaita religoius hivyo wapo wanaume wengi watawa pia.

Aliyejenga kanisa la St. Joseph pale D'Salaam hakuwa padri alikuwa religious na kwa sababu kwa kiswahili chenu mlidhani watawa ni wa kike tu na kwa sababu watawa wanaitana brother au sister huyu mkashindwa kutamka neno brother mkamuita buruda!

Hivyo watawa lazima wana msalaba na kama hujui mwangalie sister yeyote kama hana msalaba

Sasa, katika picha za Yeriko Nyerere sioni msalaba wowote naona picha za majimama wamevaa baibui! Hiki ni kituko cha Yeriko Nyerere.

Pili ni kwamba, hata kama Maryknol wangemsaidia Julius Nyerere na kumpa nauli, tena kwa mbinu za ujasusi, hivi unategemea waende wapige picha hadharani kiasi kile halafu unatudanganya wewe ni mtaalamu wa masuala ya ujasusi?!

Jasusi gani akufadhili pesa halafu afanye jambo la kipimbavu la kupiga picha hadharani na wewe wakati serikali ya mkoloni umeshasema haipendi wakatoliki inapenda waanglikana.

Sasa Yeriko anasema ujasusi wa Jesuits umethibitishwa kwenye kitabu cha Vatican Assassins cha Eric Jon Phelps. Kwa hiyo Yeriko kasoma kitabu hicho kapata tunachoita absolute truth.

Yeriko ni mbabaishaji anajua ukishakitaja hakuna watakaombishia maana watanzania ni wavivu kusoma.

Nimekwamia kwamba mimi nimelelewa na Maryknols na Jesuits. Mengi yanasemwa kuhusu Jesuit kwamba ni majasusi. Hii ni dhana kipumbavu. Ukweli ni kwamba usipojua hitoria ya kanisa katoliki hata Jesuits hutawajua.

Shirika la Jesuits lilianzishwa na Saint Ignatius wa Loyola. Yeye alikuja na mbinu ya kuwamaliza waprotestant kwamba ukiingiza elimu utawapata wakatoliki walioelimika na watapambana na uprotestant vizuri.

Hivyo, msingi wa Ignatius na shirika lake ikawa ni kusambaza elimu bora. Shirika lake likaitwa na hadi leo linaitwa Society of Jesus kwa kifupi SJ, wengi huliita nikcname Jesuits. Ignatius alipata wenzake akina Francis Xavery na wakaendeleza elimu.

Hivyo, mikakati ya Jesuit ikafanikiwa. KWamba Uprotestant unaenea kwa kasi lakini shule bora za majesuit zinafunguliwa kila kona. Ujerumani kulikokuwa kitovu cha Walutheri wakasalimu amri kwamba ingawa hawakupenda ukatoliki, lakini wakubwa wa nchi walikuwa hawana jinsi bali kupeleka watoto wao wakasome katika shule za majesuit.

Kwa ujumla majesuit wakawa wataalam wa elimu Europe. Hata ile kesi ya Galileo Galileo walimshinda majesuiti kwa hoja kwamba Galileo kashindwa kuthibitisha dhana yake kisayansi na kwamba huwezi kutuambia kwamba dunia inazunguka jua bila uthibitisho.

Kumbuka hakuna nchi hata moja ambayo ilikuwa inaendesha elimu kama ilivyo sasa. Hakuna nchi iliyokuwa na shule. Shule Ulaya zikawa za majesuit. Sylabus inakaguliwa na majesuit.

Nchini Ujerumani aliiondoa hali hii Chancelor Otto van Bismark, yule aliyeigawa Afrika na akasema kuanzia mwaka 1885 sylabus itaanza kukaguliwa na serikali ya Ujerumani na si majesuit.

Hivyo, majesuit ndiyo taasisi pekee yenye uzoefu wa miaka zaidi ya 400 ikiendesha elimu. Majesuit ndiyo waliopeleka eimu India na hasa kule Goa. Walienda hadi Japan wakati ilikuwa vigumu kwa shirika lolote kuingia kule.

Mwaka 1556 Ignatius alianzisha printing press na inaendelea kuwepo hadi leo inaongoza kwa kuchapisha vitabu inaitwa Ignatius Press. Vitabu viili vya Papa Benedict XVI kavichapishia huko.

ata kie kitabu kilichomuumbua Dan Brown aliyeandika Da Vinci Code kiitwacho "Da Vinci Hoax" kimechapishwa na Ignatius Press.

Majesuit hawakubabaisha na elimu yao popote duniani. Hawajawahi kuzidiwa na inaelekea hakuna wa kuwakaribia. Nchi zilipoanza kuchukua shule wao walikataa kubadili mfumo wa elimu.

Hapo Tanzania Julius Nyerere alipobadilisha shule zifundishwe kwa kiswahili kila somo, majesuiti wakamkatalia wakasema shule zao wataendelea na kiingereza yaani english medium. Hivyo shule za majesuit nchini Tanzania zikaendela kuwa english medium bila kujali Nyerere anapenda au la.

Moja ya shule hizo ni Saint Francis Xavier ya pale Mwanza, yenyewe ni ya majesuit ilikataa kubadili kuwa kiswahili na haijawahi kufunsha kwa kiswahili tangu Nyerere analeta uhuru hadi leo.

Majesuit walikubali masharti machache tu kwamba mitihani ya shule zao kwa darasa la saba watafanya kwa kiswahili na majina ya shule wakakubali kubadili na ndipo Saint Francis Xavier school ya Mwanza ikabadilishwa na kuitwa Nyakahoja Primary Shcool.

Hao ndiyo majesuit hawababaishiwi. Matokeo yake serikali iliposhindwa kumiliki shule zilizokuja zikaiga mfumo wa majesuiti wa kundisha katika englihs medium. Leo hii kila shule ni englieh medimu kama za majesuit.

Mafanikio ya majesui ni kila wanapoanzisha shule. Na wanapoanzisha wanazipa majina ya waanzilishi wa shirika lao au mahala alipozaliwa mwanzilishi. Mwaka 1997 pale D'Salaam wakaanzisha shule wakaiita Loyola Secondary School, nadhani iko Parokia ya Kigogo.

Pale Dodoma wakaanzisha shule inaitwa Saint Ignatius Primary School nadhani ukiwa unaelekea Miyuji. Mwaka 2009 pale Dodoma wakaanzisha shule inaitwa Saint Peter Claver nadhani iko maeneo ya Ihumwa.

Ukishajiwekeza kwenye elimu, hakuna wa kukufiki ahapa duniani. Hayo ndio mafanikio ya Jesuits yasiyofikiwa na taasisi yoyote duniani.

Viongozi kadhaa wa dunia hii ni tunda la elimu ya majesuit. Rais Bill Clinton wa Marekani alisoma Unversity of George Town ambayo ni ya Majesuit.

Baadhi mtashituka kusikia kwamba hata Rais John Magufuli ni zao la elimu ya majesuit. Kwa nini?

John Magufuli alisoma seminary na akaondoka huko akiwa FORM 3 mwaka 1977. Hakuwa seminary ya Majesuit. Najua utasema kwamba alihamia LAKE SECONDARY ya Mwanza.

Ni kweli alihamia LAKE SECONDARY lakini tunaojua ukweli zaidi ni kwamba wakati anahamia pale LAKE SECONDARY mwanzoni ilikosa mwendeshaji mzuri hadi ikaazima majesuit waiendeshe na hivyo John Magufuli aliikuta LAKE SECONDARY ikiendeshwa na majesuit.

Pale LAKE SECONDARY majesuit walimpeleka padri De Souza aliyeendesha shule hadi mwanzoni mwa miaka ya 1990. Hivyo, padri De Souza akawa anaendesha kanisa la Nyakahoja, Shule ya msingi Nyakahoja na pia Lake Secondary.

Hivyo, Bill Clinton na John Magufuli ni zao la elimu ya majesuit.

Hivyo, nguzo ya kuijua dunia ni elimu tu hakuna kitu kingine. Majesuit wanazingatia elimu tu. Kama mwanafunzi wa majesuiti aliingia ikulu ya Marekani na sasa yupo katika ikulu ya Tanzania hayo ni matokeo ya elimu yao bora na si ujasusi.

Ukija kwenye shirika la Maryknoll nimesema hata hili limenilea ninalijua. Shirika hili lilianzishwa na Baraza la Maaskofu la Marekani tuseme "TEC" ya Marekani.

Wakati majesuit wanajikita mjini, hawa Maryknoll hupenda kujikita vijijini ambako hapaendeki na kila mtu. Yaani wao lengo ni kumtoa mtu katika primitive stage kumleta mtu katika civilization.

Hivyo wanapenda kufungua centre yao huwa ni porini kwelikweli hadi unajiuliza walifikaje huko. Na wakifika huko, kitu cha kwanza ni kujifunza lugha ya huko na kutoa hata biblia kwa lugha ya huko.

Hivyo, ukimkuta padri wa Marknol anajua kijaluo, kikwaya, kijita, kizanaki.

Ni kweli Maryknoll walijikita mkoa wa Mara. Katika mazingira kama hayo, Julius Nyerere alipoacha kazi kufudisha pale St. Francis, akarudi Butiama akakuta mapadri wana kazi ya kubadili Catechism iandikwe kwa kizanani ili wanzaki waielewe.

Hivyo, mapadri wakamouomba Julius Nyerere awasaidie kuandika Catechism kutoka kilatini au kiingereza kwenda katika lugha ya kizanaki na akaifanya na kama ni kumlipa walimlipa kwa msingi huo.

Sivyo kama Nyerere anavyodanganya kwamba walimlipa Nyerere mshahara kwa kukaa tu pale Butiama eti wanamuandaa kuwa kiongozi wa nchi.

Kwanz akinachojulikana ni kwamba kanisa lilimuwekea mikwara likamshawishi abaki kufundisha ili asife na njaa. Mapadri walianza kumshawishi Maria Nyerere, ikashindikana na mwisho akajiuzulu.

Kingine ni kwamba nimesema Maryknoll ilianzishwa na Baraza la Maaskofu la Marekani mnamo mwaka 1911. Kama unalijua kanisa katoliki, kufikia mwaka 1955 yaani miaka 44 eti shirika hilo tayari liwe na waafrika.

Si rahisi ndani ya miaka 44 shirika la katoliki liwe limepata members kutoka bara jingine na hasa huku Afrika ambapo ukatoliki ndiyo kwanza ulikuwa unaibuka. Hivyo ni uongo uliopitiliza kusema hao wavaa mabaibui eti ni masista wa Maryknoll.

Hivyo sifa ya kuwa member wa Maryknoll ikikuwa uwe mmarekani na hadi leo si rahisi sana kupata asiye mmarekani kuwa Maryknoll ingawa wanaweza kuanza kuwepo.

Sasa Yeriko Nyerere ameonyesha umbumbumbu wa hali ya juu kutojua chochote kuhusu Jesuits na Maryknoll na wala hajui tofauti yao. Kwa mujibu wa maelezo yake anaona kwamba Maryknoll ni mwamvuli wa Jesuits walitumika kumfadhili Julius Nyerere.

Ukismoa nilichoeleza utaona kwamba Jesuits na Maryknoll ni mashirika tofauti kabisa na malengo tofauti.

Nimekwambai nimelelewa na haya mashirika mawili. NI rahisi mtanzani wa kawaida kusoma katika shule za Maryknoll kwa sababu wanajikita vijijini na kwa watu masikini.

Lakini kwa mtanzania wa hali ya chini ni vigumu sana kusoma katika shule za Jesuits.

Ukitaka kujua fuatilia hadhi ya watanzania waliosoma Nyakahoja Primary School, au Loyola Secondary school.

Jokate Mwegero (kidoti) amesoma u Loyola Secondary school. Unamuonaje hadhi, busara yake, pose yake, exposition yake ukimlinganisha na Wema Sepetu!

Hivyo, Yeriko Nyerere ni mabaishaji unayehitaji kuwa makini kungudua kwamba ni mbabaishaji.

Yeriko Nyerere amentaja Joseph Gabriel Zelge kwamba alijiuzulu kazi ya kanisa baada ya kugunduliwa na wakoloni. Yeriko hajui kwamba kipindi hicho ni miaka michache baada ya vita ya kwanza ambapo wamisionari wengi hawa wa nchi zilizishindwa walikuwa wanahisiwa kuvuruga nchi.

Nchi hii ilitawaliwa na Ujerumani ikashindwa. Kulikuw ana hisia kwamba wamsionari wanye asili au lugha za kijerumani wasipewe nafasi nchini na waliteseka wengine wakaondoka wenyewe.

Ili uelewe ni kwamba Polycarp Pengo ni askofu wa nane wa D'Salaam wakati huyo Joseph Gabriel Zelge alikuwa ni askofu wa tano wa D'Salaam.

Lakini Yeriko anayechanganya u-jesuit na um-maryknoll hajui huyu askofu Joseph Gabriel Zelge alikuwa wa shirika gani.

Askofu Joseph Gabriel Zelge alikuwa mkapuchini yaani O.F.M. Cap. ambao ndiyo hawa akina askofu Jude Thadaeus Ruwa'Ichi wa Mwanza.

Hivyo, huu ni umbumbumbu mwingine wa Yeriko Nyerere.

Tumalizie tena kuhusu barua ya Papa kuifanya Tanzania kuwa chini ya Bikira Maria. Yeriko hatambui kwamba hayo mambo yanafanyika kila wakati. Kitendo hicho wakatoliki tunakiita "consecration". Mapapa wengi walishaiweka duniani nzima chini ya Bkira Maria, sasa utasemaje.

Kama ungesoma ujumbe wa watoto wa Fatima hoja yao ilikuwa ni kwamba kui-consecrate Urusi iwe chini ya Bikira Maria. Hivyo hakuna la ajabu labda kwa mambumbumbu kama Yeriko Nyerere.

Yeriko Nyerere
,

Binafsi siipendi CCM na sijui kama nitakuja kuipenda. Lakini mimi si mwanasiasa hivyo CCM ianguke isianguke sijali sana.

Lakini tatizo lenu nyinyi wanasiasa mnaoichukia CCM kwa mujibu wa vyama vyenu, mnadhani tutawaunga mkono hata pale ambapo mnapotamka utumbo ilhali utumbo huo unatolewa na anayeichukia CCM kama mimi.

Yeriko, pambana na kujenga mikakati kwa chama chako ili siku moja tukichague kiwe chama tawala tuondokane na hili dude hili linaloitwa CCM na usikimbiie mambo yaliyo juu ya uwezo kwa akili yako kama haya ya Kanisa Katoliki.

Huyu dogo mpotoshaji sana. Hao wanaodaiwa kuwa watawa naona kama baadhi ni kinamama wa kiswahili. Shirika la Maryknoll halikuwa na watawa waswahili miaka hiyo. Mtawa mtanzania wa kwanza kapatikana miaka ya 80 au 90 mwanzoni binti Nyakyi.

brilliant analysis
Yericko hicho kitabu chako nitakipataje, hakuna namna imebidi nikisome tu.
Mambo mazito ya kanisa katoliki
Naam, unamtaja Sr. Mary Reese, huyu namfahamu sana. Tangu 2012 karudi nyumbani kwao Marekani. Kwa sasa umri wake ni miaka 96, sawa na umri ambao Nyerere angelikuwa nao kama angekuwa hai hadi leo hii...

Nimelazimika kuweka sawa upotoshaji wa muda mrefu wa mzee wangu Mohamed Said juu ya picha hizi...
Na Yericko Nyerere
Tunapaswa kuwa na utaratibu wa kuangalia afya za macho yetu angalau mara moja kwa mwaka

Mohammed Said yuko sahihi katika hili. Maryknoll Sisters walikuwa wameingia nchini wakati huo lakini walikuwa bado hawajapata watawa wazalendo bado.
Ulichoandika ni upuuzi mtupu, hujaweka Evidence hata moja ya Conspiracy yako

Ni wajinga wachache tu wanaweza kuamini Stori za kutunga.

Nakupa Challenge WEKA EVIDENCE hapa na si Kupikapika matukio

Mkuu kwa heshima zote naomba nikujulishe sio lazima masista weusi wote wa wakati huo wawe watanganyika. Kuna utaratibu wa kuchukua watawa toka nchi moja kwenda kufanya kazi nchi nyingine. Hata sasa shirika la Immaculate Virgin Heart of Mary wapo hapa Dar wana sisters weusi toka Kenya na Uganda ambao wanaongea kiswahili safi tu kama watanzania.

Hao sisters wa Maryknoll walipoingia Africa walianzia Tripol libya wakashuka Kenya ndio wakaingia Tanganyika maeneo ya Musoma. Laiti tungeliwajua majina yao hao wanaotajwa kama ni masista na Yericko pengine tungewajua asili yao wapi.
Nakubaliana na wewe mia kwa mia; hilo vazi walilovaa hao wakina mama katika picha ya kwanza na Mwalimu ni mabaibui na sio nguo za masista!! Ukiangalia picha ya bibi Titi ya kwanza na ya pili ndio utadhibitisha hilo!!! Hakuna masista hapo huo ni upotoshaji wa dhahili!
View attachment 710574 View attachment 710575
Inawezekana unayosema kweli mkuu,lakini hizo picha sio watawa wa kikatoliki,nimekuwekea mfano wa wanawake wa kiislam walivyokuwa wakivaa mabaibui yao,miaka ya nyuma...

Acheni kupotosha ukweli,.. hamna asiejua kama Nyerere alikaribishwa tu katika ukombozi wa Tanzania...
View attachment 710550
Picha ya juu hao wanawake ni wanawake wa kiislam,hao wanawake wamevaa mabaibui ya zamani,mabaibui ya kamba shingoni,hamna sister hata mmoja hapo....

Picha za chini ni mfano wa hayo mabaibui ambayo kwa sasa hayavaliwi tena,sema kule Zanzibar bado kuna wanawake watu wazima wachache ambao wanayavaa,..
View attachment 710553
View attachment 710558
 
Jokate Mwegero (kidoti) amesoma u Loyola Secondary school. Unamuonaje hadhi, busara yake, pose yake, exposition yake ukimlinganisha na Wema Sepetu!
Hapa ndipo ulipojiaibisha, so LOYOLA wanawatengeneza mabinti wenye hadhi ya u.m.a.l.a.y.a Are you serious? Kuna uchafu alioufanya wema sepetu ambao jokate hajafanya? Hivi kuna star Tanzania ajaonja nyapu huyo dem ambaye unamuona ndio mfano wa kuigwa?
 
Hapa ndipo ulipojiaibisha, so ROYOLA wanawatengeneza mabinti wenye hadhi ya u.m.a.l.a.y.a Are you serious? Kuna uchafu alioufanya wema sepetu ambao jokate hajafanya? Hivi kuna star Tanzania ajaonja nyapu huyo dem ambaye unamuona ndio mfano wa kuigwa?

nani mwenye kesi ya bangi kati ya hao wawili. Nani anajiendesha kw akampuni yake katika hao wawili. Halafu uwe kichwa kinachoshika haraka. Hakuna Royola kuna Loyola.
 
nani mwenye kesi ya bangi kati ya hao wawili. Nani anajiendesha kw akampuni yake katika hao wawili. Halafu uwe kichwa kinachoshika haraka. Hakuna Royola kuna Loyola.
Nimekwambia tafuta mtu mwingine sio huyo, listi ya mastaa ambao wamemgonga huyo "role model" wako tu inatosha kuonyesha uko wrong. Waliomgonga sepetu ndio hao wanamgonga Kidoti so hao ni ndege wanaofanana, Hata huyo jojo akikinzana na wenye chama anaweza kukamatwa hata cocain. Huyo dem kaanza kuchezeshewa toka yupo hapo Loyola, labda kama kipindi hicho ulikuwa bado uko nanjilinji. Pole.
 
Nimekwambia tafuta mtu mwingine sio huyo, listi ya mastaa ambao wamemgonga huyo "role model" wako tu inatosha kuonyesha uko wrong. Waliomgonga sepetu ndio hao wanamgonga Kidoti so hao ni ndege wanaofanana, Hata huyo jojo akikinzana na wenye chama anaweza kukamatwa hata cocain. Huyo dem kaanza kuchezeshewa toka yupo hapo Loyola, labda kama kipindi hicho ulikuwa bado uko nanjilinji. Pole.

sijaweka role model mmoja nimekuwambia role model kadhaa za shule za majesuit ambalo hubishi maana yake umekiri. Suala la kugongwa unavyodai hujui hata wewe unaweza kuwa unagongwa na hatujui.
 
Nakwambia hivi, Wapo watu wengi waliosoma loyola ambao wake upstairs kwa hizo sifa ulizozitaja. Kwa sisi ma mishen town ambao tumetumia mda mwingi kwenye viwanja vya bata tunajua huyo dada ameanza kufanya uhuni tokea yupo Loyola na ndio kipindi hicho ndio alipata umaarufu, sisi tunamjua Jojo tokea anavaa skert za sekondali. Nimeshangaa unavyomlinganisha na m.a.l.a.y.a mwenzake as if kuna uchafu anaoufanya wema then huyo dada haufanyi. Tafuta watu wengine wenye hadhi ya loyola sio huyo.

Kama ulimuona anafanya umalaya je, alifanya katika viwanja vya shule. Sisi tunasema tunachokithibitisha in public. Suala la boyfriend haliendani ni majesuit au maryknol ninaosema.

Inawezekana na wewe ni product ya shule za kata wale mnaogeuka kuwa waumini wa Yeriko Nyerere.
 
Aliyejenga kanisa la St. Joseph pale D'Salaam hakuwa padri alikuwa religious na kwa sababu kwa kiswahili chenu mlidhani watawa ni wa kike tu na kwa sababu watawa wanaitana brother au sister huyu mkashindwa kutamka neno brother mkamuita buruda
Acha kudanganya watu neno bruda sio kukosea kiswahili asili yake ni kijerumani na wanaitwa hivyo hivyo bruder. Hata neno shule wao wanaandika schule! Maneno mengi ila umeandika na uongo pia!
 
Kama ulimuona anafanya umalaya je, alifanya katika viwanja vya shule. Sisi tunasema tunachokithibitisha in public. Suala la boyfriend haliendani ni majesuit au maryknol ninaosema.

Inawezekana na wewe ni product ya shule za kata wale mnaogeuka kuwa waumini wa Yeriko Nyerere.
Yes boss, mimi ni product ya shule ya kata, na nimebahatika kufika mpaka elimu ya juu. Kwa hiyo kwa hii thread yako umemaanisha wema sepetu hizo tabia alifanya kwenye viwanja vya shule sio? hauwezi kuwatofautisha watu ambao kwa wakati kadhaa wameshawahi kugombania mwanaume, tena in public sasa sijui wewe unaongelea public gani. So kwa point yako watu waliosoma shule ya kata ndio hawajielewi na waliosoma loyola ndio mfano wa kuigwa?

Wema Sepetu Aanawashangaa wanaomponda Jokate
 
Kingine ni kwamba nimesema Maryknoll ilianzishwa na Baraza la Maaskofu la Marekani mnamo mwaka 1911. Kama unalijua kanisa katoliki, kufikia mwaka 1955 yaani miaka 44 eti shirika hilo tayari liwe na waafrika.

Si rahisi ndani ya miaka 44 shirika la katoliki liwe limepata members kutoka bara jingine na hasa huku Afrika ambapo ukatoliki ndiyo kwanza ulikuwa unaibuka. Hivyo ni uongo uliopitiliza kusema hao wavaa mabaibui eti ni masista wa Maryknoll.
Hivyo sifa ya kuwa member wa Maryknoll ikikuwa uwe mmarekani na hadi leo si rahisi sana kupata asiye mmarekani kuwa Maryknoll ingawa wanaweza kuanza kuwepo.
Unajua historia ya kuja kwa wamisionari wabenedictini na white Frs hapa Tanzania ilikuwa mwaka gani na walipenyapenyaje wengine kwenda kusini na wengine kaskazini ndo uhitimishe kuwa miaka ya 1955 ndo ukatoliki ulikuwa unaanza kuchipua? kafanyie utafiti kabla ya kuja hii hii conclussion Pia mbona watawa wa Maryknoll hata watanzania wapo wengi tu sembuse waafrika?
 
Yes boss, mimi ni product ya shule ya kata, na nimebahatika kufika mpaka elimu ya juu. Kwa hiyo kwa hii thread yako umemaanisha wema sepetu hizo tabia alifanya kwenye viwanja vya shule sio? hauwezi kuwatofautisha watu ambao kwa wakati kadhaa wameshawahi kugombania mwanaume, tena in public sasa sijui wewe unaongelea public gani. So kwa point yako watu waliosoma shule ya kata ndio hawajielewi na waliosoma loyola ndio mfano wa kuigwa?

Wema Sepetu Aanawashangaa wanaomponda Jokate

Anzisha thread ya kugombania wanaume. sisi tunazungumzia education product ya Jesuits kuanzia miaka ya 1500s hadi leo. Kama umesoma shule za kata mimi sina jinsi zaidi ya kukupa pole, unless umetumia personal efforts zako.
 
Acha kudanganya watu neno bruda sio kukosea kiswahili asili yake ni kijerumani na wanaitwa hivyo hivyo bruder. Hata neno shule wao wanaandika schule! Maneno mengi ila umeandika na uongo pia!
katia na chumvi eti
 
Unajua historia ya kuja kwa wamisionari wabenedictini na white Frs hapa Tanzania ilikuwa mwaka gani na walipenyapenyaje wengine kwenda kusini na wengine kaskazini ndo uhitimishe kuwa miaka ya 1955 ndo ukatoliki ulikuwa unaanza kuchipua? kafanyie utafiti kabla ya kuja hii hii conclussion Pia mbona watawa wa Maryknoll hata watanzania wapo wengi tu sembuse waafrika?

Unajua tatizo la JF na majina bandia kama tunayotumia ni kwamba unawez akujikuta unabishana na mtoto wako ambaye unajua wazi akili yake ni changa.

Pole kwa kutokujua mashirika kama wabenedictine, jesuits, Maryknoll. Niambie mtanzania wa Maryknol wa mwaka 1955 ni nani.
 
Back
Top Bottom