Yanga yagomea ushindi wa Simba FIFA

Yanga yagomea ushindi wa Simba FIFA

chimwemwe67

Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
69
Reaction score
44
TAYARI kimenuka!

Yanga jana wameliandikia barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupinga ushindi wa Simba walioupata dhidi yao Jumapili iliyopita wakitaka wanyang'anywe pointi tatu na kama TFF itashindwa kufanya hivyo basi wameweka wazi dhamira yao ya kulipeleka suala hilo mpaka Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kutafuta haki yao.

Kikubwa kilichoifanya Yanga kufikia uamuzi huo na kuitaka Simba ipokonywe pointi hizo ni baada ya Simba kumchezesha mchezaji wao, Ibrahim Ajibu mwenye kadi tatu za njano.

Awali kabla ya mchezo huo, Yanga ilituma barua TFF kutaka kujua ni kanuni ipi inamruhusu mchezaji mwenye kadi tatu kuchagua mechi za kucheza wakati ipo wazi kwamba anapaswa kukosa mechi zinazofuata kisha akaendelea na nyingine, lakini ilikosa majibu na ndipo ikaamua kuandika nyingine iliyotumwa jana iliyojumuisha na azimio jingine la Simba kunyang'anywa pointi tatu.

Katibu Mkuu wa Yanga, Dk Jonas Tiboroha, alifafanua kuwa endapo kama wao wangeshinda mchezo huo basi ingebidi Simba wapigwe faini lakini kwa kuwa wameshindwa, basi inapaswa Simba wanyang'anywe pointi tatu ambapo alisisitiza kuwa katika hilo hawatarudi nyuma mpaka wapate haki yao stahiki.

"Tumeandika barua leo (jana) mapema na tayari tumeshaipeleka TFF kuhusu kutaka Simba kupokwa pointi walizozipata kwenye mchezo wetu wa Jumapili kwa kuwa walimchezesha Ibrahim Ajibu, mwenye kadi tatu za njano, kitu ambacho ni kinyume na kanuni za soka zinavyotaka.

"Na kama itatokea TFF watakosa jibu stahiki la kutupa au kushindwa ‘ku-solve' kesi hii, basi sisi tutasonga mbele na tutakwenda Caf (Shirikisho la Soka Afrika) na kama hapo pia itakosa ufumbuzi basi tutafika mpaka Fifa, ilimradi tuhakikishe haki yetu inapatikana.

"Kama ingekuwa tumeshinda sisi siku ile, basi Simba lazima ingepigwa faini lakini kwa kuwa wao wameshinda basi adhabu yao ni kupokonywa pointi tatu, hata mechi zao walizocheza na Stand United na Prisons pia zinapaswa kupokonywa pointi kwa kuwa walikiuka kanuni kama hii.

"Kitu cha kujiuliza ni kwamba kanuni zinawezaje kubadilishwa bila ya wahusika ambao ni timu za ligi, kuwa na taarifa isipokuwa Simba pekee.


Chanzo: GlobalPublishers
 
Duh....hii aibu sana kwa Yanga!
 
Hata issue ya Okwi walisema wataenda FIFA, tupeni mrejesho wa Okwi kwanza! Msitutoe matangani!
 
huu ndo mpira wa Bongo bhanaaa, matokeo washapanga na pesa washagawana, kinachofuata ni siasa kwa kwenda mbele.
 
Siasa za kuwadanganya mashabiki wa yanga hizi na wanazipenda sana, bora sisi yule taleban wetu alikuwa anatukuna tu, lakini watani manji anapiga siasa mpaka wanapiga miayo.
 
Je wangekuwa wameshinda hayo yangetokea?

Huo ufafanuzi wa kuwa na kadi nyekundu na kupewa
ofa ya kuchagua kati ya mechi tatu zinazofuata utaacha/utachze
zipi ni kama umeshatolewa sana na akina baba wanne (Maulid wa Kitenge).

Hapa kinachoonekana ni uchungu wa kufungwa tu.
 
Tatizo walijua timu yao iko kwenye kiwango haiwezi kufungwa na Simba ambao ina wachezaji wengi wa laki mbili mbili. Dakika 90 zimeisha wamechezea kichapo hawaamini kilichowatokea kuanzia viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na hata mashabiki.

Tatizo la watu wa Yanga ni kuamini kwamba timu yao ina kikosi bora kuliko timu zote za ligi kuu kitu ambacho sio kweli. Asilimia kubwa ya wachezaji wetu wa Tanzania viwango vyao havitofautiani sana.
 
Duh....hii aibu sana kwa Yanga!

Namshukuru MUNGU kwa kuniondolea yale machungu niliyokuwa nayapata kila Yanga ilipofungwa! Sasa hivi naona kawaida tu hata kama itafungwa kwenye ndondo cup! Sasa hivi naugua Liverpool ikifungwa kuliko haya mataahira yetu! Ulishaona wapi viongozi wanapiga mdomo utafikiri Kikwe.te anazoza? Juzi hapa TifuTifu imetangaza kuahirisha mchezo wao na Ruvu, yenyewe yanakuja kuropoka eti sisi tunaendelea na msimamo wetu ule ule, sasa nikashangaa badala ya kusema tunakubaliana na uamuzi Wa TFF! She.nzy kabisa hili timu!
 
"Kitu cha kujiuliza ni kwamba kanuni zinawezaje kubadilishwa bila ya wahusika ambao ni timu za ligi, kuwa na taarifa isipokuwa Simba pekee."
Ignorance of the law is no excuse.

Wenzao waliijua kanuni, wao hawakuijua kanuni. Hata hivyo kutokuijua kwao kanuni hakuzuii utumikaji wa kanuni
 
Tushawazoea mbona hawa,kama wasingefungwa Simba wangelipa faini kwakuwa wamefungwa wanataka Simba wanyang'anywe point,poleni watani zetu naona bado mnaweweseka
 
Tushawazoea mbona hawa,kama wasingefungwa Simba wangelipa faini kwakuwa wamefungwa wanataka Simba wanyang'anywe point,poleni watani zetu naona bado mnaweweseka

Simba na Yanga mmefika hapo kweli? Mmefikia kuomba pointi za mezani? Kweli Utani wa jadi kushney! Adabu ni Simba amkung'ute Yanga uwanjani au Yanga amkung'ute Simba uwanjani ndio burdani yetu mashabiki. Hiyo ya kuomba upewe points wakati uwanjani umefungwa ni bonge la aibu aisee!!!
 
timu hazina viwanja mnashabikiaje. mm nilikua mdau wa soka la bongo, ila tangu waanze nunua wachezaji bei, ghali na viwanja hawana nimeacha.
 
Katika records haifutiki ba nimesikia saizi Jerry Murro amekana ingekua aibu kwao
 
Back
Top Bottom