YANGA MSITAFUTE MCHAWI

YANGA MSITAFUTE MCHAWI

Kichuchunge

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2020
Posts
425
Reaction score
1,027
Sakata linaloendelea la kuahirishwa kwa mechi ya Dabi ya Kariakoo.
Katika pitapita zangu nimegundua kuwa aliyewaua Yanga hadi haya yote yanatokea, kumbe ni Yanga.
Kivipi? Ukisoma Kanuni ya 36, kuna mtu anaitwa Kamishna wa mchezo.
Kamishina wa Mchezo ndiye mwakilishi Rasmi wa Bodi ya Ligi (TPLB) kwa mchezo husika aliyekasimiwa Mamlaka ya Muendeshaji wa Shindano kwa Mchezo husika ambaye TAARIFA ZAKE kwa mujibu wa Muongozo, Kanuni na Taratibu za Ligi Kuu ndio TAARIFA KUU ZA MCHEZO kwa Muendeshaji.
Kamishna wa Ligi Kuu atatokana na aidha aliwahi kuwa au ni kiongozi wa mpira wa miguu wa ngazi fulani, Mwamuzi mstaafu, Kocha (asiyefundisha timu katika Ligi Kuu/Mashindano ya TFF) au Mchezaji wa zamani aliyepata sifa na kuheshimika au mwanafamilia mwingine wa mpira wa miguu anayeaminika.
Kwa mujibu wa Kanuni ya 36 ibara ya 8; Kamishna wa Mchezo atatoa taarifa mbalimbali na za jumla za mchezo, kwa TPLB akitumia fomu mbalimbali maalum zilizoandaliwa kwa madhumuni husika na kwa mujibu wa muongozo wa Kamishina uliotolewa na TFF ambao unasomeka pamoja na Kanuni hizi.
Ibara ya 11 inasema, Kamishna atawajibika kushughulikia ipasavyo malalamiko (pingamizi) yanayotolewa kabla, baada au wakati wa mchezo pamoja na kukusanya ushahidi unaohitajika utakaosaidia vyombo husika kufanya maamuzi stahili.
Ibara ya 12 inasema Kamishna wa Mchezo anaweza kuishauri TFF/TPLB kuzuia kuchezwa kwa Mchezo katika mazingira ya kabla ya mchezo kuanza endapo atajiridhisha kukosekana kwa usalama kwa timu na maofisa wa Mchezo husika na baada ya jitihada zake za utatuzi wa hilo kushindikana. Endapo mchezo ulishaanza Maamuzi yatakuwa ya mwamuzi wa mchezo huo. Katika Mazingira maalum Kamishna anaweza kushauriana na Mwamuzi endapo hali ya Usalama inatishia Usalama wa timu na maafisa mchezo.
Sasa hebu tujiulize katika mchezo ule wa Dabi ya Kariakoo, Kamishna wa mchezo alikuwa ni nani? Hapa naambiwa kuwa ni Meneja wa Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto. Huyu aliwahi kuwa Ofisa Habari wa Yanga. Mtu wao kabisa.
 
Back
Top Bottom