Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,462
- 29,159
Kwema Wakuu?
Hii mada kila nikipost jana iliikua inakataa. Jana siku ya Wananchi nilikua naangalia matukio mbalimbali na washikaji wa kitaa ambao tunakuaga nao pamoja siku zote kwenye michezo (mipira, ndondi etc). Sasa mojawapo ya mechi za jana kwenye siku ya Wananchi ni mechi kati ya Staff wa Yanga v/s Wasanii mbalimbali.
Yanga waliwakilishwa na staff mbalimbali wakiwemo waliowahi kuichezea hapo kabla kama Mtwa Kiwhelo, Sekilojo Chambua, Fred Mbuna, Bakari Malima, Mohammed Hussein "Mmachinga", Abdi Kassim "Babi", pia staff wa kawaida kama Eng. Hersi, Ally Kamwe, Abeid Mvuma, CPA Haji Mfikirwa, Wakili Patrick Simon na wengineo.
Wasanii waliwakilishwa na KR Mula, Barafu, Foby, Golikipa H. Kidiaba JR, na wengineo siwakumbuki majina sababu siwafuatiliagi sana. Sasa hii mechi kwa kuiangalia tu utaona Yanga walipaswa washinde nyingi sababu angalau walikua na watu waliowahi kucheza mpira hata kama ni zamani wakati Wasanii wengi hatujui mpira walichezaga au wanachezaga wapi.
Lakini mechi iliisha kwa suluhu ya bila kufungana, kikwazo kikubwa akiwa Golikipa wa wasanii H. Kidiaba JR alieokoa michomo mingi. Sasa unaweza ukaidharau hii mechi sababu ilikua ya kujifurahisha na hata Wachezaji wa Yanga hawako katika ubora wao wa miaka hiyo, wengi tayari miili ishakua mizito (vitambi) ila Golikipa wa wasanii anaujua kiasi chake.
Nimeona nisiache kumpa maua yake huyu jamaa na kama hana timu basi akikazana atapata timu. Aliokoa michomo mingi ya karibu, ya mbali na hata ya krosi. Nimejaribu ku Google nione taarifa zake lakin zinakuja za Kidiaba wa DRC (TP Mazembe) aliekuja kua Waziri. Sijui anatokea wapi huyu jamaa. Msanii mwengine alieisumbua Yanga ni Foby, nae sijui ni Msanii wa nini ila hakua vibaya pia.