Yanga yainyima Stars nyota saba

Yanga yainyima Stars nyota saba

Rugby Union

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2012
Posts
402
Reaction score
257
Dar es Salaam.

Huku homa ya mchezo wa watani wa jadi ikipanda, Yanga imewazuia nyota wake saba kujiunga na kambi ya Taifa Stars inayojiandaa na mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Benin utakaofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Stars iliingia kambini juzi kabla ya jana kufanya mazoezi na wachezaji 20, huku wale wa Yanga wakishindwa kuonekana katika mazoezi hayo. Wachezaji wa Yanga walioitwa Stars ni kipa namba moja, Deogratius Munsihi ‘Dida', Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Nadir Haroub na Edward Charles aliyeumia Jumapili dhidi ya JKT Ruvu.

Imedaiwa kuwa uongozi wa Yanga umefikia hatua hiyo mpaka pale itakapopata barua rasmi kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiwaomba kwa maandishi wachezaji hao.

Lakini, habari nyingine za ndani zinaeleza kuwa Yanga wameuchukulia mchezo wa Benin kama wa kawaida, hivyo ungepaswa kuchezwa na wachezaji wengine kwani wao wanakabiliwa na mechi ngumu ya Ligi Kuu dhidi ya wapinzani wao, Simba Oktoba 18. Hivyo wanataka kuanza maandalizi mapema wakiwa na wachezaji wao wote.

Mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga, Seif Ahmed ‘Magari' aliliambia gazeti hili kuwa wachezaji wa Yanga wataripoti muda wowote kwani sheria za Shirikisho la Soka la Kimataifa ‘Fifa' zinasema kuwa wachezaji wanatakiwa kuripoti katika kambi ya timu ya taifa saa 48 kabla ya mechi.

"Mimi sioni kama kuna tatizo , wachezaji wataripoti katika kambi ya Stars kwani sheria zinasemaje, si wanatakiwa kuripoti saa 48 kabla ya mechi? Hivyo muda bado upo, wataripoti hakuna shaka," alisema Magari.

Mwananchi
 
Back
Top Bottom