Yanga yamsajili Danny Mrwanda!

Yanga yamsajili Danny Mrwanda!

kovai tamil taiga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2013
Posts
1,571
Reaction score
2,192
Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
MSHAMBULIAJI Daniel ‘Danny’ Davis Mrwanda amesaini Mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Yanga SC akitokea Polisi ya Morogoro.
Mrwanda aliyewahi kuwika Simba SC amesaini Mkataba huo usiku huu na amesema mashabiki wa Yanga SC watarajie vitu vizuri.
“Hii ni changamoto kwangu, kusaini klabu nyingine kubwa kama Yanga baada ya kucheza Simba SC wakati fulani, maana yake ninatakiwa kudhihirisha kitu,”amesema Mrwanda akizungumza na BIN ZUBEIRY mida hii.
Mrwanda amesema kwamba Simba SC na Azam FC zote zilifanya naye mazungumzo, lakini hawakufikia makubaliano na baada ya Yanga SC kukidhi matakwa yake, anajitoa kuitumikia klabu hiyo. [TABLE="class: tr-caption-container"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption, align: left"]
Danny Mrwanda akitia dole gumba fomu za Mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Yanga SC usiku huu na picha za chini anasaini na akifurahia baada ya kusaini
​
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Mrwanda kutua Yanga SC ni kutimia kwa ndoto zake, kwani wakati anachipukia kisoka aliwahi kwenda kufanya majaribio ya kuomba kusajiliwa, lakini hakufanikiwa mwaka 2005 na karudi AFC ya Arusha.
Mrwanda, mwenye umri wa miaka 31 sasa, aliibukia AFC ya mwaka mwaka 2003 ambako alicheza hadi 2006 alipohamia Simba SC alikocheza hadi 2009 alipokwenda Al Tadamon ya Kuwait.
Alirejea Simba SC mwaka 2009 na akacheza hadi 2010 alipokwenda Vietnam kujiunga na Dong Tam Long An ambayo aliichezea kwa msimu mmoja kabla ya kuhamia Hoang Anh Gia Lai aliyochezea hadi mwaka huu alipojiunga na Polisi Morogoro.
Baada ya kusaini Mkataba huo, usiku huu Mrwanda anakwenda kujiunga na wachezaji wenzake katika hoteli ya Landmark, Mbeazi Beach kwa maandalizi ya mechi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Simba SC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Sina hakika iwapo huyu naye kama alishawahi kuwa kwenye mipango ya Maximo.Ni nafasi yake naye kuonyesha ukomavu iwapo benchi litamuhusu kama wenzake i.e Kaseja,Nizar,Kiiza na wengine ......!!!!
​
 
Huyu wiki iliyopita, alikuwa anaenda Simba Sijui ikawaje!! Ni bonge la mchezaji alitupa raha sana washabiki wa AFC hatutaisahau!!
 
Huyu mbona ameshazeeka kitambo, anakuja kufanya nini Jangwani?

Katika mzunguko wa kwanza Danny alionyesha kiwango kizuri na kuibeba sana Polisi.Nadhani ni wa kwanza au wa pili kwa ufungaji mpaka sasa.Apewe nafasi aonyeshe kiwango chake, sometimes ukubwa dawa, si unaona Drogba ndio Jembe tena pale Chalsea.
 
Mrwanda ilikuwa zamani kaka lakini sio sasa, nahisi ni Maximo ndiye aliyetowa wazo la kusajiliwa huyu jamaa...

Yanga tayari ina wachezaji wazuri mbele kuliko Danny isipokuwa ni namna ya kuwachezesha tu...

Katika mzunguko wa kwanza Danny alionyesha kiwango kizuri na kuibeba sana Polisi.Nadhani ni wa kwanza au wa pili kwa ufungaji mpaka sasa.Apewe nafasi aonyeshe kiwango chake, sometimes ukubwa dawa, si unaona Drogba ndio Jembe tena pale Chalsea.
 
Kijana wetu Danny tumemtuma kazi maalumu Jangwani.
 
mmh

inawezekana Danny Mrwanda wa Yanga akawa kama Didier Drogba wa Chelsea? Tusubiri tuone.
 
Huyu mbona ameshazeeka kitambo, anakuja kufanya nini Jangwani?

Yanga kusajili wazee ni kawaida yao hebu shabiki yeyote wa yanga anitajie katika first eleven ya yanga ni wachezaji wangapi ambao ni below 30.
 
Mpira wa bongo una vituko kama siasa,ndo maana Yanga wameona aibu hata kurusha magazetini,kimya kimya kama wauza bange
 
Mrwanda ilikuwa zamani kaka lakini sio sasa, nahisi ni Maximo ndiye aliyetowa wazo la kusajiliwa huyu jamaa...

Yanga tayari ina wachezaji wazuri mbele kuliko Danny isipokuwa ni namna ya kuwachezesha tu...

Kweli Kabisa, Atakuwa Maximo Ndio Katoa Wazo Hilo Ili Apate Mchezaji Kama Jaja.
 
Huyu tumemsajili kuwakomoa simba maana tulisikia simba wanamtaka tukaona tuwawashi ili kuwakomoa
 
Back
Top Bottom