Yanga wafungwa 7-1 Uturuki

Yanga wafungwa 7-1 Uturuki

Status
Not open for further replies.
Jana niliwasiliana na mchezaji mmoja wa Yanga alieko Uturuki ambae ni jirani yangu kaniambia walifungwa 7-1 na timu moja ya huko siku ya jumatano ila waliambiwa wasiseme na waandishi wa habari waliambatana na timu wametakiwa wasiripoti. Soka yetu tunamdanganya nani?
Ndio maana mpaka leo Matokeo ya mechi hiyo hayajaripotiwa!! Kweli yebo ni yebo tu.
 
hizi habari huenda ni utani tu wa Simba na Yanga, nilizisikia hata mm wengine wanasema 7-0, wengine wanasema ni safari ile ya kwanza wengine ni safari hii, nadhani ni uzushi tu

kUNA ILE TIMU ILIKULA 12-1 NA PAMBA YA MWANZA
 
aibu tupu (.... ila huu ndiyo uwezo wa Yanga../ila hongereni angalau kwa kufunga goli moja)
 
inaelekea we ni mtalaam wa zengwe sasa fanya basi tukamtoe aden rageee
 
aibu tupu (.... ila huu ndiyo uwezo wa Yanga../ila hongereni angalau kwa kufunga goli moja)

Hata wewe umeingia mkenge na kuiamini taarifa ya mwendawazimu!.....

Unatia aibu mkuu wangu....
 
Mimi si sima damu na nimepitia Page ya Flamurtari na nimeona matokeo ni bila bila sasa sijui kama jamaa wanaweza wadanganya washabiki wao wakati wameshinda, nadhani tuache ushabiki maandazi wa kitoto, JF si sehemu ya kutoa habari za uonga. mod fanya kazi yako
 
Mimi si sima damu na nimepitia Page ya Flamurtari na nimeona matokeo ni bila bila sasa sijui kama jamaa wanaweza wadanganya washabiki wao wakati wameshinda, ...
Umeambiwa mechi ya 7-1 ilichezwa Jumatano, sio hiyo mechi ya juzi dhidi ya Kulafutari, sijui Flamurtari
 
Kuharisha siyo lazima kuwe ni kwa njia ile iliyozoeleka...huku kwa namna hii kama ya mleta hii mada pia ni kuharisha
 
Mada imeanza 'UNCONFIRMED...', kumsakama ni kumwonea, huyu ni mtani! Huu ndio utani wenyewe. Ni kweli Yanga ilicheza siku ya Jumatano na timu ya Altay SK, matokeo yake haya hapa: The Official Website of Young Africans Sports Club angalia pale kwenye 'MORE ARTICLES', poleni sana mliokwazwa na poleni sana kwa mliofurahi kupoza machungu ya 1-0; Mapinduzi Cup na Mtibwa Sugar.
 
Inaonesha walijua kwamba wangefungwa saba, maana mechi zote walizopangiwa kucheza zilikuwa zikitangazwa tangu awali. Hii haikutangazwa tangu mwanzoni, na huyo aiyekuambia hata jina lake haijui. Utakwa ama unajifurahisha kwa kuwafanya Watanzania wote ni mbumbumbn wenzako (hasa hawa wanaokubali bila kujiuliza) au na wewe ni miongoni mwa akina 'akili kuambiwa'!
 
Jana niliwasiliana na mchezaji mmoja wa Yanga alieko Uturuki ambae ni jirani yangu kaniambia walifungwa 7-1 na timu moja ya huko siku ya jumatano ila waliambiwa wasiseme na waandishi wa habari waliambatana na timu wametakiwa wasiripoti. Soka yetu tunamdanganya nani?

Kuna kanga zimeandikwa ''MYAHAKIKISHE NDIPO MYAFIKISHE''...
Ntakununulia
 
Mambo ya kufungwa goli saba hata kama ni ya kweli poa tu.subirin moto kwenye ligi ndipo mtabaini ukweli.
 
Jana niliwasiliana na mchezaji mmoja wa Yanga alieko Uturuki ambae ni jirani yangu kaniambia walifungwa 7-1 na timu moja ya huko siku ya jumatano ila waliambiwa wasiseme na waandishi wa habari waliambatana na timu wametakiwa wasiripoti. Soka yetu tunamdanganya nani?

Hivi karne hii ya internet utawaambia watu msiseme wakati kila kitu kipo wazi? Hiyo itakuwa na website yake na nani atawazuia kuweka hizo habari? Ni vyema kutafakari kabla ya kuandika utumbo
 
Umeambiwa mechi ya 7-1 ilichezwa Jumatano, sio hiyo mechi ya juzi dhidi ya Kulafutari, sijui Flamurtari

Unajua maana ya maneno haya ya Kimombo? Wednesday, 15 January 2014 17:00 administrator News
Hiyo ndiyo Jumatano, Yanga ilicheza na Altay SK na kushinda 2-0, timu isingeweza kucheza mechi nyingine siku hiyo hiyo, 'Penye uongo, ukweli hujitenga'.
 
Kila mara nasema JF imeingiliwa na wababaishaji watu hawaamini matokeo yake ndio haya,hivi kweli JF kwa post kama hizi members tunaweza kujiita Graet Thinkers?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom