mwanamichakato
JF-Expert Member
- Mar 20, 2015
- 1,168
- 1,071
GSM ambayo ni kampuni mtoto katika kikundi cha makampuni ya ALOSCO Holdings wanaomiriki viwanda vya chuma {GSM Steel,Galco-transport,GSM petroleum,GSM Media,Silversands Investments-Real estate,maduka makubwa ya nguo {Msasani City Malls na Pugu Malls}, na pia ndio waliokuwa wamiriki wa Home Shopping Centre sasa Discount Store .Pia kampuni hii ya GSM ndio yenye kuendesha GSM Foundation ambayo imekuwa bega kwa bega na Mh. Makonda katika kusaidia huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo ujenzi wa jengo la Hospitali {Mwananyamala} na misaada ya madawati na vifaa vya ujenzi.
Kutokana na udhaifu wa mikakati ya upanuzi wa bandari ya Dar es salaam ikiwemo kujitanua kieneo kwa kununua maeneo jirani na kuepuka kuuza nyumba zake zilizo karibu na bandari..fulsa ya uwekezaji katika bandari kavu,staffing yards,container yards n.k imekuwa ikikua kwa kasi kwa matajiri wachache wenye kutuhumiwa kubebwa na mifumo ya kiserikali kuchanua na kushika hatamu.
Huku kukiwa na migogoro isiokwisha inayosababishwa na uvamizi wa maeneo ya wazi ama maeneo ya Umma lakini pia viongozi wa taasisi za umma kutumia madaraka yao vizuri au vibaya kugawa maeneo kinyume na utaratibu au kwa upendeleo.Hivi karibuni mwanajamvi ametujuza juu la eneo pembezoni karakana ya Tazara kujengwa bandari kavu inayotangazwa kumilikiwa na kikundi cha makampuni ya Lakeoil..
Kampuni ya GSM wamejenga na sasa wanatumia eneo lilipo mkabala na viwanja vya sabasaba ,na pembezone mwa JWTZ {twalipo},Miaka ya nyuma wengi wetu tulifahamu eneo husika kuwa ni mali ya jeshi hivyo kushangaa matumizi yaliopo sasa japo yawezekana hatukuwa sahihi.Swali kubwa tulilonalo Je hapo kabla eneo lilikuwa likimilikiwa na nani? Je mchakato wa kuuza,kugawa ulikuwa kwa mujibu wa sheria za nchi?