Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,499
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kigamboni kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Yericko Nyerere ameahidi kuibadilisha Kigamboni kwa kuhakikisha barabara zote kuu zinawekwa lami.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni, Yericko amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kukamilisha mradi wa barabara ya kilomita 60 kutoka Feli hadi Buyuni, licha ya kuanza tangu mwaka 2008, ambapo kila mwaka wamekuwa wakijenga kilomita moja pekee.
Ameongeza kuwa CCM imekuwa ikiwaletea wananchi kanga na vitenge badala ya kutekeleza miradi ya maendeleo, hali aliyoitaja kuwa ni hatari kwa mustakabali wa wananchi wa Kigamboni.
Kuhusu Tozo za daraja na vivuko amedai ni haramu na wizi ambao wanafanya CCM na Serikali yake