Jospina
JF-Expert Member
- Apr 19, 2013
- 2,421
- 1,387
Anayevunja mkataba ndiye anamlipa mwenzake wa upande wa pili kwa kuvunja mkataba huo. Tangu itangazwe mpaka leo kupitia vyombo vya habari tunaelezwa Yanga IMEVUNJA MKATABA na mchezaji Haruna Niyonzima na inataka mchezaji ailipe TZS 149 m, a hell of a lot of money! Inakuwaje anayesema "naomba mkataba wetu uishie hapa" ndiye alipwe fidia?
Afisa Habari wa Yanga anasema sababu za Yanga kuvunja mkataba huo na mchezaji huyo ni yeye kutojibu barua ya tuhuma dhidi yake na hivyo Yanga imeona isiendelee na mkataba na mchezaji huyo. Hapo ni wazi Yanga ndiyo kweli wamevunja mkataba na wanastahili kumfidia Haruna aendelee na maisha yake mengine kwa sababu kutojibu barua naamini si kipengee kikubwa (fundamental term) cha kumfanya asiyetekeleza awe amefanya uvunjifu mkubwa (fundamental breach) wa kumfanya atafsirike kuwa amevunja mkataba.
Yanga inavunja mkataba wa mchezaji kipindi ambacho uhamisho bado na hivyo kumfanya asiwe na ajira. Inapaswa imlipe fidia kwani si yeye aliyeamua kuitosa Yanga.
Halafu inakuwaje mkataba wa pande mbili unaingia kwenye mgogoro halafu upande mmoja unageuka hakimu wa kuamua mgogoro huo, unahukumu na kuadhibu? Yanga haina mamlaka kuamua kwamba mchezaji anastahili kuwajibika kulipa mihela mingi kwao kwa mkataba uliovunjika. Hiyo ilipaswa ifanywe na chombo kingine cha kusikiliza kesi ya mgogoro huo na si mmoja wa wanamkataba.
Waandishi wa habari muwe mnauliza maswali yenye changamoto kama haya mnapopokea taarifa kama hiyo ya Afisa Habari wa Yanga. Msiwe wa kupokea na kutuma tu.