Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,255
- Thread starter
-
- #21
Rutashubanyuma kwa hilo bed mkipeana migongo ujue matatizo ni makubwa sana, bed zuri kama nn
Rutashubanyuma, naomba nikushauri kwa roho safi tu, ingawa mimi sina taaluma ya ushairi lakini kuna maeneo ambayo kwa uelewa kiasi nadhani unahutaji kuyafanyia kazi. Huwa nasikia kwenye mashairi kuna kitu wanaita vina na mizani, mimi sijui hivi ni vitu gani, maana kama nilivyosema mimi sio mtaalamu wa tasnia hii. lakinnadhani huwa ni ile hali ya sauti kufanana fanana hasa kwenye maneno ya mwisho wa kila mstari nitatoa mfano ili nieleweke:
Yako majina ya vitu, mengine yasiyotajwa,
Yashangaza kuna watu, wenye uovu kujawa,
Waona kuwa si kitu, ni kama wanaolipwa,
Thawabu yako motoni, sikia mwenye matusi.
Mtu sio hayawani, anatumia akili,
Kuboboka hadharani, huwa ni kwake katili,
Matusi siwe kinywani, kama lusu tafadhali,
Thawabu yako motoni, sikia mwenye matusi.
Mdomo wako ni moto, wewe mja nakwambiya,
Wanena mambo mazito, hutaki kuyawaziya,
Ulimi wako ufito, mwilini wateketeya,
Thawabu yako motoni, sikia mwenye matusi.
Haya sasa angalia shairi lako hapa chini:
Mlipoanzana sisi, hatukuwepo kabisa!
Mlipotongozana siye hamkutualika!
Mlipokuwa mkibipiana ilikuwa siri yenu!
Mlipokuwa mkikonyezana mlikuwa pweke!
Mlipoanzana kufukuziana hamkutujuza hata!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?
Mlipowekana sawa sote mlitualika!
Mlipovalishana pete ilikuwa karamu!
Mlipovikana vilemba vya ukoka...........
Mlipotumiana posa si mliniita mshenga?
Mlipomiminiana mizawadi mbona furaha?
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?
Miaka kweli haina subira, hupeperuka tu!
Miaka kweli imesonga tangia uushike ufyagio!
Miaka kweli imetupa kisogo tangia uuteme ukapera!
Miaka kweli imeishia tangia ufue na kusuuza kufuli zako!
Miaka kweli haichelei tangia uunguze kidole gumba jikoni!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?
Ukiangalia tofauti ya mashairi hayo hapo juu utagundua kuwa la kwako lina mistari mitano katika kila beti wakati hilo lingine lina mistari minne, ambayo nadhani ndio sahihi, yaani inakuwa rahisi kuliimba kishairishairi. ukitaka kujua kama shairi lako linaimbika jaribu kuliimba kwa kutumia sauti ya lile shairi maarufu la sungura la sizitaki mbichi hizi.
Sasa hebu ngoja nijaribu kuli editi shairi lako bila kubadili maana yake japo ubeti mmoja tu:
Mlipoanzana sisi, hatukuwepo kabisa!
Mlipotongozana siye hamkutualika!
Mlipokuwa mkibipiana ilikuwa siri yenu!
Mlipokuwa mkikonyezana mlikuwa pweke!
Mlipoanzana kufukuziana hamkutujuza hata!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?
Wakati mkianzana, peke yenu mlikuwa
Ukope mlipigana, penzi lenu likakuwa
Mahaba mlipeana, taarifa hatukupewa
Ya kupeana migongo, ni wapi yametokea
Nawakilisha.
unajua nn watu siku izi hawaangalii life time compatibility bali bed compatibility ndo majanga yanaanzia hapo, sio kila bed mate lazima uoane nae, ukiangalia kitanda ndo ukafanya decision walahi nakwambia mtapeana migongo na kulala mzungu wa nneFranky utashangaa wanaolala hapo ni migongo tu.........na kila siku ni kubweka na lawama.......na suluhu hawatafuti..................................iko shida sana dunia hii..............
View attachment 77406View attachment 77407View attachment 77408View attachment 77409
Hicho ni kitanda chako, hakistahili kupeana migongo, lol
Mlipoanzana sisi hatukuwepo kabisa!
Mlipotongozana siye hamkutualika!
Mlipokuwa mkibipiana ilikuwa siri yenu!
Mlipokuwa mkikonyezana mlikuwa pweke!
Mlipoanzana kufukuziana hamkutujuza hata!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?
Mlipowekana sawa sote mlitualika!
Mlipovalishana pete ilikuwa karamu!
Mlipovikana vilemba vya ukoka...........
Mlipotumiana posa si mliniita mshenga?
Mlipomiminiana mizawadi mbona furaha?
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?
Miaka kweli haina subira, hupeperuka tu!
Miaka kweli imesonga tangia uushike ufyagio!
Miaka kweli imetupa kisogo tangia uuteme ukapera!
Miaka kweli imeishia tangia ufue na kusuuza kufuli zako!
Miaka kweli haichelei tangia uunguze kidole gumba jikoni!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?
Yaelekea sasa umemchoka na humtaki tena!
Yaelekea sasa umegundua kumbe ni chongo tu!
Yaelekea sasa umetambua havielei hivi hata!
Yaelekea sasa umefumbuka macho, hakuna chenga!
Yaelekea sasa mtaani umeonjeshwa asali na manenge!
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?
Zile ahadi na mapochopocho kweli hukumbuki?
Kama kazeeka na wewe je ungali mbichi?
Kama hawaki je na wewe nawe wawaka?
Kama kajiachia na wewe kweli hujioni?
Mbona hivyo walakini wawaka tamaa hivyo?
Yawaje sasa mwapeana migongo,, imekuwaje?
unajua nn watu siku izi hawaangalii life time compatibility bali bed compatibility ndo majanga yanaanzia hapo, sio kila bed mate lazima uoane nae, ukiangalia kitanda ndo ukafanya decision walahi nakwambia mtapeana migongo na kulala mzungu wa nne
Nadhani mkuu Ruta unastahili kuwa malenga wa JF wa mwaka 2012. Hongera sana kwa tunzi zako
duh nimeappreciate mshairi mwenzangu
Power G Nimeona niufunge mwaka 2012 kwa staili hii maana haurudi
tena.......
Da! What a nice poem!
Lukansola labda nianze na swali la kimsingi kabisa......................nani kakuambia haya ni mashairi?
umeona eeeh? hapo ndo inabidi mtu uwe patient in a prowl ili upate the compatible ribs that God removed from you in order to make your Eve,....kuzipata mbavu zako ndo mtihani Mungu alotuletea duniani tuukamilishe kaka RutashubanyumaFranky umepasua bomu.........................yaani bedmate huchomokea kuwa lifemate......................na matokeo yake..............ubedmate wake ukifikia ukomo na hamu nayo imedodomea kabisa...............waishia kupeana migongo.......................it is a tough world...................labda nia huwa nzuri lakini....mvuto na mandhari za awali ndivyo vichochewo vya kukanyagana........
gfsonwin ukipewa mgongo si inaumiza sana...........ehhhhhhhhhhh
Umewalenga wakina nani?
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums