Yanga yatinga fainali Kombe la Shirikisho

Danny greeny

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,856
1,645
yangasc.png

Coastal Union imepoteza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga baada ya washabiki wake kuwa chanzo cha Mwamuzi kuvunja mchezo huo uliofanyika Aprili 24, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana leo (Aprili 27, 2016) jijini Dar es Salaam kwa kuzingatia Kanuni ya 28(2) ya Kombe la Shirikisho. Wakati mechi hiyo inavunjwa, Yanga ilikuwa ikiongoza kwa mabao 2-1.

Pia Coastal Union imepigwa faini ya sh. 2,000,000 (milioni mbili) kwa kuzingatia Kanuni ya 42(26) ya Ligi Kuu kutokana na vitendo vya vurugu za washabiki wake wakati wa mechi hiyo. Pia TFF haitasita kufungiwa uwanja huo iwapo vitendo hivyo vya vurugu za washabiki havitakoma.

Mwamuzi wa mchezo huo Abdallah Kambuzi amefungiwa mwaka mmoja wakati Mwamuzi Msaidizi namba mbili Charles Simon ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi. Adhabu hizo zimetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 38(1) ya Ligi Kuu.

Mchezaji Adeyum Ahmed wa Coastal Union anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa ajili ya hatua zaidi kutokana na kitendo chake cha kumpiga kichwa Mwamuzi wa Akiba baada ya kutolewa nje. Hata hivyo, Ahmed hakufanikiwa kutimiza azma hiyo baada ya Mwamuzi huyo kumkwepa.

Yanga imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa mujibu wa Kanuni ya 14(13) ya Ligi Kuu kutokana na kutoingia vyumbani kwenye mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho.

Vilevile malalamiko ya Coastal Union kutaka mechi hiyo irudiwe yametupwa baada ya Kamati ya Mashindano kubaini kuwa hayana msingi wowote.

SOURCE: http://tff.or.tz/news/article/431
 
Hii game nilitamani sana irudiwe ili tumpige bao za uzalilishaji huyu Coast kama tulivokuwa tumemchapa gongo 8-0 msimu uliopita.
 
Watoto wajeycha oyee...

Kipi kinawafurahisha wakati "jeycha" kafungiwa mwaka mmoja kutokana na maamuzi yake mabovu yaliyopelekea team jeycha kupata huo ushindi?

Team jeycha mkizidiwa kimchezo mkubali matokeo...muwaambie na hao majeycha walijue hilo.
 
duniani kote, mazingira yaliyotokea Tanga , lazima iwe adhabu kwa timu shindwa. Mashabiki walitakiwa wasusie kushangilia na kuondoka uwanjani, halafu viongozi wa timu ya coastal baada ya mpira kulalamika ndo wangekata rufaa. ..na pengine zile dakika 15 zilizobaki wangewafunga Yang's...huwezi Jua...ila timu kubwa ni kubwa tu...mdogo jitahidi kufia uwanjani....ukicheza na yanga acha hasira!!
 
Ninacho washangaa vyura ni chuki na simba.Mechi ilikua baina ya vyura na coast simba sisi tunaingiaje hapo?Acheni ushabiki usio na tija.
 
Tunachojua sisi nyinyi kwa mwarabu bado,ndio maana haka kawimbo cha hallua a.k.a sweet,good etc kaliwaacha na majonzi hadi mkasingizia kujambiwa dawa ya usingizi.
 
Msinijie juu ila hilo neno hapo namaanisha,mlipuliziwa dawa.Tunataka kuona Yanga ya kuibeba Nchi na si Yanga ya kuitusi simba.
 
Yanga raha sana, sijuti kuipenda! mwakani tena timu yangu lazima ipande ndege, kuna raha yake bwana!
 
mabingwa wa tanzania yanga, level zetu ni waarabu,waangola, sio mikia. tunabeba FA,na ubingwa wa ligi, mikia mmetupwa namba 3
Kumbe ndio maana mimi na wewe damudamu namna hii?
Jangwani raha....
Karaha ziko msimbazi
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom