Kamgomoli
JF-Expert Member
- May 3, 2018
- 1,865
- 3,802
Wengi walipoona GSM akifanya usajili wa dirisha dogo walizani neema imerudi Yanga na ni mwendo wa shangwe km lote. Nilipomsikiliza Nugaz akihojiwa wasafi Radio kwenye Sport Arena nilithibitisha bila shaka kuwa pale Yanga kuna shida kubwa.
Nilishangaa aliposema wachezaji wote wa Kizanzibar waliokuwa Cecafa hawajaambatana na timu kwa ajili ya michezo 2 migumu ya Mbeya. Pia wachezaji Yondani na Juma Abdul nao hawajaambatana na timu. Mlisho Ngasa nae hatokuwepo kutokana na family matters. Jumla Yanga itawakosa wachezaji 7 muhimu.Kinyume chake wachezaji wa Simba wote waliokua na timu ya taifa wametakiwa kuripoti kambini kujiunga na wenzao mara moja. Zanzibar walitolewa mapema sn je hayo mapumziko waliyopewa wachezaji wa Zanzibar yana sababu gani za msingi? Mbona wenzao wa Simba tena waliocheza mpaka mwisho wameripoti kambini?
Sote tumeona Ngasa anavyolalamikia malipo yake kwenye mitandao huku Nugaz akimjibu Ngasa kwa dhihaka kana kwamba yeye si sawa na Moro alielipwa stahiki zake haraka baada ya kukimbilia kwao. Mi naamini hawa wachezaji wa Kizanzibar watakua wamegoma pamoja kwani wakiwa Uganda nazani walipata muda wa kujadili hatima yao kwa kina na kuamua kutengeneza Solidality ili kushinikiza madai yao. Nugaz anasema waliwapa mapumziko ya siku 3,na sasa ni zaidi ya wiki mapumziko gani hayo. Km ni kweli ni mapumziko basi viongozi wa Yanga watakua hawajielewi na watakua wameshakata tamaa na ubingwa.
Viongoz wa Yanga wanashughulika zaidi na matatizo ya wachezaji wa kigeni kuliko local players. GSM hana lengo la kuondoa matatizo ya Yanga bali anatumia matatizo ya Yanga kupatia umaarufu biashara zake. Ndio maana ananunua wachezaji yeye,anawapeleka kuwatambulisha kwenye ofisi zake yeye mwenyew bila hata kiongozi wa juu wa Yanga kuwepo. Pia Nugaz anajitapa kwamba yeye ndio aliyeenda kumshawishi GSM na yule bosi Sport pesa kusajili wachezaji dirisha dogo. Najiuliza je hayo ndio majukumu ya afisa Muhamasishaji? M/ kiti,Makamu M/kiti na katibu wa Yanga wako wapi na nini faida ya uwepo wao pale Yanga?
Namuona Nugaz akianza kufanya ya Zahera. Mda si mrefu utaibuka mgongano wa maslahi.
Hii ndo Yanga ya Msolwa msomi wa level ya Phd.
Sent using Jamii Forums mobile app