Yawahusu wapangaji

Yawahusu wapangaji

Zogoo da khama

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2013
Posts
638
Reaction score
607
Habari
Kuna hii tabia ya wapangaji kutojishughilisha/ kutoshiriki shughuli za kijamii katika maeneo waliopanga shida nini?

Mtu anapanga lakini hashiriki iwe msiba, harusi, kutengeneza barabara, kuchimba mtaro wa maji anasema hayamuhusu anayehusika ni mwenye nyumba hii iko sawa kweli?

Haya mtaani jamaa kafiwa na mzazi wake maiti ipo mwananyamala hospitali nyumba yote ni wapangaji tupo pia kila mtu na zake, majirani wanapita kafunga turubai ni yeye na nduguze toka jpili leo ndio wanazika, wamepita juu kwa juu toka mwananyamala hadi makaburini, jibu analo, huko FC dada kafiwa na mtoto kapakia maiti kwenye daladala wakagoma, pesa ya kukodi usafiri hana wala jeneza, mtaani wamemsusa kwavile hashirikiani nao, inabidi wana FC waitane kwenda kumfariji na kuona jinsi ya kuzika.

Tunajenga kizazi cha aina gani? Ukiwa mpangaji ndio huruhusiwi kuchangamana na jamii inayokuzunguka kweli, yakikufika utafanyaje?
 
Mtu anapanga lakini hashiriki iwe msiba, harusi, kutengeneza barabara, kuchimba mtaro wa maji anasema hayamuhusu anayehusika ni mwenye nyumba hii iko sawa kweli? Haya mtaani jamaa kafiwa na mzazi wake maiti ipo mwananyamala hosp nyumba yote ni wapangaji tupo pia kila mtu na zake, majirani wanapita kafunga turubai ni yeye na nduguze toka jpili leo ndio wanazika, wamepita juu kwa juu toka mwananyamala hadi makaburini, jibu analo, huko FC dada kafiwa na mtoto kapakia maiti kwenye daladala wakagoma, pesa ya kukodi usafiri hana wala jeneza, mtaani wamemsusa kwavile hashirikiani nao, inabidi wana FC waitane kwenda kumfariji na kuona jinsi ya kuzika. Tunajenga kizazi cha aina gani? Ukiwa mpangaji ndio huruhusiwi kuchangamana na jamii inayokuzunguka kweli, yakikufika utafanyaje?
Kwani wapangaji wamelalamika au nongwa zako tu.
 
Tuna kizazi cha hovyo sana sasa hivi,si cha watanzania wale, huenda hiki kizazi ndiyo kile kilichokaa bweni tangu shule ya msingi, yaani si adabu si maadili,hakina chochote wala upendo kwa ndugu, hakina uzalendo
 
huko FC dada kafiwa na mtoto kapakia maiti kwenye daladala wakagoma, pesa ya kukodi usafiri hana wala jeneza, mtaani wamemsusa kwavile hashirikiani nao, inabidi wana FC waitane kwenda kumfariji na kuona jinsi ya kuzika.
Huko Fc ndio wapi?
 
Tuna kizazi cha hovyo sana sasa hivi,si cha watanzania wale, huenda hiki kizazi ndiyo kile kilichokaa bweni tangu shule ya msingi, yaani si adabu si maadili,hakina chochote wala upendo kwa ndugu, hakina uzalendo
Unataka kusemaje?
 
Mwenye masikio na asikie na mwenye macho na aone.

Na Sio wapangaji tu.
Kijamii inabidi uishi na watu vizur.

Atleast usikose makund matatu/manne ya kijamii unayokaa nayo vizur na kujitoa kwako kwenye shughuli zinazohusu hayo makundi.

Maana naona mara nying huwez kuiva na makund yote yanayokuhusu. Ila tujitahidi 75% ya makund jamii yanayotuzunguka basi tunashiriki kwenye ishu zinazohusu.

Kuna faida nying kuliko hasara.

Hata kama ww ni kijana na hauna familia. Kuna siku utahitaj msaada wa kijamii. Hivyo usipuuzie.
 
Mchawi pesa
Kama unazo, unafunga vioo tu
Kama hana, basi atakuwa anaumwa ule ugonjwa wa wapiga punyeto unaitwa Introvert
 
Tajirekebsha maana mi huwa nakuwa mgumu maana nimepanga na naendelea na ujenz sehem nyngne tatzo kuna mambo unakuta nawaza kesho stakuwepo hapa takuwa sehemu nyngne napo nijiunge na nzengo napo nikienda kwngne huwa nawaza ukiwa kwako ni lazma ujihusishe na hvyo vitu maana n makaz permanent.
 
Hayo ni mambo ya mjini hakukosekani mambo kama hayo watu wapo bize na kufukuzia shilingi.
 
Habari
Kuna hii tabia ya wapangaji kutojishughilisha/ kutoshiriki shughuli za kijamii katika maeneo waliopanga shida nini?

Mtu anapanga lakini hashiriki iwe msiba, harusi, kutengeneza barabara, kuchimba mtaro wa maji anasema hayamuhusu anayehusika ni mwenye nyumba hii iko sawa kweli?

Haya mtaani jamaa kafiwa na mzazi wake maiti ipo mwananyamala hospitali nyumba yote ni wapangaji tupo pia kila mtu na zake, majirani wanapita kafunga turubai ni yeye na nduguze toka jpili leo ndio wanazika, wamepita juu kwa juu toka mwananyamala hadi makaburini, jibu analo, huko FC dada kafiwa na mtoto kapakia maiti kwenye daladala wakagoma, pesa ya kukodi usafiri hana wala jeneza, mtaani wamemsusa kwavile hashirikiani nao, inabidi wana FC waitane kwenda kumfariji na kuona jinsi ya kuzika.

Tunajenga kizazi cha aina gani? Ukiwa mpangaji ndio huruhusiwi kuchangamana na jamii inayokuzunguka kweli, yakikufika utafanyaje?
Mambo ya kishamba
 
Mchawi pesa
Kama unazo, unafunga vioo tu
Kama hana, basi atakuwa anaumwa ule ugonjwa wa wapiga punyeto unaitwa Introvert
Kuna jamaa alikuwa akifika msibani anatoa rambirambi na michango tu huyoo anaenda
siku yalipomfika nae kila mwana nzego anatoa mchaango wake na kuondoka hadi ndg zake wakawaita wazee kuwauliza wale wazee ndo wakasema tabia za ndg yao.

Promondo likalia upya jamaa kajihukumu ng'ombe 2 wakubwa nakuomba msamaha kwa jamii.
Tangu siku hiyo yakitokea yakutokea yeye ndo utamkuta kashafika muda! Amekuwa mdau mzuri wa kutununulia karata hadi pakiti 10 ili tubaki active msibani.

Usiku hukodi wauza kawaha kuja msibani kutuhudumia.Hili ni funzo kubwa sana mkuu.

Nadhani hujawahi fiwa wewe akili hufika mwisho bila msaada wa watu/jamii unaweza wehuka
 
Mbona kwa wazungu msiba ni watu watano mpaka kumi na maisha yanaenda vizuri sana kila mmoja ana uwezo wake wa kimaisha na nchi zao zinazidi kuwa na uchumi mkubwa sana
Haya mambo ya kujazana kwenye misiba yamepitwa na wakati, ni sisi watu weusi tunaendekeza huku wengi wanakuja kula msosi na kutia hasara tu, hawana faida yoyote.
Kwani wakijaa hapo nyumbani ndio marehemu atafufuka, ni ushamba tu.
 
Kwahiyo nawewe umekuwa mzungu?
Wazungu wanatamaduni zao na sisi tunatamaduni zetu. Ndio maana huku hamuwezi kuzika watu3 au6 hasa mkiwa wa familia moja bila kibali maalumu.

Huku msiba ni jambo la kijamii sio la Kifamilia na hat harusi ni jambo la kijamii wewe kama familia ni kutoa mwongozo tu kuwa tunasafirisha au tunazika hapahapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom