Yericko Nyerere: Kizazi cha dotcom hakipendi kujishughulisha!

Che-lee

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
318
88
Katika kipindi cha Pbcloudsfm nimefurahishwa na mada iliyokuwa inajadiliwa iliyohusu vijana wengi wa kiume kupenda kubebwa na mijimama yenye mkwanja,
Ambapo ktk mahojiano nimemsikia Yericko Nyerere akisema ugumu wa maisha na aina ya kizazi chetu cha dotcom vimechangia hayo!

Namfahamu huyu Yericko kupitia twitter @YerickoNyerere ni mmoja ya watu wa tata sana!

Jf great thinkers kunauhakika wa maoni hayo?
 
Mnamjua huyu Nyerere ? Naomba mkutane nae siku moja. Ni bonge la msanii hapa town, kijiwe chake pale opposite na wizara ya nishati na madini, anajifanya kishoka. Be care na huyu jamaa.
 
Mnamjua huyu Nyerere ? Naomba mkutane nae siku moja. Ni bonge la msanii hapa town, kijiwe chake pale opposite na wizara ya nishati na madini, anajifanya kishoka. Be care na huyu jamaa.
Hayo ni maisha yake binafsi na hayatusaidii sisi kama great thinkers, tujadili mawazo yake juu mada husika!
Tukisema tuanze kuchunguza maisha ya watu hapa tz tutageuka taifa la wanafiki!
 
Ni kweli niliombwa kutoa maoni yangu kwa tatizo hilo, ingawa siamini sana kama lipo kwa wingi sana,
Nilichokieleza nimawazo yangu kwa aina ya maisha tunayoishi leo, Vijana wengi hawajitumi, hasa wapatapo fursa hawazitumii ipasavyo, japokuwa ni ukweli usiopingika kuwa serikali yetu imeshindwa kutengeneza fursa za vijana kujitafuta riziki lakini vijana nao wamelowea ktk ombwe la utandawazi wa kigiza!

Vijana wameongeza bidii ya anasa huku wakipenda kuishi maisha ya kukopi na kupesti (maisha ya Kendra nk) jambo ambalo ni hatari kwa aina ya taifa tulilonalo, linalohitaji ujasiri, hekima na maarifa!
 
Kuongea kuendane na vitendo, sijui huyo Nyerere kafanya nini angalau kuwaonyesha hao vijana wenzeke mfano?
 
Sina hakika kama u kijana au mzee; lkn la msingi ni kwamba ni jambo la kheri sana kwamba nawe umeliona tatzo hili la vijana wengi hapa nchini kwetu swali langu ni kwamba baada ya kuona jopo kubwa la vijana wapatao fursa wanazichezea ni JITIHADA gani umeifanya ili kuwasaidia vijana wa namna hiyo ilhali nao waje watusaidie hata sie tusio bahatika kuzipata fursa hizo badala ya kuishia kuilaumu serikali na vijana hao?
 
Nikweli nilitarajia kukumbana na swali la namna hii, mimi ninasaidia na ninaendelea kusaidia kadiri ya uwezo wangu, vilevile kuwakumbusha kwa maandiko ni sehemu ya kusaidia kuwafungua akili zao!
 
...wengine wanaabudu pombe na kushndwa kuheshmu vyanzo vya pesa zao, hawashauliki katu, wanajiona wako sawa wakitumia ujana wao....kama wana laana au wamerogwa....hata uwapeleke kwa saikolojist maisha yao ni yale yale tu hawabadiliki hawa....wengine ni mabangi kama chakula wanajifariji na maisha ya bob marley bila kujua kuwa mwenzao alipenda muziki wake na alikuwa great thinker, wengine wanapenda ngono tena zembe na kibaya zaid wanaziendekeza kwa vigono mkononi...(yaani no job, no edctn, no future, dry is normality)....inatia huruma kwa kweli, wengi wanakufa kzembe wakiwa angali na umri mdogo...wanaugua magonjwa ya k'zembe kila kukicha yaani gono, kaswende....aisee kweli hii .com
 
Nikweli nilitarajia kukumbana na swali la namna hii, mimi ninasaidia na ninaendelea kusaidia kadiri ya uwezo wangu, vilevile kuwakumbusha kwa maandiko ni sehemu ya kusaidia kuwafungua akili zao!

Binadamu wote tulio chini ya jua daima fikra zetu hufanana kibinadam hivyo sioni ajabu kulitarajia kupata swali hilo; Nimependezwa na jibu lako zuri kama hivyo ndivyo ufanyavyo basi ni jambo la kheri sana na usichoke wala usibague wala usitegemee malipo ya hapa duniani tu"
 
Back
Top Bottom