Rugby Union
JF-Expert Member
- Nov 21, 2012
- 402
- 257
Kiungo Haruna Niyonzima 'Fabregas' wa Yanga ameingia kwenye orodha ya wachezaji wanne wa timu hiyo walio hatarini kuikosa mechi ya kwanza ya watani wa jadi, Simba na Yanga msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kesho baada ya kuumia kifundo cha mguu.
Mchezaji huyo wa zamani wa APR ya Rwanda aliyetua Yanga Juni 23, 2011 aliumia enka wakati wa mazoezi ya juzi kwenye Uwanja wa Boko Veterani jijini na kupelekwa nje ya uwanja akiwa amefungwa barafu.
Baraka Kizuguto, Kaimu Ofisa Habari wa Yanga, aliliambia NIPASHE jijini jana mchana kuwa Niyonzima ameungana na majeruhi wengine watatu, mabeki Nadir Haroub 'Cannavaro' na Kevin Yondani pamoja na mshambuliaji Mbrazil Genilson Santana Santos ‘Jaja' ambao pia wako hatarini kuikosa mechi hiyo ya 'heshima' nchini.
Kizuguto alisema wanne hao jana walifanya mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa daktari na ripoti ya kitabibu kuhusu hatma yao kuelekea mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu nchini, inatarajiwa kutolewa leo.
"Ni kweli wachezaji hao ni majeruhi na wanaendelea na mazoezi mepesi chini ya usimamizi wa daktari. Ripoti kamili juu ya afya zao itatolewa kesho (leo) na daktari (Juma Sufiani)," alisema Kizuguto.
Wachezaji wengine wa Yanga wapo vizuri kuelekea mchezo huo wa mzunguko wa kwanza wa VPL. Yanga imeweka kambi Jangwani Beach jijini Dar es Salaam wakati mahasimu wao walirejea jana alfajiri kutoka Johannesburg, Afrika Kusini walipokuwa wameweka kambi tangu Oktoba 8, mwaka huu kuwawinda Wanajangwani hao.
Simba iliyo nafasi ya 10 katika msimamo wa VPL, itaingia uwanjani ikisaka ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuambulia sare katika mechi zote tatu za mwanzo.
Watani wao wa jadi, Yanga walio nafasi ya tatu watasaka ushindi wa tatu mfululizo baada ya kushinda 2-1 katika mechi mbili zilizopita dhidi ya Tanzania Prisons na JKT Ruvu kutokana na kikosi hicho cha Mbrazil Marcio Maximo kuanza kwa kipigo cha 2-0 dhidi ya mabingwa wa 1999 na 2000 wa Tanzania Bara, Mtibwa Sugar.
Nipashe