Yanga kuanzia round ya pili CAF? Uongo wa Haji Manara mwezi mtukufu

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,245
103,948
Screenshot_20220420-104751_Chrome.jpg
Msimu huu wa mashindano ya CAF, Simba ya Tanzania ilianzia raundi ya pili ya mchujo. Siyo kwa sababu walikuwa mabingwa wa Tanzania, hapana. Hakuna bingwa wa ligi yoyote anayeanzia raundi ya pili ya mchujo.

Simba walianzia raundi hiyo kwa sababu ya mafanikio yao kwenye mashindano ya Afrika kwa miaka mitano iliyopita. Robo fainali mbili za Ligi ya Mabingwa ziliwafanya wajikusanyie alama 24 na kupanda kwenye viwango vya CAF. Hadi ratiba ya 2021/22 inapangwa, Simba ilikuwa nafasi ya 15 Afrika kwa viwango vya ubora vya CAF 👏👏👏!

Lakini hata hivyo, kwa nafasi hiyo, bado walikuwa hawastahili kuanzia raundi ya pili ya mchujo. Kwa kawaida, vilabu vinavyoshika nafasi 10 za juu kwa ubora ndiyo huanzia raundi ya pili. Simba walifaidika na kushindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwa RS Berkane ya Morocco ambayo ni ya nane.

Nafasi yake ilitakiwa ichukiliwe na aidha Pyramids (11) ya Misri, JS Kabylie (12) ya Algeria na hata AS Vita (13) ya DRC au Kaizer Chiefs (14) ya Afrika Kusini, lakini wote hawa hawakufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa kwenye nchi zao. Hivyo Simba aliyekuwa wa 15, ndiyo akapata nafasi hiyo. “Man Jadda Wa Jadda".

MSIMU UJAO Simba watakuwa nafasi ya 12 kutokana na robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambayo wamefika msimu huu. Alama zao zimeongezeka hadi kuwa 28, na kama watafika nusu fainali wanaweza kujiongezea alama zaidi na kupanda juu zaidi. Na kama itakuwa hivyo, wanaweza kuingia 10 bora na kupata moja kwa moja haki ya kuanzia raundi ya pili ya mchujo.

Lakini kama watatolewa na Orlando Pirates, basi watabaki katika nafasi ya 12 na kuomba zali kama la msimu huu...yaani wa juu yake wasifuzu ligi ya Mabingwa. Na hao ni Pyramids wa Misri na RS Berkane ambao nchi mwao ni ngumu sana kupata nafasi ya ligi ya mabingwa kwa sababu ya ushindani.

Pyramids wana kikwazo cha wale miamba wawili wa Cairo, Al Ahly na Zamalek; na RS Berkane pia wana kikwazo cha miamba wawili wa Casablanca, Raja na Wydad. Kwa hiyo Simba wanayo nafasi nzuri zaidi ya kuanzia raundi ya pili kuliko sisi wengine wa KAWAIDA!😡 Sisi kuanzia raundi ya pili ya mchujo bado sana. Ni hadi tuingie 10 bora ya viwango vya CAF! Anyway, Mwenyezi Mungu ni wa wote!

Credit: Zakazakazi

My Take
Ikumbukwe kuwa Haji alishawahi kuwaita Yanga nzima haina akili isipokuwa Kikwete na Sunday Manara. Huu ni mwendelezo?
 
Jinsi hawa watu waitwao waandishi wa habari bongo wanavyoshindwaga kuwa na follow up questions inafikirisha sana, siku ya kocha wa orlando pirates nilijua labda sababu ya english wakanyamaza kimya wakati maswali ya kumchapa kuhusu upupu alioongea yalikuwepo ya kutosha ila jana msukule albino unaongea utumbo majamaa makanjanja yanacheka tu yanafuurahi yenyewe , he
 
Haya yote ni kwa sababu anayeuliza sio kwamba anauliza kwa ajili ya consumers bali hata yeye hajui. Mwandishi anapaswa kuuliza jambo analolijua na kulifanyia utafiti ili majibu ya anamuuliza yasaidie watumiaji wa huduma
 
Jinsi hawa watu waitwao waandishi wa habari bongo wanavyoshindwaga kuwa na follow up questions inafikirisha sana, siku ya kocha wa orlando pirates nilijua labda sababu ya english wakanyamaza kimya wakati maswali ya kumchapa kuhusu upupu alioongea yalikuwepo ya kutosha ila jana msukule albino unaongea utumbo majamaa makanjanja yanacheka tu yanafuurahi yenyewe , he
Hakuomba kuwa ALBINO, unapomsema mtu basi usitumie ulemavu wake kama shambulio lako. Na ukute eti na wewe umeolewa kabisa na umeshazalishwa lkn huna uchungu kwa watoto wa wanawake wenzako.
 
Hiyo Simba yuko nafasi ya 12 mwaka gani mazee?? Hata 50 bora hiyo timu haipo.

Kielelezo hiko hapo.

Screenshot_20220420-112633_Chrome.jpg
Screenshot_20220420-112700_Chrome.jpg
Screenshot_20220420-112731_Chrome.jpg
Screenshot_20220420-112800_Chrome.jpg
Screenshot_20220420-112824_Chrome.jpg
 
huyu mimi kabisa,unaenda na moto wake. Unadhalilisha wengine halafu wewe uheshimiwe. Hiyo haipo
Kabisa..Hata hapa JF kuna member unatakiwa kwenda na moto wake.

Watu wanajitahidi kulinda heshima yao kwa gharama kubwa, halafu anakuja mtu kwa chuki za kifala anakuporomosha, utakubali vipi..!

Hivi sasa Ahmed Ally anamuita mbana pua, ambayo ni sauti yake aliyojaaliwa na muumba, je hii si Kejeli na Udhalishaji? halafu unataka heshima kwa wenzako inawezekana vipi?
 
Hakuomba kuwa ALBINO, unapomsema mtu basi usitumie ulemavu wake kama shambulio lako. Na ukute eti na wewe umeolewa kabisa na umeshazalishwa lkn huna uchungu kwa watoto wa wanawake wenzako.
Achana na huyo jamaa ni shoga maarufu sana hapa jf ..watu kibao kawafata inbox inahitaji miti.
 
Back
Top Bottom