Danny greeny
JF-Expert Member
- Feb 6, 2014
- 3,856
- 1,647
Mabingwa watetezi Kombe la Shirikisho, Yanga wameanza kampeni yao ya kulitetea kombe hilo vizuri kwa kuitwanga Ashanti United kwa mabao 4-1.
Yanga imeitwanga Ashanti katika mechi nzuri kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, leo.
Mabao Mawili ya Mwanzo yalifungwa na Amisi Tambwe na Thabani kamusoko aliyefunga kwa Mkwaju wa Penalt na kuifanya Yanga kwenda Mapumziko wakiwa kifua mbele kwa Magoli mawili.
Yanga iliongeza mabao mengine mawili kupitia kwa Simon Msuva katika dakika ya 54 na kinda Yusuf Mhilu akafunga la nne kwa kichwa dakika ya 89.
Ashanti ilijitutumua na kupata bao moja lakini bado ilionekana kushindwa kuhimili vishindo vya Yanga.