Yanga yamteka Ngoma Airport Dar!

Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,372
2,000
KUNA kitu kinaendelea Dar es Salaam. Leo Jumanne kutakuwa na mchuano mkali baina ya vigogo wa Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, kila mmoja akimwwania Donald Ngoma.

Yanga wamesikia kwamba mchezaji huyo ameshapata ushawishi mkubwa na ameridhia kusaini Msimbazi, ndio maana wameamua kukomaa na leo wamedai kuwa watakinukisha Uwanja wa Ndege waondoke naye kwani amewaambia anarudi Dar es Salaam kwa ajili yao na si Simba.

Lakini Simba na wenyewe wanakomaa kwa vile tajiri yao na wasaidizi wake inadaiwa wamezungumza na Ngoma na amewaambia kwamba leo ndio anasaini kumaliza ishu. Simba wanaamini kuwa wakimtia Ngoma mikononi kwa dakika chache tu wanampa chake na biashara imeisha.

Mchezaji huyo hajasaini popote zaidi ya kuzungumza kwenye simu na kuchat Whatsapp, lakini Simba wamepania kumnasa si tu kuwaziba midomo Yanga, lakini kuboresha safu yao ya ushambuliaji tayari kwa Kombe la Shirikisho mwakani huku Yanga wakifikiria hivyo hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa.

Habari zinasema kwamba Ngoma alikubaliana na Simba mambo mengi, lakini wamepatwa na mshtuko kuwa Yanga inaweza kupindua meza dakika yoyote kwavile wao Simba hawajamtia mikononi. Yanga wanasisitiza kwamba si Ngoma wala Amissi Tambwe anayeondoka Jangwani. Tambwe amerejea nchini akitokea kwao Burundi ambapo juzi alikuwa na kikao kizito na uongozi wa Yanga makao makuu ya klabu hiyo Jangwani.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema: “Ngoma ni mchezaji wa Yanga hadi Julai atakapomaliza mkataba, lakini pia tumeshazungumza naye na tumekubaliana atabaki Yanga na yuko kwenye programu za kocha msimu ujao.

“Tunao wachezaji watatu wa kigeni ambao tutawaongezea mikataba kipindi hiki.”Hata hivyo Mkwasa aligoma kuwataja majina kwa madai kwamba wamewaandalia utaratibu maalumu wa kuwatambulisha.

Hata hivyo, habari za ndani zinaeleza kwamba miongoni mwa wachezaji hao ni Tambwe na Ngoma ambao wako katika hatua za mwisho mwisho za kusaini mikataba mipya ingawa lolote linaweza kutokea kutokana na hali ya kiuchumi kudorora Yanga.

Kiongozi huyo alifafanua hatma ya mchezaji Vicent Bossou kwa kusema: “Bossou hatokuwepo, Yanga ilipenda kuendelea naye lakini tatizo ni mchezaji mwenyewe amekataa kuongeza mkataba.”

Mbali na Bossou, tayari Yanga imeachana na kiungo wake Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, ambaye kulikuwa na tetesi za kushindwana naye kwenye maslahi na Justin Zullu ‘Mkata Umeme’ ambaye hakuwa na msimu mzuri tangu alipotua.

--------------------------------------------------------
UPDATES:
Ngoma atua Dar usiku na kupokelewa na Yanga.
C__Data_Users_DefApps_AppData_INTERNETEXPLORER_Temp_Saved Images_ngoma donald-salehjembe.jpg

Mshambuliaji Donald Ngoma ametua jijini Dar es Salaam usiku huu na kupokelewa na mashabiki wa Yanga.

Ngoma amepokelewa na mashabiki hao wa Yanga na kupelekwa mafichoni.

Baadhi ya wanachama wa Yanga waliofika kumpokea walionekana wako makini na kulikuwa na taarifa kwamba Simba nao walitaka kufika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kumchukua.

Lakini taarifa zilieleza kwamba Simba hawakuwa na mpango huo lakini ni kweli wamefanya mazungumzo na Ngoma.

Leo mchana kuna magazeti yalieleza kwamba Ngoma tayari alikuwa jijini Dar es Salaam akiwa amefichwa na Yanga.

Lakini SALEHJEMBE ikagundua Ngoma hakuwa ameingia nchini kama ambavyo ilielezwa.
 
PAULN

JF-Expert Member
Jan 18, 2011
300
500
KUNA kitu kinaendelea Dar es Salaam. Leo Jumanne kutakuwa na mchuano mkali baina ya vigogo wa Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, kila mmoja akimwwania Donald Ngoma.

Yanga wamesikia kwamba mchezaji huyo ameshapata ushawishi mkubwa na ameridhia kusaini Msimbazi, ndio maana wameamua kukomaa na leo wamedai kuwa watakinukisha Uwanja wa Ndege waondoke naye kwani amewaambia anarudi Dar es Salaam kwa ajili yao na si Simba.

img-20170627-wa0000-jpeg.531448

KickOff.com can confirm that Polokwane City
have completed the signing of Zimbabwean
striker Donald Ngoma.
The 27-year-old has penned a three-year deal
with Rise and Shine after undergoing a medical
with the Premiership side.
Ngoma is set to join the MTN8 participants as a
free agent once his contract with Young Africans
expires at the end of June.
Meanwhile, midfielder Tlou Segolela and veteran
hitman Esau Kanyenda are on the way out of
City, according to a source close to the club
"Ngoma's deal is done. It's a three-year
contract," says the source.
"He was here in the country for a medical
recently and now the paper work has been
done."
 
Mgagaa na Upwa

JF-Expert Member
Sep 30, 2013
6,309
2,000
KUNA kitu kinaendelea Dar es Salaam. Leo Jumanne kutakuwa na mchuano mkali baina ya vigogo wa Simba na Yanga kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam, kila mmoja akimwwania Donald Ngoma.

Yanga wamesikia kwamba mchezaji huyo ameshapata ushawishi mkubwa na ameridhia kusaini Msimbazi, ndio maana wameamua kukomaa na leo wamedai kuwa watakinukisha Uwanja wa Ndege waondoke naye kwani amewaambia anarudi Dar es Salaam kwa ajili yao na si Simba.

Lakini Simba na wenyewe wanakomaa kwa vile tajiri yao na wasaidizi wake inadaiwa wamezungumza na Ngoma na amewaambia kwamba leo ndio anasaini kumaliza ishu. Simba wanaamini kuwa wakimtia Ngoma mikononi kwa dakika chache tu wanampa chake na biashara imeisha.

Mchezaji huyo hajasaini popote zaidi ya kuzungumza kwenye simu na kuchat Whatsapp, lakini Simba wamepania kumnasa si tu kuwaziba midomo Yanga, lakini kuboresha safu yao ya ushambuliaji tayari kwa Kombe la Shirikisho mwakani huku Yanga wakifikiria hivyo hivyo kwenye Ligi ya Mabingwa.

Habari zinasema kwamba Ngoma alikubaliana na Simba mambo mengi, lakini wamepatwa na mshtuko kuwa Yanga inaweza kupindua meza dakika yoyote kwavile wao Simba hawajamtia mikononi. Yanga wanasisitiza kwamba si Ngoma wala Amissi Tambwe anayeondoka Jangwani. Tambwe amerejea nchini akitokea kwao Burundi ambapo juzi alikuwa na kikao kizito na uongozi wa Yanga makao makuu ya klabu hiyo Jangwani.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa alisema: “Ngoma ni mchezaji wa Yanga hadi Julai atakapomaliza mkataba, lakini pia tumeshazungumza naye na tumekubaliana atabaki Yanga na yuko kwenye programu za kocha msimu ujao.

“Tunao wachezaji watatu wa kigeni ambao tutawaongezea mikataba kipindi hiki.”Hata hivyo Mkwasa aligoma kuwataja majina kwa madai kwamba wamewaandalia utaratibu maalumu wa kuwatambulisha.

Hata hivyo, habari za ndani zinaeleza kwamba miongoni mwa wachezaji hao ni Tambwe na Ngoma ambao wako katika hatua za mwisho mwisho za kusaini mikataba mipya ingawa lolote linaweza kutokea kutokana na hali ya kiuchumi kudorora Yanga.

Kiongozi huyo alifafanua hatma ya mchezaji Vicent Bossou kwa kusema: “Bossou hatokuwepo, Yanga ilipenda kuendelea naye lakini tatizo ni mchezaji mwenyewe amekataa kuongeza mkataba.”

Mbali na Bossou, tayari Yanga imeachana na kiungo wake Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, ambaye kulikuwa na tetesi za kushindwana naye kwenye maslahi na Justin Zullu ‘Mkata Umeme’ ambaye hakuwa na msimu mzuri tangu alipotua.
Yan Yanga imteke mchezaji wao wenyewe,mchezaje ambae wao wenyewe wamemtumia tiketi!hz habari za kuzusha nyie mbu3 uwa zinawasaidia nn!ebu waulizeni viongozi wenu zile point za fifa mnarudishiwa lini kwanza
 
Wonderful

JF-Expert Member
Apr 8, 2015
7,372
2,000
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma amehitimisha miaka yake miwili ya kucheza Yanga ya Tanzania, baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Polokwane City ya Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Polokwane, Ngoma mwenye umri wa miaka 27 sasa, amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Na Ngoma anajiunga na timu hiyo iliyofuzu michuano ya MTN8 kama mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wake Yanga ya Tanzania mwezi huu.
Na baada ya kumpata Ngoma, Polo City inawatema kiungo Tlou Segolela na mkongwe Esau Kanyenda.

Ngoma alikuwa na msimu wa kwanza mzuri Yanga SC, akiiongoza kutwaa mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kuiwezesha pia kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ua kutolewa 16 Bora Ligi ya Mabingwa.
Hata hivyo, msimu wake wa pili Ngoma hakuwa mzuri Yanga kutokana na kusakamwa na maumivu ya goti, huku timu yake ikiweza tu kutetea taji Ligi Kuu na kuvuliwa mengine ya Ngao ya Jamii iliyochukuliwa na Azam na ASFC lililobebwa na Simba.
Na hata katika michuano ya Afrika, Yanga haikuweza kurudia mafanikio yake ya msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu hatua ya makundi.
Ngoma aliyezaliwa Kwekwe, Zimbabwe alijiunga na Yanga SC mwaka 2015 akitokea FC Platinum ya kwao, aliyoanza kuichezea mwaka 2012 akitokea Monomotapa United iliyomuibua mwaka 2011.
Amewahi kuitwa timu ya taifa ya Zimbabwe mara kadhaa tangu mwaka 2011na hadi sasa amecheza mechi nane na kufunga mabao matatu.
Na anakwenda Afrika Kusini, huku nchini Tanzania kukiwa kuna habari anakuja kesho kujiunga na mahasimu wa Yanga, Simba.
 
Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,125
2,000
Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe anayeichezea klabu ya Yanga, Donald Ngoma usiku huu ametua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius na kupokelewa na makomandoo wa timu ya Yanga.

Gazeti maarufu, linaloaminika na la michezo nchini Afrika ya Kusini la The Kickoff sikumbuki ni lini limewahi kuandika habari ya uwongo au isiyo na uhakika. Ninavyojua Mchezaji Donald Ndombo Ngoma amesajili rasmi kuichezea Klabu ya Polokwane ya nchini Afrika ya Kusini kwa Kandarasi ya miaka mitatu. Sidhani kama ujio wake ni wa kusaini Yanga FC bali yawezekana amerudi tu kuagana vyema na Klabu yake ya Yanga na kuchukia ' belongings ' zake kisha atimue zake na hata hao ' Makomandoo ' uchwara wa Yanga FC wanaoonekana hapo wanajisumbua tu bure huku wakionekana ni Mapopoma / Wapumbavu wa Kutukuka.
 
mwangalingimungu

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
1,292
2,000
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Dombo Ngoma amehitimisha miaka yake miwili ya kucheza Yanga ya Tanzania, baada ya kukamilisha uhamisho wake kwenda Polokwane City ya Afrika Kusini.
Kwa mujibu wa Polokwane, Ngoma mwenye umri wa miaka 27 sasa, amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na timu hiyo ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Na Ngoma anajiunga na timu hiyo iliyofuzu michuano ya MTN8 kama mchezaji huru, baada ya kumaliza mkataba wake Yanga ya Tanzania mwezi huu.
Na baada ya kumpata Ngoma, Polo City inawatema kiungo Tlou Segolela na mkongwe Esau Kanyenda.

Ngoma alikuwa na msimu wa kwanza mzuri Yanga SC, akiiongoza kutwaa mataji yote matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), au Azam Sports Federation Cup (ASFC) na kuiwezesha pia kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, baada ua kutolewa 16 Bora Ligi ya Mabingwa.
Hata hivyo, msimu wake wa pili Ngoma hakuwa mzuri Yanga kutokana na kusakamwa na maumivu ya goti, huku timu yake ikiweza tu kutetea taji Ligi Kuu na kuvuliwa mengine ya Ngao ya Jamii iliyochukuliwa na Azam na ASFC lililobebwa na Simba.
Na hata katika michuano ya Afrika, Yanga haikuweza kurudia mafanikio yake ya msimu uliopita baada ya kushindwa kufuzu hatua ya makundi.
Ngoma aliyezaliwa Kwekwe, Zimbabwe alijiunga na Yanga SC mwaka 2015 akitokea FC Platinum ya kwao, aliyoanza kuichezea mwaka 2012 akitokea Monomotapa United iliyomuibua mwaka 2011.
Amewahi kuitwa timu ya taifa ya Zimbabwe mara kadhaa tangu mwaka 2011na hadi sasa amecheza mechi nane na kufunga mabao matatu.
Na anakwenda Afrika Kusini, huku nchini Tanzania kukiwa kuna habari anakuja kesho kujiunga na mahasimu wa Yanga, Simba.
Sidhani kama hilo linawezekana. Mchezaji ambaye hajamaliza muda wake wa mkataba hawezi kupimwa afya na kuingia mkataba na timu nyingine bila ya ridhaa ya timu yenye mkataba naye. Anachoweza kufanya ni kuongea tu na timu inayomuhitaji, iwapo muda wa mkataba wake umebakia miezi sita na chini ya hapo. Kama hayo yanayosemwa yamefanyika, na sidhani kama yamefanyika kwa jinsi timu za Ligi ya Afrika ya Kusini zinavyojitambua, basi tayari usajili huo ni batili; ni sababu tosha ya mchezaji na timu hiyo kuadhibiwa na FIFA.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom