Daniel Mbega
JF-Expert Member
- Mar 20, 2013
- 338
- 180
MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Yanga, wanaonekana katika nafasi kubwa ya kukwea pipa kwenda Misri kuvaana na National Al Ahly katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa wataulinda ushindi wao wa mabao 2-1 dhidi ya APR ya Rwanda wakati timu hizo zitakaporudiana mwishoni mwa wiki hii.
Yanga wanahitaji sare tu katika mechi hiyo ya raundi ya kwanza ili kwenda Cairo kukabiliana na timu ya Al Ahly, ambayo mwishoni mwa wiki iliyopita ilibanwa mbavu na C.R.D. Libolo ya Angola mjini Luanda na sasa inataka ushindi wa nyumbani Ijumaa hii Machi 18.
Uchunguzi wa FikraPevu unaonyesha kwamba, timu za Afrika Kaskazini zina kawaida ya kulazimisha hata sare ugenini, lakini daima huwa na kawaida ya kugangamala nyumbani na kupata ushindi, hali ambayo ndiyo inayoonekana hata kwa Al Ahly ambayo inahitaji kurejesha heshima ya kutwaa ubingwa huo wa Afrika unaoshikiliwa na TP Mazembe ya Congo DR.
SOMA ZAIDI...