Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Yanga wamepanga kutuma barua TFF kuhusu waamuzi kutoka nje ya nchi kwaajili ya Derby ya kesho dhidi ya Simba
Wanawasiliana na TFF ili kupata ufafanuzi, kutoa maoni, mapendekezo au malalamiko na wanaamini vilabu vilipaswa kushirikishwa kwasababu ni jambo jipya.
"Nikiri kuwa hatujashirikishwa kwenye maamuzi yaliyofanyika ila kwa kuwa kanuni zinatuelekeza vilabu tukiwa na shida yoyote na waamuzi ni kuwasilisha kwa maandishi TFF basi uongozi wa Yanga utawasilisha hayo maoni, mapendekezo kama kuna malalamiko kwa maandishi TFF."- Ali Kamwe, Afisa Habari wa Yanga SC.
"Taarifa hiyo na sisi tumeiona tu kwenye mitandao ya kijami na Uongozi utakaa chini kulishughulikia hili jambo."
Mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC hapo kesho Jumatano Juni 25,2025 na utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Misri.
Mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Omar, msaidizi namba moja ni Mahmoud Ahmed Abo El Regal, huku msaidizi namba mbili akiwa Samir Gamal Saad Mohamed.