Yanga wana Mwanasheria kweli?

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,084
12,406
Habari za ijumaa wapenzi na mashabiki wa soka nchini Tanzania pamoja na afrika mashariki.

Ikiwa yamepita masaa machache toka kutambulishwa kwa mchezaji aliyekuwa akisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa mpira Tanzania huku hali ikiwa shwari pale jangwani baada ya kuwa na uhakika wa usajili wa Ki Aziz licha ya changamoto mbali zilizojitokeza katika kukamilisha dili hilo.

Sasa twende kwenye mada muhimu:‐

Ukiangalia baadhi ya mambo yanavyoendeshwa pale jangwani kuna vitu vinashangaza sana swali la kujiuliza kila shabiki na mpenda soka kwa sasa nchini Tanzania ni kweli yanga wana mwanasheria?
Mbona mambo yao wanafanya kama team ya ndondo cup maana ni ya kukurupuka tu kwa mfano,

Sakata la Morrison lilivyokuwa kabla hajaenda simba tuliaminishwa kuwa Morrison aliongeza mkataba baada ya ule wa awali kuisha na picha zilisambaa mitandaoni zikimuonyesha akiwa na mwenyekiti wa kipindi hcho kwenye kochi lile lile analotumia kumsainisha kila mchezaji ila mwisho, wa siku taarifa zilikuwa za uongo na picha zilikuwa danganya toto tu hakuna mkataba wowote uliosainiwa na mwisho wa siku Morrison alienda upande wa pili na kesi baadae ilitolewa maamuzi na Morrison alishinda na kulipwa fidia kweli yanga wana mwanasheria?

Kisa cha pili ni sakata jipya lililoibuka la kuahirisha kambi nchini uturuki ambayo ilitarajiwa kuanza kufanyika kuanzia tar 15/07/2022 mpaka tar 04/08/2022 ambapo kutokana na sababu zisizo julikana yanga wamesitisha kuweka kambi nchini humo wakati huo walishafanya bookings ,na sehemu waliyoiandaa kufika katika kipindi chote watakachokua huko na baadae wametakiwa kulipa hela za kitanzania Million 200 kama fidia na usumbufu waliosababisha na bookings waliyofanya kabla kweli yanga ndugu zangu wana mwanasheria?

Sakata la tatu kwenye mechi ya CAF champion's league iliyofanyika Benjamin William mkapa yanga walipewa taarifa kuwa wasiingie mashabiki katika mechi hyo kutokanaila na sheria za Covid–19 badala yake mechi ilipofika mashabiki walikuwepo uwanjani na CAF kuwapiga faini ya, dola 5,000 pamoja na onyo kali baada ya kuwafanyia vurugu viongozi na baadhi ya wachezaji wa Rivers United walipokuja kucheza Tanzania ni kweli yanga wana mwanasheria halafu wanataka kufika mbali CAF si watafilisika kwa faini maana inaonekana hata mikataba wanayosaini wachezaji wake ina shida sema tu ni vile wachezaji wetu wazawa walikimbia umande.

NB: Msipobadilika mtafilisika kwa faini tafuteni mwanasheria mzuri kama yasmin yule wa msuva nawakumbusha tu maana CAF champion's league inaanza muda si mrefu.
 
Na wewe nilishajua huwezi maliza mada bila kumtaja yule Dada wa Msuva.. Yaan mmemfanya very clever kwa kuwa wamebapa bahati ya kulipwa zile pesa..
Mambo ya Yanga waachie wenyewe Yanga na viongozi wao, Mashabiki wake wanataka usajiri wa maana na vikombe tu hyo ndo heshima ya mtaa
 
Back
Top Bottom