Kaka unatutafuta,
Pamoja na kuwa amecheza Yanga na kufundisha katika vipindi tofautitofauti kujumlisha na uchungu alio nao kwa Club, lkn bado uwezo wake katika harakati za kuivusha Yanga kuelekea level nyingine ni mdogo sana,tuwaache kina Mwesigwe wafanye kazi yao kwani kuna maombi yaliyoambatanishwa na C.V kama 20 hivi za makocha wa maana,wa humu barani africa excluding Tanzania na wengine kutoka Ulaya na America ya kusini huko ma'brazil nini na ma'nchi mengine yaliyo katika ramani za juu ki'soka,mtatutaka...
Kwani kuwa na kocha mzungu imekuwa fasheni? Mpeni timu Felix minziro analijua soka la bongo na mazingira yetu na anauchungu na timu yetu kuliko hao wahindi
unajidanganya sana kuhusu watu weupe,subiri waje wazee wa 10% kama kina kina Papic. Mwape alikuwa anakosa magori kama taahira lakini alikuwa anamngangania just bcoz of ushkaji na 10 kutoka kwake
Sasa kama Tanzania hakuna wazawa-walimu wazuri wa soka ulitakaje?,makocha wote wa kigeni ndo wamekamatia nafasi 4 za juu katika Ligi iliyomalizika Milovan,Stewart,Papic na Olaba,kati yao hawa wa'3 ni wazungu,unafikiri Yanga ni ya majaribio kama ilivyokuwa Kilimanjaro Stars kwenye Challenge iliyoisha,wazungu watatufundisha sana tutake tusitake.
unakumbuka kuna wakati Simba walikuwa na kocha JULIO,lakini yanga ilikuwa inabadilisha makocha wazungu na bado yanga ilikuwa inafungwa na simba au kukosa ubingwa?!
Vipi tena watani, nasikia mnataka kubomoa timu yetu, mmuchukue Nyoso, Jabu na Uhuru Seleman.
Nyoso ni mzuri lakini washabiki wengi wa Simba hawampendi kwa sababu ya kadi zake za kujitakia, Jabu alitusaidia sana round ya kwanza kipindi hicho Amir ni majeruhi, Uhuru alikuwa majeruhi muda mrefu lakini nilimwangalia kama mechi tatu za mwisho alijitahidi, kama mtawapata tunawatakia kila la heri, mchango wao hasa Nyoso na Jabu ni mkubwa maana wamekaa na Simba muda mrefu wakitokea Ashanti United.Ni mipango tu Masuke usiogope,hadi sasa hivi habari ninazoweza kukuthibitishia kuwa tumeshamweka kwenye himaya yetu Nizar Khalfan,ame'sign mwaka mmoja,tunawapigia hesabu Kinda mmoja wa kulia wa Mtibwa pamoja na Nyoso(I personally dont recommend this),Jabu,Uhuru Selemani pamoja na Mrwanda kuna habari zinasema yupo hapa Town kimyakimya Viongozi wetu wanajaribu kumalizana naye silently,lkn tukifanikiwa kuwapata hasa Uhuru na Jabu wakijumuika na wengine watakaoingia kwenye radar zetu itakuwa bomba sana.