YANGA NA SIMBA YAINGIZA SH. MILIONI 390/; A LYON na TOTO siku hiyo hiyo Dar SH.27,000 watu 9

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2]Thursday, October 4, 2012[/h][h=3]*[/h]

Pambano la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.

Watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Umeme sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.

Wakati huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000 imeingiza sh. 27,000.

Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na DRFA sh. 915.2

Kwanini Mechi ya TOTO na A. LYON Ichezwe siku hiyo hiyo YANGA na SIMBA wakicheza ?

Sasa wao waambulia washabiki 9 tu... Jamani, ni Uhalali ?
 
milioni 390!! Rooney na Van persie wanalipwa paundi 250,000 kwa wiki. kweli kambuzi kadogo sana.Mshahara wa rooney/RVP unaingiza washabiki uwanja wa taifa na chenji inabaki.
 
Mbona Dstv walionyesha washabiki uanjani walikuwa zaidi ya 59,000? Hao 9000 hela yao imeliwa?
 
Haki ya nani wamewaonea! Kwa nini wasiwapangie siku nyingine? Hii TFF ina wachumi kweli au ina wachumia tumbo? tumbafu kabisa! Hiyo mechi imeingiza hasara!
 
Thursday, October 4, 2012

*

Pambano la watani wa jadi Yanga na Simba la Ligi Kuu ya Vodacom lililochezwa jana (Oktoba 3 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya bao 1-1 limeingiza sh. 390,568,000.

Watazamaji 50,455 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa usiku kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 30,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 93,345,549.15 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 59,578,169.49.

Mgawo mwingine wa mapato hayo ni posho ya msimamizi wa kituo sh. 240,000, kamishna wa mechi sh. 250,000, waamuzi sh. 591,000, mwamuzi wa akiba (reserve referee) sh. 70,000, usafi na ulinzi wa uwanja sh. 2,350,000 na Wachina (stadium technical support) sh. 2,000,000.
Umeme sh. 750,000, maandalizi ya uwanja (pitch preparation) sh. 400,000, ulinzi wa mechi sh. 5,860,000 wakati tiketi ni sh. 7,327,000. Gharama za mchezo sh. 31,115,183.05, uwanja sh. 31,115,183.05, Kamati ya Ligi sh. 31,115,183.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 18,669,109.83 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 12,446,073.22.

Wakati huo huo, mechi ya ligi hiyo kati ya African Lyon na Toto Africans iliyochezwa Uwanja wa Azam Complex na kushuhudiwa na washabiki tisa kwa kiingilio cha sh. 3,000 imeingiza sh. 27,000.

Mgawo wa mechi hiyo ulikuwa VAT sh. 4,118.6 wakati kila timu ilipata sh. 6,864.3. Uwanja sh. 2,288.1, gharama za mchezo sh. 2,288.1, Kamati ya Ligi sh. 2,288.1, FDF sh. 1,372.8 na DRFA sh. 915.2

Wachina bado wapo tu? Kweli vyuo vyetu vinatoa "vihiyo." Garbage in ......!

Kamati ya ligi wana mgawo wa nini hasa?
 
Dah hapa kazi ipo kwa kweli

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Maskini Toto Africa.Kutoka Mwanza mpaka Dar unaambulia elfu sita?
 
Sio kweli kwamba yanga na simba wameingiza 390 milioni,wameingiza sh 500 milioni,kwa mujibu wa gazeti la super sport lilivyoripoti leo.
 
Wachina bado wapo tu? Kweli vyuo vyetu vinatoa "vihiyo." Garbage in ......!

Kamati ya ligi wana mgawo wa nini hasa?

Hawata ONDOKA; Haujaona ya LUANDA, ANGOLA ? Wamejenga Apartments for Sale... Wanaomwagilia Majani; Safisha

Playgrounds ni Wachina hawataondoka... Waangola Wanalia...
 
Bado kidogo wataanza kufyatua vitu, afrochinese, wadai na uraia kabisa. Hawa jamaa ni hatari kweli.
 
Yeah, Wawekezaji wale wa pale Kariakoo Wengine WanaUraia... Wengine wameweka kinadada wa kwetu na kuwapa yale machupa ya kujichubua na wanakubali kuolewa lakini no SEX... MCHINA anataka tu GAMBA...
 
Maskini Toto Africa.Kutoka Mwanza mpaka Dar unaambulia elfu sita?

Sindio nasema... wangeiahirisha hiyo MECHI... Lakini Wameuza Wachezaji wawili Mmoja UGANDA mmoja ZAIRE
Angalau wanavisenti... na VODACOM inalipa Usafiri, Malazi na Chakula...
 
Nadhani ni busara kupitia tena mgao. TFF na wadau wengine, ukioondoa timu zilizocheza wawekewe ceiling amount, mfano TFF na wadau wengine, kwa pamoja mgao wao usizidi milioni 50 baasi. Ili watafute vyanzo vingine vya mapato badala ya kuwa parasite kwa vilabu.
 
siamini kama Yanga na Simba wameingiza kiasi hicho tu, lakini naamini ni zaidi ya hicho nikizingatia kuwa kiingilio kilikuwa kikubwa-kuna jamaa yangu aliwahi kuniambia kuwa timu hizo mbili zinapocheza, huingiza si chini ya nusu bilioni, na huyu ni mtu wa TFF, sasa kwa uongo huu wa TFF ufisadi hautaweza kumalizika katika nchi hii-yaani upo katika kila sekta, jamani tutaponea wapi? Hata mpirani? Halafu katika hicho hicho kidogo unaambiwa makato kibao, timu zinaambulia kiduchu. Du kazi tunayo watanzania, lakini ipo siku!
 
Back
Top Bottom