Yanga yabamizwa Bukoba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga yabamizwa Bukoba

Discussion in 'Sports' started by Kaa la Moto, Oct 4, 2008.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Habari zilizopatikana toka Bukoba zinaeleza kwamba Yanga imeumizwa na Kagera Sukari goli 2 bila majibu.
  Wakati huo huo habari zinaeleza kuwa nao Simba nao wamelia kwa Azam goli mbili hizo hizo.
  Ama kweli ni mwaka wa shetani.
   
 2. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #2
  Oct 4, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Klabu kongwe hazikutumia wakati wao vizuri, ili kukabili mabadiliko yanayotekea sasa.......wawaulize wenzao Gor Mahia na AFC Leopards wako wapi sasa.Timu kama Azam inaweza kuwa timu nzuri huko mbeleni kwa sababu sio rahisi kuwa na wachumia tumbo ndani yake bila mwenye mali kuwawajibisha kama zilivyo Yanga na Simba ambapo hata mwanachama asiyetoa chochote anaona ana haki.
   
 3. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #3
  Oct 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Afadhali maana angebamizwa mmoja kati ya Simba na Yanga mmoja angetamba sana
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nimeambiwa mchezo ulikuwa mkali kiasi kwamba kila timu imepata majeruhi wa red card mmoja mmoja.:(
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Oct 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Ha ha ha ha Pole wewe unaelekea ni wa Jangwani ndiyo maana umesema afadhali, mie mpira wa bongo umeshaniboa miaka nenda miaka rudi migogoro kila mwaka hasa Simba na Yanga na hii inachangia sana katika kushusha kiwango cha soka Tanzania. Timu yangu Arsenal karibu tuadhiriwe tena leo lakini dakika za majeruhi tulisawazisha.

  Weekend njema.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Oct 4, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kulikuwa na michezo miwili, unazungumzia mchezo gupi?
   
 7. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #7
  Oct 4, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huu bado ni MWAKA WA MUNGU WETU na si Mwaka wa SHETANI.

  Kubamizwa kwa Yanga na Simba hakubadilishi chochote katika mwaka; Tena maisha ya kawaida ya mwanadamu wa Kitanzania yanaweza yakawa mazuri kuliko yalivyokuwa kabla.

  HATA SIMBA NA YANGA WAKISHUKA DARAJA hadi daraja la tatu hauwezi kuwa mwaka wa shetani, bali utaendelea kuwa mwaka wa Mungu Muumba wa Mbingu na Nchi.
   
 8. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #8
  Oct 4, 2008
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Heshima kwako mkuu..ngoja niende nje ya mada...vipi kuhusu lile goli la Van Persie???,mbona naona kama linesman katubania vile
   
 9. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #9
  Oct 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Hujakosea kabisa!maana Simba walianza kusema Yanga inawahujumu na wakafukuza wachezaji na kuwapa onyo kali wengine!ila bado mambo ni yaleyale
  leo pia wamebamizwa
   
 10. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #10
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  LILE GOLI LA Van Persie naona hamkubaniwa.ni hali halisi mkuu.usjali hata hivyo, YOU WILL NEVER WALK ALONE
   
 11. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #11
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Timu kongwe zinapofungwa na timu changa inaleta utamu japo inauma.afadhali aloanza kufungwa leo kuliko anayeendelea kufungwa.
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Yanga na Kagera sukari
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Oct 4, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ni kweli ni mwaka wa Mungu wetu muumba mbingu na nchi na mwaka wa shetani wa Simba na Yanga.
   
 14. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #14
  Oct 4, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,445
  Likes Received: 7,182
  Trophy Points: 280
  Halafu wewe inaelekea ni SIMBA!maana the way ulivyoweka heading ya thread yako!mimi nilishtuka nikafikiri Simba wamepeta kumbe yale yale tu!Tuambie basi na mechi ya SIMBA VS Azam ilikuwaje?
   
 15. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #15
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Ah,

  Simba pia wamekandamizwa mbili bila!

  :(
   
 16. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mkuu kulia ama kucheka zote ni kelele....
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,661
  Trophy Points: 280
  Marefa naona wana njama za kutufutia magoli yetu, kutunyima penalty tunapostahili au opponent kupewa penalty ya kiushkaji. Inabidi uongozi wa Arsenal uje juu kuhusu hili au marefa wataendelea kutuminya kila mechi. Yule SAF hakosi kulalamika kila siku kuhusu marefa hata kama wao ndiyo waliopendelewa, lakini Wenger huwa hatii neno.
   
 18. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ni kweli lile goli la RvP lilikuwa murwa kabisa.. lakini tukumbuke hata kwenye mechi na Bolton Arsenal ilipewa goli la offside vilevile, hivyo bila bila wakuu.
   
 19. K

  Kenge (Eng) JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2008
  Joined: Dec 7, 2006
  Messages: 502
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nilkuwa shahidi uwanja wa Kaitaba Bukoba, mpira ulitawaliwa na vituko vingi:-.

  1. TBL (Kilimanjaro bia) kutandaza mabango ya matangazo kuzunguka uwanja jambo ambalo Kagera Sugar walipinga kata kata na kudai katika uwanja wao ni VODACOM tu anayetambulika kama mdhamini, hivyo mabango hayo kuondolewa kwa nguvu na uongozi wa Kagera Sugar baada ya TFF mkoa kugwaya na kushindwa kutoa uamuzi hasa baada ya Mwakalebela (TFF HQ) kuwatishia kuwachukulia hatua iwapo watayatoa. Je, TBL ni wadhamini wa Premier Ligi?
  2. Kitendo cha watu ambao walionekana baadaye kuwa ni viongozi wa Yanga kugombea mapokezi ya Refa uwanja wa ndege (Bukoba) na wale waliokuja baadaye kuonekana ni watu wa Simba (Friends Of Simba) kinatia shaka mwenendo mzima wa kukua kwa soka nchini. Kilikuwa ni kituko cha aina yake kwani upande mmja ulifanikiwa kupokea mizigo na upande wa pili kumshikilia refa ambapo Simba walifanikiwa kuondoka naye. (Nisijue kama ilisaidia kwenye matokeo)
  3.Nipasho ya mashabiki wa Kagera Sugar kwa Yanga kabla ya mechi kuwa walizoea kununua magoli na kuonga wachezaji wa timu pinzani jambo ambalo walisema kwamba hapo wamekwama na wategemee kipigo.
  4. Kitendo cha Kagera Sugar kumpeleka nahodha wao Michael Katende kwenye pre match meeting na ukaguzi wa awali uwanjani na baadaye kutomchezesha kwa kumweka bench kama sub. kiliwaumiza vichwa Yanga (habari za ndani za Yanga) kwani kilitibua mikakati ya ushindi wao!!!!!
  5. Mashabiki kumzomea Juma Kaseja aliyekuwa anamuomba kocha kutoka baada ya kufungwa goli la pili na kuimba nyimbo za kumsifu MAXIMO kwa uamuzi wake wa kutomchagua Timu ya taifa hasa kutokana na kufungwa goli la kwanza mpira uliopigwa toka mbali na kushindwa kuuokoa kutokana na ufupi.
  6. Vitendo vya ubabe vya wachezaji wa Yanga (Idd - Chuji) kupigana na mashabiki jukwaani baada ya mechi.
   
 20. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2008
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  This is marvelous and amazing..

  Congratulations to TZ's soccer!!!
   
Loading...