Yanga ina matatizo makubwa kimataifa

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,802
Ukiitazama Yanga vizuri utagundua kuwa timu inamatatizo mengi ndani ya uwanja kuliko ubora na sifa inazopewa. Kwanini? Naomba unifuatilie kwa makini.

1. Kuwa na mabeki wafupi eneo la kati ni tatizo kubwa. Ukiangalia timu nyingi zinazoshiriki haya mashindano zimejidhatiti kwa kucheza kimbinu ikiwamo kutumia set-peaces(mipira ya kutenga)kupata ushindi. Hivyo wanatumia washambuliaji warefu eneo la mbele. Yanga wameenda kwenye mashindano wakitumia walinzi wale wale wa eneo la kati. Unaweza kuwatumia Job na Bangala kwenye ligi yetu nzima na usiadhibiwe kwa mipira ya juu lakini si kwenye mashindano haya makubwa. Ukiondoa Yanga, timu zingine zote TP Mazembe,Monastery,na AFC Bamaco zote zina watu kweli kweli! Ni mijitu haswaaa! Kocha atake asitake lazima apange walinzi warefu hata km wanamangufu mengine hasa Mamadou na Mwamnyeto. Vinginevyo tutawalaumu bure akina Job.

2. Si sawa Kumtumia Kibwana eneo la kushoto. Unapomtumia Kibwana eneo la kushoto unaongeza idadi ya mabeki wafupi. Lakini pia kwenye kushambulia kibwana si mzuri. Hivyo unapata hasara mara mbili. Ni bora kumtumia Lomalisa mwenye kimo kizuri na tabia ya kupanda kushambulia ukaongeza kiungo wa kumsaidia kukaba.

3. Yanga inakosa viungo wakabaji wenye mapafu ya Mbwa. Aucho hana kasi na kwenye kukaba si mzuri na hawezi kukimbia eneo kubwa la uwanja. Hata Sureboy anashida hiyo hiyo. Mudathiri anaweza kukaba lakini anapiga pasi mkaa nyingi. Msimu ujao atafutwe kiungo mkabaji ila kwa waliopo sioni wa kuziba hili pengo.

4. Ubunifu mdogo na viungo wasio na kasi eneo la mbele. Yanga inakosa viungo wabunifu na wenye kasi eneo la mbele. Kwa namna viungo wa Yanga wanavyocheza kama mpinzani ana mkakati mzuri wa kujilinda mechi inaweza kuchezwa wiki nzima bila Yanga kupata goli. Timu inatabirika kirahisi sana kwenye kushambulia. Hakuna viungo wanaoweza kulazimisha mabeki kufanya makosa. Kimataifa hii ni "disadvantage" kubwa.

5. Mawinga wa Yanga wana kiwango duni. Winga pekee pale Yanga mwenye hadhi ya kucheza kwenye mashindano makubwa ni "Kichaa" Morrison. Twisila na Moloko hawana viwango vya kucheza haya mashindano. Huwezi kuwa na winga ambaye yeye ndo anaongoza kufanya faulo kuliko yeye kufanyiwa faulo.

6. Mipira kupotea kirahisi eneo la mbele. Viungo na washambuliaji wote wa Yanga wanatatizo la ama kupiga pasi mkaa na "poor ball control ". Mayele, Tuisila, Aziz Ki,Msonda, Faridi na Moloko wote wana hili tatizo. Unapokuwa na pasi mkaa nyingi na uwezo mdogo wa kumiliki mpira unakuwa unawasaidia mabeki wa timu pinzani kujilinda. Ndio maana kumkaba Mayele huwa kazi rahisi. Fuatilia mechi nyingi za kimataifa Mayele huwa hana madhara na hugeuka mzurulaji.

7. Kushambulia kwa idadi ndogo. Viungo washambuliaji wanaotakiwa kumsaidia Mayele huwa hawasogei jirani na goli. Hata km Mayele atajitahidi kupambana bado anajikuta yupo peke ake. Sijui ndo mbinu ya kocha au ni uzembe wa wachezaji wenyewe! Hapa ndipo napowapongeza Simba. Simba wakiamua kumtafta mpinzani Shabalala,Kapombe,Sakho,Chama,Bocco na Mzamiru wote utawaona wanaingia kushambulia. Hiki kitu hakipo Yanga.

8. Yanga wanacheza staili moja mwanzo mwisho. Haya si mashindano ya kujisifu kumiliki mpira au kipiga chenga. Haya ni mashindano ya mabingwa kila timu inauwezo wa kuchezea mpira,muhimu ni mkakati wa kukufanya ushinde. Timu zetu za Kitanzania bado zina "mentality" ya kumiliki mpira. Hata tufungwe ngapi utasikia mashabiki wanasema tumeupiga mwingi sana. Wenzetu wameshahama huko na sasa wanacheza kimalengo na kimkakati zaidi. Kila tendo analolifanya mchezaji analifanya kwasababu sio kukimbia kimbia na mpira tu.

Timu haijengwi siku moja. Yanga wamefanikiwa kujenga timu ya ushindani kwa mashindano ya ndani sasa wanatakiwa kutengeneza timu kwa mashindano ya kimataifa. Hizi mechi mzitumie kuona mapungufu na si kufikiria kushindana pekee. Hata Simba nao hawako salama nimeitumia Yanga km reference pointi tu.

Nawasilisha.
 
Jemedari kila siku anawaambia mabeki wenu wa kati wafupi hilo ni tatizo, hamumuelewi, zaidi mnamtupia matusi tu, sasa wacha vipigo viwarudishie akili zenu taratibu.
Viungo warefu kama hawa?
Screenshot_20230213-073317_Twitter.jpg


Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Viungo warefu kama hawa?View attachment 2515691

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
Wanzako wametulia ila we bado jeuri

Wenzako wanaojua kutafsiri mambo saizi wameinamisha vichwa chini kwasababu wanajua ili ubeze vipigo vya namna hiyo inatakiwa usiwepo kwenye hiyo michuano

Waliobeza Simba kupigwa moja, jana walizima data mapema sana, mji ulikuwa kimya, JF ilikuwa kimya nikadhani imehakiwa.
 
Jemedari kila siku anawaambia mabeki wenu wa kati wafupi hilo ni tatizo, hamumuelewi, zaidi mnamtupia matusi tu, sasa wacha vipigo viwarudishie akili zenu taratibu.
Kwani wewe hutoshi kushauri hadi umtaje Jemedari?
 
Wanzako wametulia ila we bado jeuri

Wenzako wanaojua kutafsiri mambo saizi wameinamisha vichwa chini kwasababu wanajua ili ubeze vipigo vya namna hiyo inatakiwa usiwepo kwenye hiyo michuano

Waliobeza Simba kupigwa moja, jana walizima data mapema sana, mji ulikuwa kimya, JF ilikuwa kimya nikadhani imehakiwa.
Simba sasa mmekuwa wachambuzi wa kikosi cha Yanga mnasahau juzi mmepigwa. Kwa Yanga hii ndio ilikuwa mechi ngumu kuliko zote, ni sawa na Raja wanavyowasubiri nyumbani.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom