Yanga kumtuza atakayebuni ramani Kaunda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yanga kumtuza atakayebuni ramani Kaunda

Discussion in 'Sports' started by nngu007, May 31, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 31, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  na Juma Kasesa
  UONGOZI wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga, umeandaa tuzo maalumu kwa wasanifu majengo wazawa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kitengo cha ardhi ambaye atafanikiwa kuchora ramani nzuri ya uwanja wao wa Kaunda na jengo la kitega uchumi la Mafia ambako atakabidhiwa na Rais Jakaya Kikwete.
  Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mjumbe wa Kamati ya Uendelezaji Rasilimali za Yanga, Seif Mohamed, alisema wanatarajia kutangaza shindano hilo kwa wasanifu majengo wa chuo hicho, ili kutoa changamoto ya kupata ramani ya kisasa ya vitega uchumi hivyo ambapo mshindi huyo atakadhiwa tuzo siku ya Harambee ya kuchangia ujenzi wa majengo hayo Julai 7 mwaka huu katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam na Rais Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
  Alisema, wanaamini kupitia ushindani huo, wasanifu hao wataweza kushindana kwa kila mmoja kuonyesha kipaji chake ambapo kutakuwa na jopo maalumu la wachambuzi wa ramani hizo ili kumteua mshindi.
  Aidha, Mohamed alisema katika kujindaa na harambee hiyo, kamati yake juzi iliendesha semina kwa makatibu na wenyeviti wa matawi wa Yanga, ili kuwapa mwongozo wanachama na wapenzi wa klabu hiyo namna watakavyoweza kushiriki kuchangia ujenzi huo.
  Alisema, kila mwanachama na mpenzi wa Yanga, atapewa akaunti maalumu ambayo ataweza kuingiza kiasi cha fedha anachomudu ili kufanikisha harambee hiyo ambayo itaongozwa na Rais Kikwete. “Huwezi kusubiri kuchangiwa ikiwa wewe mwenyewe hujajiandaa, ni vyema tukawapa semina wanachama wetu ili nao kama wadau wakubwa wakaweza kushiriki bila kupata usumbufu,” alisema Mohamed.
   
 2. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #2
  May 31, 2011
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Safi sana! washirikishe hata wasanifu majengo walionje ya nchi

  Yanga Imara
   
 3. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #3
  May 31, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  hapo kwenye red umekosea...... chuo kikuu cha dar es salaaam hikitoi wasanifu majengo hao watu wanapatikana ardhi university
   
Loading...